Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

ni takribani miaka 5 tokea nianze kuwa mnywaji wa pombe kali ya korean drama na kadri ninavyoendelea kunywa cha kushangaza satisfaction inaongezeka tofauti na jinsi wachumi wanavyotuaminisha kama kadri unapo consume na satisfaction inapungua.
nahisi umefika wakati wa Damushin kupunguza au kuacha kabisa kunywa ulevi huu mkali ili kuendelea kudumisha afya yake, hivyo basi
  • kuanzia wiki ijayo akipenda Mungu nitakuwa nakunywa pombe chupa moja tu yenye ujazo kama wa chupa ya kahawa, naamini hii ni njia ya kwanza itakayonifanya nipunguze ulevi.
  • nitapunguza kutembelea baadhi ya bar zinazotoa huduma ya ulevi pendwa bila ya malipo yoyote, miongoni mwa bar ninazopenda kuzitembelea ni pamoja na dramanice, kissassian,dramacool, kshow, ikshow na bar nyenginezo.
  • nitapunguza kutembelea baadhi ya kuta zinazotoa matangazo na taarifa zinazohusu kuzalishwa kwa ulevi mpya ambao tokea nianze kunywa nimeshindwa kuachana nao,miongoni mwa kuta hizo ni pamoja na soompi, reddit,dramabeans,alkpop,soompi forum n.k
  • bila ya kuathiri vifungu vya hapo juu nitalazimika kumalizia kreti zangu takribani 40 ambazo nimezihifadhi kwenye store yangu ndipo niache kabisa kunywa ulevi huu pendwa.
  • nitalazimika kuwakimbia walevi wenzangu waliokubuhu kwenye ulevi huu kwani hii ndio njia nyengine itakayonisaidia nisipate taarifa zozote kuhusiana na kuzalishwa kwa ulevi mpya, aigoooo walevi wenzangu naomba munisamehe.
  • kubadili mfumo mzima wa kimaisha ndani ya nyumba hii kama vile kutokutembelea kabisa chumba hichi cha hatari na vile vile nisipokee simu yoyote yenye lengo la kunishawishi kutembelea chumba hichi.
  • je ! haya yote yatawezekana? wakati ambapo ulevi unaoitwa money flower,black knight, hwayugi ndio zinazidi kuninogea
  • EMPTY dongsaeng, aminas, mjr95 na walevi wengineo kama mumegundua njia nyengine japo ya asili ya kuacha ulevi huu basi tupeane taarifa.
  • hiii pombe ya leo imenifanya niwashwe washwe, niwe frustration na kuishia kutamani kukutana na rais wa korea ya kaskazini mwenye namba yake ya simu aiweke humu ndani.
  • mwisho nawaambia walevi wenzangu tuendeleze kunywa ulevi huu wa korean drama hadi hapo wapishi wa ulevi wa bongo movies watakapoweza kutengeneza ulevi wao kwa kiwango cha juu.
  • yote haya niliyoyaandika asilimia (x) nipo kwelini na asilimia (y) natania, hivyo basi wale wazee wa betting waje watabiri asilimia x ni ngapi na y ni ngapi, mshindi atapata nafasi ya kwenda joseon
Usitake kuwa Kama Khantwe .Tuuh
 
Inaitwa Hwayugi
a korean odyssey nadhani itakuwa rahisi zaidi kuitafuta kwenye tovuti
fewtgrt.jpg
 
aigoooo mlevi wewe hunifai nilitegemea utanipa njia nyengine ya kuachana na ulevi huu.
au ndio mlevi hamkatazi mlevi mwenziwe kuacha pombe
Unakumbuka kuna Muda nilijitapa Nataka Acha Izi Mambo Lol!!!
Nimeacha Sasa Ndo Kwanza Nasubiri Nimalize Kitu Flani Ivi Then Nianze Izo Mambo Zile Zilizonipita Nijitahidi Kuziwatch Tena.
Hahahaha Sina Hakika Kiukweli Lol!!

Kwaiyo Ushauri Wangu Ni Usiache Labda Upunguze Kama Utaweza!!!
 
yule mwanamama aliyeimba wimbo wa mazoea yana tabu hakukosea, kupunguza naweza kwa sababu naweza kukaa siku tatu bila ya kuangalia hata episode moja lakini kuacha kabisa ndio siwezi.
kwa mfano nikitembelea youtube hata kama nitafute history zote lakini home itabaki vile vile na masuala ya korean entertainment, matokeo yake naanza tena kuangalia show na nyimbo za kikorea.
nadhani google washanibandika muhuri ya kwamba ni mwanachama wa kudumu wa korean entertainment.
 
Napendaga drama za kibabe
The vegeance
Into the badlands
Ni mkono.mwanzo mwisho
ungelitembelea thread ya wapenzi wa series ingependeza zaidi na inapatikana kwenye jukwaa hili la entertainment, naamini utajifunza na kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na sanaa ya uigizaji kwa nchi za magharibi
nakuomba radhi kama nitakuwa nimekukwaza kutokana na maandishi yangu
 
ni kweli dini haina mahala maalumu pa kuitangaza hii ni kwa sababu mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini ila itapendeza zaidi kama utatembelea jukwaa la dini.
nakuomba radhi kama itakuwa maandishi yangu yamekukera
Hahahahahhaha! Sorry Kwani Iyo ni dini Maana ata Sijaifungua.
 
yule mwanamama aliyeimba wimbo wa mazoea yana tabu hakukosea, kupunguza naweza kwa sababu naweza kukaa siku tatu bila ya kuangalia hata episode moja lakini kuacha kabisa ndio siwezi.
kwa mfano nikitembelea youtube hata kama nitafute history zote lakini home itabaki vile vile na masuala ya korean entertainment, matokeo yake naanza tena kuangalia show na nyimbo za kikorea.
nadhani google washanibandika muhuri ya kwamba ni mwanachama wa kudumu wa korean entertainment.
Uko Mwanachama Na Utabaki kuwa Mwanachama..kuacha Si Rahisi Ndugu

Nina Miaka Sijajua Exactly Mingapi Tangu Nianze Kufutaria Korea Entertainment Lakini Sifikiria kuacha Coz Navitu Bado Nahitaji Kujua,Kujifunza Na Nakupata Buradani Pia.
 
hahahahaaaaaa noona unanichukulia poa?
ili niache kuangalia korean drama pia itanibidi nisisikilize wala kufuatilia korean ost na suala hili nalo gumu sana ila ngoja nijaribu.
ila korean drama ni za kipekee.
 
Mola Akuatangulie Uweze Acha Na Kusahau Kabisaaa InshaAllah.
 
Back
Top Bottom