Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Na dimpozi zake zina kila ishara ya mood aliyonayo muda husika[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Yani nkiri walivoitoa na rangi clear
Yani naona wazuri sana wote
Kuna mbaba katika wale wengi hadi alienda kudai sausage ya kwenye corndog alisema hao wote huwa wazuri eti ninyooshe shingo nisionekane mzee

Nlicheka
 
Kweli ina mapishi na comedy tamu sana
We mwanamke unapenda sana mapishi, ukaona comedy haitoshi lazima ukumbushie na mapishi sio?😂

Hapa Tz kungekuwa na restaurants za Kikorea tungekutuma uende utuonjee mapishi yao kisha utuletee mrejesho.

Me huwa navutiwa na zile snacks zao maarufu (jina limenitoka).
 
😂😂😂😂😂😂ipo huko dar tulielekezwa humu humu ndani ya uzi, ina mapishi yao yoote.sasa sie wa mikoani huku kufika dar mpaka tufiwe na watu wa dar wakifiwa wanatuambia wanakuja kuzika huku😂😂😂😂😂😂
We mwanamke unapenda sana mapishi, ukaona comedy haitoshi lazima ukumbushie na mapishi sio?😂

Hapa Tz kungekuwa na restaurants za Kikorea tungekutuma uende utuonjee mapishi yao kisha utuletee mrejesho.

Me huwa navutiwa na zile snacks zao maarufu (jina limenitoka).
 
Kuna mwingine alidhani ni familia yaan siblings wamefungua biashara ila boss akawaambia wao ni actors kule korea hivyo hawana undugu😂😂😂
Yani nkiri walivoitoa na rangi clear
Yani naona wazuri sana wote
Kuna mbaba katika wale wengi hadi alienda kudai sausage ya kwenye corndog alisema hao wote huwa wazuri eti ninyooshe shingo nisionekane mzee

Nlicheka
 
Jamani Kaka ake careen usimchokoze khantwe wetu ni mstaarabu. Anyway karibu kwa mkapa ushuhudie mpira wa wananchiiii 😂😂😂😂

Sitegemei kumuona Khantwe akikwazika kirahisi namna hiyo.

Kuhusu swala la kukaribia kwa mkapa, nadhani jukumu langu leo litakuwa ni kuwasagia kunguni tu😂😂.
 
Aah kumbe huwa unayatafuta mabango yake makusudi haya mwanakulitaka mwanakulipata

Tukishinda mtaumia sana nawahurumia😂😂😂😂
Sitegemei kumuona Khantwe akikwazika kirahisi namna hiyo.

Kuhusu swala la kukaribia kwa mkapa, nadhani jukumu langu leo litakuwa ni kuwasagia kunguni tu😂😂.
 
😂😂😂😂😂😂ipo huko dar tulielekezwa humu humu ndani ya uzi, ina mapishi yao yoote.sasa sie wa mikoani huku kufika dar mpaka tufiwe na watu wa dar wakifiwa wanatuambia wanakuja kuzika huku😂😂😂😂😂😂

Kwakweli tunakosa vizinsingizio vya kwenda Dar, nimecheka sana😂😂
 
Sad week kwa Scholar Jung[emoji45]


Moment pekee waliyospend as mother & son ni heartbreaking[emoji174]



Wazee wa The Secret Romantic Guesthouse wiki ijayo tunafunga mahesabu
photogrid.collagemaker.photocollage.squarefit_2023510121357524.jpg
 
Mwaka 2018 nilipojiunga Jf nilijua hakuna mtu anajua mambo ya kuhusu Korea kunishinda, pia nilikuwa nimejifunza kusoma na kuandika kikorea, kuhusu kuelewa nilikuwa bado kwenye amateur level. Lakini nilipofika humu ndani, niliona andiko lake, na kuna vitu nilikuwa nadhani navielewa sana lakini Jamaa alikuwa anavielewa zaidi. Nami sikutaka battle nae bali nilijinyenyekeza na kumwambia kuanzia leo nitajifunza mengi toka kwako. Wapo wengine wapo vizuri mno pia wanafanya vizuri, k Hata hawa dada zetu wakuu wakuu(Numbisa n.k). Wewe nimekuona recently.
Anyway watu nilowakuta humu walinifanya niwe humble nakujifunza zaidi.
Huyu Daemusin aliwahi kunipa kitabu cha grammar za kikorea.
Baada ya Daemushin hatimaye nimepata Seoulmate mwingine anayefuatilia Wakorea na kuwaelewa kama kiganja cha mkono wake[emoji23]


Hii nayo ni addiction hata mimi huwa nafuatilia kisirisiri tangu nina miaka 16 enzi hizo 2013 sasa nikihisi Wabongo wengi hawana sana interest siku moja nikakutana na andiko la mwamba[emoji16]
 
Nimeangalia K-drama nyingi za historical zikihusisha
himaya za (Goguryeo,Silla,Baekje,Goryeo,Joseon-hapa ndo za kumwaga-early Joseon, middle Joseon and late Joseon during Japan invansion, pia za Joseon-during independence fighting).

View attachment 2610414

Kitu ambacho kinashangaza hawa wakorea jinsi wanavyo-depict historia yao kwenye maigizo zinaonesha himaya zao zilikua na nguvu sana na wababe sana. Drama nyingi za kihistoria toka Korea zikiachiwa mara nyingi wachina wanalalama wakisema historical kdramas baadhi zinakengeuka na ku-edit baadhi ya matukio halisi ya kihistoria tofauti na jinsi yalivyotokea hapo zamani.

Miongoni mwa himaya za mashariki ya kati na mashariki ya mbali basi;himaya zilizokuwepo ndani ya Korea wakati huo ( Goguryeo, Silla, Baekje, Balhae,Goryeo na Joseon) kwenye historia inaonekana zilikua himaya dhaifu kwa sababu :

1. Mgawanyiko ulikua mkubwa katika utawala. Wakorea ni watu wanaopenda kuwa katika makundi makundi ya ukabila, koo na kikanda hali iliyopelekea kukosekana kwa umoja miongoni mwao hivyo kuwa dhaifu na kupelekea kupigwa kirahisi na maadui zao.

✓Mfano China alitumia mbinu ya kuungana na Silla akampiga Goguryeo
na Baekje na kwa mfuatano na kuzi-conquer hapo ikaundwa Goryeo (Unification of the three kingdoms).

✓Joseon kulikua na mpasuko mkubwa ilikua kila baada ya muda wanapindua wafalme wao na kuweka wengine madarakani mvutano ukihusisha factions zenye mrengo tofauti kama (Sarim,Seo-in,Dong-in,So-ron,No-ron).

View attachment 2610132

✓Hali hii imeendelea hadi karne ya 20 na 21 baada ya uhuru nchi imejigawa kuwa Korea ya kaskazini na kusini. Tangu zamani wenyewe ni wazee kuungana, kusalitiana, kupigana kisha kutengana.

2. Himaya za zamani za Korea zilipigwa na zikatawaliwa na karibia kila himaya mbabe wa enzi hizo.

✓Kwanza walisumbuliwa na himaya za China ya Wakati huo zikiwemo (Han, Ming,Liao/Khitan,Yuan,Tang na Qing,Jin).

Hizi himaya zilipigana vita kwa vipindi tofauti tofauti na himaya za Korea na baadhi zikafanikiwa kuwatawala wakorea na kupelekea wafalme wa korea kuongoza nchi kama vibaraka/viongozi kivuli hivyo kukosa maamuzi ya mwisho kama watawala.

✓Katika nyakati hizi watawaliwa walitumia lugha ya kichina katika kuandika, wakaletewa dini ya buddhism, na mfumo wa kuongoza falme zao ulifanania sana na mfumo uliokuwepo China.

✓Hapa drama nyingi zimeonesha hili zikiwemo Emperor of the sea na Chuno/Slave hunters.

View attachment 2610154

✓Korea ilitawaliwa na Japan 1910-1945. Hili lilitokea juzi tu hapo dunia ikiwa imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika nyanja za teknolojia na viwanda.
✓Japan alikua ameendelea sana kipindi hicho. Kulinganisha Japan na korea ilikua kama mbingu na ardhi.
✓Kilichowaokoa kutoka katika huu utawala ni pale Japan aliposhindwa katika vita kuu ya pili dunia hivyo Korea wakapata uhuru wao 1945.

Drama zilizoonesha kwa uzuri maisha halisi yalivyokua Joseon chini ya utawala dhalimu wa Wajapan ni pamoja na The Land (Toji), Mr Sunshine na Pachinko.
zikionesha (mateso, manyanyaso, umaskini,mauaji ya wazalendo, mapambano ya kudai uhuru, wanawake wakisafirishwa kama watumwa)

View attachment 2610155View attachment 2610156View attachment 2610157

✓Wakorea pia walipigwa na Wamongolia (himaya ya Yuan) . Mongol (Yuan) chini ya mtaalamu Genghis Khan mnamo karne ya 13-14 ilikua himaya yenye nguvu sana Asia na ilipenda vita. Yaani huyu mpuuzi Genghis Khan alikua mbabe sana kila akiamka asubuhi yeye anawaza kutanua tu mipaka ya falme yake na alifanikiwa kuitanua Mongol kwa kiasi kikubwa wakati wa utawala wake kwa kuzipiga himaya nyingi na kuzitawala.

View attachment 2610408

✓Mongolia wakati huo ilikua ya moto iliitawala China, ikaitawala Korea, ilipigana vita na kuzi-conquer himaya kama Ottoman,India,Serbia,Poland, Bulgaria, Croatia, Hungary na Japan na ilishinda katika vita walizopigana na kutanua mipaka yake kuifanya Mongolia kuwa himaya yenye nguvu sana mshariki ya kati na mashariki ya mbali kwa wakati huo.

View attachment 2610409

✓Nikiwaangalia Wamongolia sasa hivi walivyo masikini nikalinganisha na ubabe waliokua nao zamani nashindwa kuelewa imekuaje wamepooza hivi!!!!

View attachment 2610411

✓Yuan dynasty (Mongol) chini ya mtoto wa 3 wa Genghis Khan aitwae Ögedei Khan iliingia vitani na himaya ya Goryeo na kujaribu kuitawala kwa vipindi tofauti katika karne ya 13 ikifanya uvamizi mara kwa mara takribani mara tisa (9) na baadae ilishinda vita na hivyo Goryeo ikatawaliwa na Mongolia (Yuan dynasty).

View attachment 2610410

✓Utawala na Vita ya Mongol (Yuan) dhidi ya Goryeo imeoneshwa kwenye drama ya Empress Ki.

View attachment 2610399

✓Himaya za Korea kwa vipindi tofauti zimeingia vitani dhidi ya Han,Qing, Tang, Ming,Japan, Mongol,Jurchens ,Khitans nk kwa vipindi tofauti tofauti.

✓Kitu kinachoshangaza kwenye Drama za wakorea tunazoangalia zinaonesha Korea lilikua dude kubwa ikiwa na watu-watu kweli wababe wa vita na wajuzi wa elimu ya siasa na sayansi ya ulimwengu waliopikwa kutokea Sungkyunkwan.

View attachment 2610401

✓Historical figures walioshiba wamepambwa wakiwemo miamba kama Queen Seondeok,Lady/Empress Ki,mwanasayansi Jang Yeong-sil, Daemusin Muhyul, Jumong, General Yi Seong-Gye (King Taejo), Warrior Yi Bang-Ji, Yi-San (King Jeongjo), King Gwanggaeto, King Geunchogo,Yi Do (Sejong the great), General Choi young, General Kim Yushin, General Gye-Baek, Kim Suro, Bidam,Great scholar Jeong Do-Jeon (Sambong). Jang Bogo, King Yeongjo, Shin Sa im dang nk

View attachment 2610136
View attachment 2610139

✓Drama zinaonesha himaya za korea zilikua zimeendelea kimapigano na hivyo kupelekea kushinda vita nyingi, Pia zinaonesha korea ilikua imestaaribika na ni jamii bora kimavazi na vyakula, pia inaonesha kielimu ilipiga hatua kiasi ya Sungkyunkwan kutoa scholars wengi waliochonga mfumo wa uongozi wa vizazi na vizazi katika Joseon na baadae Korea ya Sasa.

View attachment 2610413

∆Je, hawa wataalamu hawatufungi kamba kweli? na kuikuza historia ya nchi yao tofauti na uhalisia ulivyo? Sababu historia inaonesha yeye(Korea) ndiye aliekua kibonde wa wote akisumbuliwa na majirani wa karibu na wa mbali.

View attachment 2610138
Hii imekaaje?
Gwanggaeto the Great
Japan angeshinda vita ya pili dunia ingekua kakamavu sana
 
Back
Top Bottom