Wazazi wengi siku hizi hatuna muda na watoto wetu... Watoto wamekuwa ni wa wadada wa kazi na walimu, makuzi ya mtoto kiakili na kimaadili yanahitaji uwepo na ukaribu wa mtoto kuliko mtu mwingine yeyote yule.
Pamoja na harakati za kimaisha lakini ni vema ni muhimu na kuna wakati kutenga muda wa kukaa na familia yako ili kile ukitafutacho kiwe na manufaa na baraka mbeleni.
Dada wa kazi ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4
Mwalimu ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4 pia
Mzazi ana majukumu yake ambayo ni 1/2
Kwahiyo kama mzazi usibweteke nusu nzima ya malezi ya mtoto inakuhusu wewe.
Balaa linaanzia kuanza kushika ujauzito bila kupanga nini kitakwenda vipi huko mbeleni.
Kunakitu kinaitwa uzazi wa mpango sijui kwann vijana na mabinti wanahisi hili jambo haliwahusu. Sababu ukitazama kwa kina uzazi wa mpango unazo program na maelekezo ya namna life ya uzazi inatakiwa kupangwa from the beginning kabla hata mwanamke hajabeba ujauzito.
Mipango ya mtaishi wapi, nani atakaa na mtoto na mama wa mtoto wakati wa uzazi yaani ile miaka 2 ya kwanza sababu hiki ni kipindi ambacho mwanamke anatakiwa kutoa 100% ya attention yake kwa mtoto muda wote ili akue vizuri na kiwa imara.
BAJETI YA MALEZI YA MAMA NA MTOTO WAKE.
Miezi 6 ya kwanza mtoto hali kitu chochote nje ya maziwa ya mama, so mama anatakiwa kula vizuri ili aweze kuproduce maziwa mazuri kwaajiri ya mtoto. Anatakiwa kupumzika kwa maana kutokuwa na shughuli nje ya mtoto kama kwenda kazini na kadhalika.
Maziwa au lishe ya mtoto atakapo anza kula vyakula nje ya mama yake. Kuna yale maziwa ya kopo kama haujajipanga utaona kama mtoto na mama yake wamekula njama kukufilisi maana mfano mtoto wa kiume anakata kopo moja ndani ya wiki tu maana hawa wanakunywa sana maziwa kuliko wa kike.
Je, kama kama bibie atashika ujauzito na wewe bado upo na mishe mishe atakaa wapi, utapanga nyumba au ataenda kukaa kwa mama mkwe au mama yako? Na je utakuwa unawawezesha kwa namna gani kwa maana ya kuwapelekea mahitaji sio tu mkeo na mtoto ila hata familia husika ambapo mkeo yupo ili ulezi wa mkeo na mtoto uwe na manufaa kwa wote.
Kama itawezekana baada ya mwaka anaweza kufanyiwa mpango wa kwenda gym ili kurejesha uimara wa mwili sababu ya kukaa muda mwingi ndani ili kurudisha mwili na mvuto wake.
Haya yanawezekana kama mtakaa na kupanga mapema. Hivi niwaulize unapokaa na girlfriend wako, mchumba wako au mume wako huwa mnajadili nini nje ya haya maana haya ndio maisha yenu so kama hamjadili nje ya haya it means huwa hamna la maana mnapanga juu ya umoja wenu na kuishi pamoja.