Miongoni mwa reform zilizofanywa na Serikali ya awamu ya tatu, ilikuwa ubinafishaji wa mashirika ya Umma na uanzishwaji wa wakala za Serikali.
Mashirika ya Umma yaliuzwa kwa bei ndogo kwa wazawa na foreigners.
-Mashirika ya Umma na viwanda vingi vilivyo uzwa havikufanya kazi na majengo yao kugeuzwa magodown ya kuhifanyia mazao.
-Mashirika ya Umma ambayo yalikuwa yanaleta faida ndiyo yaliuzwa Kama benki ya NBC nk.
-Shirika la ATC,TRC,Tanesco yaliuzwa/kukodishwa/kuingia ubia na wawekezaji kutoka Afrika Kusini na India ambao walikuja kuchota fedha na kuacha mashirika dhoofu hali.
-Idara za Serikali ambazo hazikuwa na Majukumu mama ya Serikali ziligeuzwa kuwa wakala wa Serikali.
-Wakala za Serikali,zilipewa Uhuru wa kujiendesha kibiashara,kwa kuruhusiwa kutumia maduhuli yao au sehemu ya maduhuli yao kuesha wakala hizo.
-Kimsingi Majukumu ya Serikali ni ulinzi wa nchi,usalama wa wananchi na mali zao,utoaji wa huduma za kijamii kama vile elimu,maji, Afya kwa wananchi wake.
- Serikali haipaswi kufanya biashara, Serikali unatakiwa kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na kutoza kodi.
-Wakala za Kwanza kuanzishwa zilikuwa Mamlaka ya usafiri wa Tanzania na Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania.
-Mamlaka hizi zinajiendesha zenyewe,isipokuwa unapohitajika uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu kama ujenzi viwanja na ununuzi wa mitambo nk.
Maoni
1).Ni kweli Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, mipango yake haina uendelevu,inabadilika badilika kutegemea nani yupo madarakani.
2). Uamuzi wa Serikali ya awamu ya sita ni mwendelezo wa mipango na mikakati ya Serikali ya awamu ya tatu na tano.Kwa mfano huo uamuzi wa TTCL ni sera za awamu ya tatu na uamuzi wa kuendelea kununua ndege 5 za abiria na mizigo ni sera za awamu ya tano.
Ushauri
1). Serikali iachane na masuala ya kufanya biashara au kuwekeza kwenye biashara,haitakuja kupata faida/gawio
2). Serikali ijikite kuweka mazingira mazuri ya kuwekeza na kufanya biashara sekta binafsi.
3). Fedha zinazowekezwa kwenye biashara,zitumike kuwekeza kwenye vyuo vya ufundi, Afya, maji safi, miundombinu,nk.
-Kwa kufanya hivi vijana wetu watapata ujuzi, watakuwa na Afya bora,maji safi yatapunguza magonjwa na kuwezesha kilimo cha umwagiliaji, miundombinu itasaidia mawasiliano na uchukuzi, umeme kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo na viwanda vikubwa nk.
4) Serikali iwe inatoa dhamana(Government guarantee) kwa Mashirika ya Umma yenye maslahi mapana kwa taifa, kukopa kwa ajili ya uwekezaji na watendaji wakuu wapewe Majukumu ya kurejesha mikopo hiyo.
5). Serikali inaweza kusaidia mashirika ya Umma kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha za kimataifa yenye riba ndogo, kwa ajili ya miradi ya maendeleo