Kwa watu makini, adui wa Chadema sio Samia na CCM, na wala adui wa CCM sio Lissu na Chadema; nyote mna adui mmoja - Wanamtandao!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Kuna kitu kimoja wanamtandao wamefanikiwa sana kuchezea akili za watu wa CCM na Chadema. Wamewafanya wajione kuwa ni maadui wa kufikia hata kuuana.

Sijui lini haya makundi mawili yatatambua kuwa yanakuwa playe dhidi ya mmoja na mwenzake. Na siku makundi mawili haya yakitambua hilo, basi matatizo yote ya nchi hii yatakwisha.

Kwa mfano, wengi wa watu wa Chadema wanaamini serikali chini ya CCM ndio inafanya matukio ya utekaji na uuaji. Si sahihi. Sio rahisi mtu kama Samia kuwa na ujasiri ndani ya moyo wake wa kuamuru watu watekwe na kuuwawa. Lakini hana uwezo wa kuzuia hili. Hili kundi lime-ingilia sana serikali, kwa kutumia wastaafu na walio kazini, kiasi kwamba ndilo linaamua mambo yote haya. Hakuna anaeweza kupinga wala kuzuia - hata Samia mwenyewe.

Kundi hili limeingilia si serikalini tu, bali hata vyombo vya sheria kama mahakama, Polisi na hata Uslalama wa Taifa. Wanachotaka ndicho kinakuwa.

Sasa ni wakati Watanzania kuanza kutambua kwamba nchi ina adui mmoja mkubwa sana, mwenye nguvu za utajiri na uwezo mkubwa, na adui huyo si CCM wala Chadema - ni Wanamtandao.

Tanzanians, stop being blind - unite to face your common enemy, Wanamtandao!
 
hivi huwa ni ngumu kiziwi kusikia alarm ya asubuhi?
 
Polepole nadhani bado hajatambua kuwa si juu ya Samia kuamua nini kifanyike, na yeye anaambiwa nini afanye. Hapo ndio tatizo lipo Siku hizi kuna spika za kuchaji kuna vipaza sauti za kuchaji na kurekodi inatakiwa iandaliwe strategy ya kurekodi sauti kuelewa wanamtandao wakina na nani kwa jinsi wanavyotafuna nchi unaenda kupeleka vijijini ndani ndani wasio jua Kiswahili mnarekodi kwa lugha za kwao hapo wananchi wote wakijua adui yao basi
 
Na ndo adui wa Taifa kwa ujumla Asante sana
Unajua, kabla ya kuwa raisi, Samia alikuwa mdada mmoja mtundu mtundu hivi, wa kuvaa suruali na hana habari na kuvaa mitandio. Alikuwa mtu wa story sana na kinywaji mtapiga nae kwa sana tu. Wale walioshiriki zile marathon za kutafuta maoni ya katiba mpya watakueleza undani wake. Sasa swali la kujiuliza ni moja; Wanamtandao wamemshika pabaya kiasi kwamba hawezi kufurukuta?
 
Kuna kitu kimoja wanamtandao wamefanikiwa sana kuchezea akili za watu wa CCM na Chadema. Wamewafanya wajione kuwa ni maadui wa kufikia hata kuuana.

Sijui lini haya makundi mawili yatatambua kuwa yanakuwa playe dhidi ya mmoja na mwenzake. Na siku makundi mawili haya yakitambua hilo, basi matatizo yote ya nchi hii yatakwisha.

Kwa mfano, wengi wa watu wa Chadema wanaamini serikali chini ya CCM ndio inafanya matukio ya utekaji na uuaji. Si sahihi. Sio rahisi mtu kama Samia kuwa na ujasiri ndani ya moyo wake wa kuamuru watu watekwe na kuuwawa. Lakini hana uwezo wa kuzuia hili. Hili kundi lime-ingilia sana serikali, kwa kutumia wastaafu na walio kazini, kiasi kwamba ndilo linaamua mambo yote haya. Hakuna anaeweza kupinga wala kuzuia - hata Samia mwenyewe.

Kundi hili limeingilia si serikalini tu, bali hata vyombo vya sheria kama mahakama, Polisi na hata Uslalama wa Taifa. Wanachotaka ndicho kinakuwa.

Sasa ni wakati Watanzania kuanza kutambua kwamba nchi ina adui mmoja mkubwa sana, mwenye nguvu za utajiri na uwezo mkubwa, na adui huyo si CCM wala Chadema - ni Wanamtandao.

Tanzanians, stop being blind - unite to face your common enemy, Wanamtandao!
Sidhani kama kuna ukweli hapa.

Kujaribu kutenganisha CCM (chama dola) na hao unaowaita "wanamtandao" inaweza kuwa aina ya njozi (illusion) ili kujipa faraja kiaina tu (convenience).

Mwaka 2014, Kikwete alibanwa na wanamageuzi akafikia hatua ya kukubali marekebisho ya katiba yafanyike. Ikaundwa Tume ya Warioba iliyokuja na mapendekezo yake. Pendekezo kubwa lilikuwa kupunguza au kurekebisha madaraka ya Rais ili kuwe na uwanja sawa wa kisiasa kati ya CCM na vyama vingine vya siasa, na kiutendaji kati ya muhimili wa serikali, dola na mihimili ya bunge na mahakama. Kwamba Rais atimize majukumu yake akizingatia katiba na sheria za nchi kikamilifu.

Kulitokea mtafaruku mkubwa sana ndani ya CCM. Wengi walifikia hatua ya kudai "kofia" ya uRais wa JMT itenganishwe na ile ya Mwenyekiti wa CCM kwa vile waliona Kikwete kalegea sana na kupwaya kiasi cha kuweza kupelekea chama kumfia mikononi mwake. Hawakuwa tayari kabisa kuona dola ikitenganishwa na CCM wala madaraka ya Rais na Mwenyekiti wa CCM yakirekebishwa. Aidha, hawakutaka kuona Muungano "ukilegezwa". Hao wana CCM huwezi kuwaita wote wanamtandao. JK ndiye anayetambulika kama "mwanamtandao". Lakini ndiye aliyekuwa akishambuliwa na wana CCM wengi kwa kule tu kujaribu kuruhusu mageuzi kuimarisha haki na usawa nchini.

Magufuli alipoingia madarakani 2015, masuala ya katiba na tume huru ya uchaguzi akayatupilia mbali na kutumia vyombo vya dola moja kwa moja kuiimarisha CCM na kudhoofisha upinzani. Wana CCM wakamshangilia sana kama "mkombozi" wao aliyewanusuru na fedheha za siku kwa siku na kuwawezesha kuvaa kijani zao hadharani bila hofu ya kuzomewa. Ulinzi wa polisi ulikuwa ukiwahakikishia kutozomewa na magwanda yao 24hrs! Magufuli hakuwa mwanamtandao. Lakini alikamata dola na nyenzo zake kisawa sawa na akazitumia kama alivyotaka. Iwe kudhibiti bureau de change au kusomba korosho au kujenga majengo ya serikali, au ...

Sasa kama kweli unaamini nje ya "wanamtandao", CCM wanaweza kukubaliana na NRNE ya CHADEMA, kila la heri.
 
Screenshot_20250823-084911~2.png
 
Unaongelea vipindi tofauti. Kwanza wakati huo wanamtandao hawakutishiwa na katiba kiasi hicho.
 
na kubwa lao ni huyu Muajemi, akiondoka huyu ni kama tutakuwa tumeshinda pa kubwa sana,
 
Huwezi tenganisha CCM na Wana Mtandao,maana hao ndo watoa pesa za kugharamia shughuli za chama,ni wazi kwamba katika makundi yenye kugombania madaraka huko katika chama chenu kundi hili ndo lenye nguvu kwa sasa,hivyo ni mwendo wa kubuluzwa tu.

Walio shangilia kubuluzwa kwa vyama vya upinzani katika kipindi cha JPM ndo wale wale sasa wanalia kubuluzwa huko kwenye chama Chao.

Alafu hii ni thread yako ya pili sasa nasoma, Kuna kitu unakigusia juu juu tu kuhusu Rais Samia kushikwa pabaya na hao wanamtandao (CCM) ni kitu Gani hicho ebu kiweke wazi,maana Uzi mwingine ulitaja mfano wa Putin na Trump.
 
na kubwa lao ni huyu Muajemi, akiondoka huyu ni kama tutakuwa tumeshinda pa kubwa sana,
Muajemi hawezi fanikisha mipango yote bila kupata support toka kwa Wana CCM,ni Sawa na wezi wa kura katika chaguzi kule Zanzibar, Wazanzibar hushirikiana na Watanganyika,lakini katika kujitoa kwenye lawama huwapa Watanganyika lawama k
 
Unaongelea vipindi tofauti. Kwanza wakati huo wanamtandao hawakutishiwa na katiba kiasi hicho.
Sijui mwelekeo wako na malengo yako hasa.

Ninachojua, wale wote wasiotaka kabisa uwezekano wa CCM kupoteza madaraka ya uRais ikiwa ni pamoja na kupoteza mamlaka kamili ya Rais (absolute power) ni maadui wakubwa wa mageuzi nchini. Hawa ni watu wasiotaka kabisa marekebisho ya katiba yanayoitenga CCM na dola na kuisawazisha na vyama vingine vya siasa. Wanamtandao wamo katika kundi hilo. Hawataki kupoteza fursa ya kumiliki uchumi wa taifa. Lakini pia wana CCM wengi huo ndio msimamo wao - chama chao kuendelea kuwa chama dola.

Sasa ukisema dai la marekebisho ya katiba halikuwa tishio kwa wanamtandao "kiasi hicho" nashangaa. Ninachojua enzi hizo, hawakuwa na ujasiri sana wa kutumia vyombo vya dola kutishia wapinzani na wakosoaji. Vyombo vya habari vilikuwa huru kuripoti scandals kubwa kubwa kama za Escrow, EPA, Richmond, Rada, n.k.

Enzi hizo Kikwete hakufikiri kuwa anaweza kuzima mjadala wa katiba mpya kwa nguvu za dola kama alivyofanya Magufuli kwa jeuri kubwa, kutishia media, na kuzuia shughuli zote za kisiasa asizotaka. Kikwete na wanamtandao walikuwa bado na "haya" kufanya hayo. Baada ya awamu ya tano kufungua milango ya ujasiri ndio sasa sura halisi ya wanamtandao na wote wasiotaka mageuzi inajitokeza wazi.

Bila marekebisho ya katiba, tume ya uchaguzi na sheria zake, urafiki kati ya CHADEMA na CCM utabakia wa mashaka - wawepo wanamtandao au wasiwepo.
 
Wana CCM na CHADEMA pamoja na Watanzania wenye uzalendo na nchi yao waungane kudai Haki kwa wote! Piga chini wanamtandao maana wapo kila mahali. Kwenye vyama vya siasa hadi taasisi za dini.
 
Kuna kitu kimoja wanamtandao wamefanikiwa sana kuchezea akili za watu wa CCM na Chadema. Wamewafanya wajione kuwa ni maadui wa kufikia hata kuuana.

Sijui lini haya makundi mawili yatatambua kuwa yanakuwa playe dhidi ya mmoja na mwenzake. Na siku makundi mawili haya yakitambua hilo, basi matatizo yote ya nchi hii yatakwisha.

Kwa mfano, wengi wa watu wa Chadema wanaamini serikali chini ya CCM ndio inafanya matukio ya utekaji na uuaji. Si sahihi. Sio rahisi mtu kama Samia kuwa na ujasiri ndani ya moyo wake wa kuamuru watu watekwe na kuuwawa. Lakini hana uwezo wa kuzuia hili. Hili kundi lime-ingilia sana serikali, kwa kutumia wastaafu na walio kazini, kiasi kwamba ndilo linaamua mambo yote haya. Hakuna anaeweza kupinga wala kuzuia - hata Samia mwenyewe.

Kundi hili limeingilia si serikalini tu, bali hata vyombo vya sheria kama mahakama, Polisi na hata Uslalama wa Taifa. Wanachotaka ndicho kinakuwa.

Sasa ni wakati Watanzania kuanza kutambua kwamba nchi ina adui mmoja mkubwa sana, mwenye nguvu za utajiri na uwezo mkubwa, na adui huyo si CCM wala Chadema - ni Wanamtandao.

Tanzanians, stop being blind - unite to face your common enemy, Wanamtandao!
Nkweli
 
Mkuu sasa tunafanyaje?
Maana Malalamiko yamezidi kuliko kutafuta solution!
Unapendekeza tuanzie wapi kuwaondoa hao wana Mtandao?
 
Sidhani kama kuna ukweli hapa.

Kujaribu kutenganisha CCM (chama dola) na hao unaowaita "wanamtandao" inaweza kuwa aina ya njozi (illusion) ili kujipa faraja kiaina tu (convenience).

Mwaka 2014, Kikwete alibanwa na wanamageuzi akafikia hatua ya kukubali marekebisho ya katiba yafanyike. Ikaundwa Tume ya Warioba iliyokuja na mapendekezo yake. Pendekezo kubwa lilikuwa kupunguza au kurekebisha madaraka ya Rais ili kuwe na uwanja sawa wa kisiasa kati ya CCM na vyama vingine vya siasa, na kiutendaji kati ya muhimili wa serikali, dola na mihimili ya bunge na mahakama. Kwamba Rais atimize majukumu yake akizingatia katiba na sheria za nchi kikamilifu.

Kulitokea mtafaruku mkubwa sana ndani ya CCM. Wengi walifikia hatua ya kudai "kofia" ya uRais wa JMT itenganishwe na ile ya Mwenyekiti wa CCM kwa vile waliona Kikwete kalegea sana na kupwaya kiasi cha kuweza kupelekea chama kumfia mikononi mwake. Hawakuwa tayari kabisa kuona dola ikitenganishwa na CCM wala madaraka ya Rais na Mwenyekiti wa CCM yakirekebishwa. Aidha, hawakutaka kuona Muungano "ukilegezwa". Hao wana CCM huwezi kuwaita wote wanamtandao. JK ndiye anayetambulika kama "mwanamtandao". Lakini ndiye aliyekuwa akishambuliwa na wana CCM wengi kwa kule tu kujaribu kuruhusu mageuzi kuimarisha haki na usawa nchini.

Magufuli alipoingia madarakani 2015, masuala ya katiba na tume huru ya uchaguzi akayatupilia mbali na kutumia vyombo vya dola moja kwa moja kuiimarisha CCM na kudhoofisha upinzani. Wana CCM wakamshangilia sana kama "mkombozi" wao aliyewanusuru na fedheha za siku kwa siku na kuwawezesha kuvaa kijani zao hadharani bila hofu ya kuzomewa. Ulinzi wa polisi ulikuwa ukiwahakikishia kutozomewa na magwanda yao 24hrs! Magufuli hakuwa mwanamtandao. Lakini alikamata dola na nyenzo zake kisawa sawa na akazitumia kama alivyotaka. Iwe kudhibiti bureau de change au kusomba korosho au kujenga majengo ya serikali, au ...

Sasa kama kweli unaamini nje ya "wanamtandao", CCM wanaweza kukubaliana na NRNE ya CHADEMA, kila la heri.
We NTU kuna kitu unajua, hyaani mulemule....
Deep state capture, tunatokaje sasa ktk kundi hilo...!!? Maana sasa mnaojua kinachoendelea na nyie ni kama mmeshajiunga nao, hapo ndo pagumu..., lkn sikio la kufa Polepole alisha tutahadharisha mapema na kundi hili...
 
Back
Top Bottom