Ulaji kwa watoto chini ya miaka mitano ni changamoto ila kuna mambo mengi inapasa kuchunguza ili ku kufahamu sababu na kukabiliana nazo kama mtoto anapata joto,rash,anatapika,anakohoa,anakataa chakula muda wote au kuna nyakati tu.Sababu zinaweza kuwa Meno,Minyoo,Kupewa maji mengi au juice au maziwa natumbo lake ni dogo,Kuwa na afya dhaifu,Mafua,Kifua,Joto kali,Kutokwa jasho kwa wingi,Kumuanzisha vyakula vigumu ambavyo kwake ni vigeni anahitaji kupewa kidogo kidogo hadi azoee,Kuchoka,Vidonda kooni vinamfanya ashindwe kumeza,Chanjo mbalimbali nyingine husababisha homa,mumps,Rash,Kuharisha na kama haya yataendelea kwa siku mbili mpaka tatu ni vema kumuona daktari ili apatiwe tiba kwa tatizo la upungufu wa damu ambalo pia huleta shida kubwa ya ulaji na kuwa pale,mikono na miguu kuwa baridi ukimlinganisha na watoto wengine apewe vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi,mama ahakikishe anazuia yeye anakua na damu ya kutosha akiwa mjamzito ili asimpe udhaifu mtoto atakaezaliwa,mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama angalau mwaka mmoja wa kwanza na ikiwa haiwezekani apewe fomula zenye madini ya chuma kwa wingi na anayekula apewe maharage makavu yapikwe,Soya ,Samaki,Kuku,Bata mzinga,,siagi ya karanga,Spinach,mboga za majani kwa wingi Tujizuie sana kuwapa maziwa ya ng'ombe watoto chini ya mwaka mmoja,tujitahidi sana kuwapa vyakula vyenye vyanzo vya vitamin C kwa wingi machungwa,mananasi nkTusicheze na afya za watoto tunapoona dalili tofauti yoyote twende hospitali na TUSIACHE KUWAPELEKA WATOTO KLINIK KUPIMA UZITO KILA MWEZI HADI AFIKE MIAKA MITANO MAMBO MENGI YANAFUNDISHWA MIMI NASHAURI HIZI ZA SERIKALI MAANA CHANJO NYINGI HUTOKEA NA NIMEJIFUNZA HUWA ZIPO SERIKALINI UNAKUTA MTOTO ANAEENDA PRIVATE ANAKOSA NI HATARI NA HATA TAARIFA HAKUNA.