Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Kwaheri TTCL, kila lenye mwanzo halikosi mwisho

Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa na kueleza madudu ya TTCL, Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu, lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
Babu mmoja aliwahi kunisimulia adithi ya ngedere kuchekelea wakati pori linaungua mchana.bila kukumbuka ni makazi yake ya kujilaza usiku.
Ni rahisi kukebei kufa kwa mashirika ya umma bila kujua kama watakaokosa ajira kama sio ndugu basi ni wajukuu zako wajao.
Mimi naamini wenye kampuni zao ambao mpaka kesho tunawalalamikia kwa kupandisha bando,wameishafanya yao. Ni kama ATCL na TRC zilivyokufa vifo vya kimkakati kupisha biashara za watu.
Ngoja tuendelee kunawa mikono na maji tiririka tukidhani tunamkomesha magu,
kumbe kiuhalisia marehemu hakomolewi bali wewe unayepumua unajipa presha bure kufukuzana na upepo.
 
Tatizo ni mifumo.

Tanzania hakuna mifumo imara, wako tu wahuni wanajiamulia wanavyotaka kwa maslahi yao siyo kwa ajili ya taifa.

Kutengeneza mifumo iwe inadhibiti na kuwaadhibu hao hata kama ni mafia wa namna gani waadhibiwe vikali kama kule China, Cuba walifanya mageuzi na walifanikiwa, hata Tanzania inawezekana.

Kama hatutaweka mifumo imara nchi itaendelea kuwa Banana republic siku zote kwa miaka na mikaka.
Mfumo unatoa dira ya taifa, Tanzania hivi ina dira ya taifa? Au aliepita alifufua ttcl leo huyu anasema hiyo hiyo ttcl ambaye yeye alikuwa msaidizi wa aliyetoa maauzi kuifufua ttcl leo anatoa maamuzi ya kuiua.
Anakuambia anaongeza ndege nyingine,wakati huohuo anakuambia maneno hayo. Hapo sijui tuelewe vipi
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa na kueleza madudu ya TTCL, Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu, lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
Na watumishi mliambiwa sharti muwe na line za shirika hilo la Serikali lilitoa gawio kubwa zaidi kwa Serikali mwaka juzi!
 
Kwa hali ilivyo sasa ttcl ili ifufuke kwanza wahakikishe wanapatikan kila sehemu ya nchi hii yaani wanakuwa na coverage kubwa na speed ya kutosha kisha washushe mabando hasa internat, wapige promosheni ya kutosha maofisini na vyuoni ninahakika baada ya miezi michache wataona mabadiliko chanya. Ni aibu kwa shirika la serikali lenye ruzuku kushindwa na mashirika binafsi, mbona UDSM ni mali ya serikali na inakimbiza vyuo vyote binafsi nchini.
 
Miongoni mwa reform zilizofanywa na Serikali ya awamu ya tatu, ilikuwa ubinafishaji wa mashirika ya Umma na uanzishwaji wa wakala za Serikali.
Mashirika ya Umma yaliuzwa kwa bei ndogo kwa wazawa na foreigners.
-Mashirika ya Umma na viwanda vingi vilivyo uzwa havikufanya kazi na majengo yao kugeuzwa magodown ya kuhifanyia mazao.
-Mashirika ya Umma ambayo yalikuwa yanaleta faida ndiyo yaliuzwa Kama benki ya NBC nk.
-Shirika la ATC,TRC,Tanesco yaliuzwa/kukodishwa/kuingia ubia na wawekezaji kutoka Afrika Kusini na India ambao walikuja kuchota fedha na kuacha mashirika dhoofu hali.
-Idara za Serikali ambazo hazikuwa na Majukumu mama ya Serikali ziligeuzwa kuwa wakala wa Serikali.
-Wakala za Serikali,zilipewa Uhuru wa kujiendesha kibiashara,kwa kuruhusiwa kutumia maduhuli yao au sehemu ya maduhuli yao kuesha wakala hizo.
-Kimsingi Majukumu ya Serikali ni ulinzi wa nchi,usalama wa wananchi na mali zao,utoaji wa huduma za kijamii kama vile elimu,maji, Afya kwa wananchi wake.
- Serikali haipaswi kufanya biashara, Serikali unatakiwa kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na kutoza kodi.
-Wakala za Kwanza kuanzishwa zilikuwa Mamlaka ya usafiri wa Tanzania na Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania.
-Mamlaka hizi zinajiendesha zenyewe,isipokuwa unapohitajika uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu kama ujenzi viwanja na ununuzi wa mitambo nk.

Maoni
1).Ni kweli Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, mipango yake haina uendelevu,inabadilika badilika kutegemea nani yupo madarakani.
2). Uamuzi wa Serikali ya awamu ya sita ni mwendelezo wa mipango na mikakati ya Serikali ya awamu ya tatu na tano.Kwa mfano huo uamuzi wa TTCL ni sera za awamu ya tatu na uamuzi wa kuendelea kununua ndege 5 za abiria na mizigo ni sera za awamu ya tano.

Ushauri
1). Serikali iachane na masuala ya kufanya biashara au kuwekeza kwenye biashara,haitakuja kupata faida/gawio
2). Serikali ijikite kuweka mazingira mazuri ya kuwekeza na kufanya biashara sekta binafsi.
3). Fedha zinazowekezwa kwenye biashara,zitumike kuwekeza kwenye vyuo vya ufundi, Afya, maji safi, miundombinu,nk.
-Kwa kufanya hivi vijana wetu watapata ujuzi, watakuwa na Afya bora,maji safi yatapunguza magonjwa na kuwezesha kilimo cha umwagiliaji, miundombinu itasaidia mawasiliano na uchukuzi, umeme kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo na viwanda vikubwa nk.
4) Serikali iwe inatoa dhamana(Government guarantee) kwa Mashirika ya Umma yenye maslahi mapana kwa taifa, kukopa kwa ajili ya uwekezaji na watendaji wakuu wapewe Majukumu ya kurejesha mikopo hiyo.
5). Serikali inaweza kusaidia mashirika ya Umma kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha za kimataifa yenye riba ndogo, kwa ajili ya miradi ya maendeleo
 
JPM alimleta yule jamaa kutoka ughaibuni asimamie TTCL akawa apigana kwelikweli.

Baada ya JPM kufariki yule jamaa akaondolewa hapo na nadhani amepewa nafasi ya kisiasa ya ukatibu tarafa au kitu kingine.
Waziri Kindamba ni Mkuu wa Mkoa. Alianzia Songwe na mwezi jana kahamishiwa mkoani Tanga. Alijitahidi sana kuipigania TTCL lkn ndio hivyo kasogezwa mahali pengine
 
Pole mkuu, hiyo line fanya kuihifadhi tu na kuwa kumbu kumbu kuwa kuliwahi kuwa na line za TTCL
Weka kwenye makumbusho ya familia
Imeisha hiyo. Na siku wakiruhusu wawekezaji binafsi kuzalisha na kusambaza umeme. Tanesco watakufa kama ttcl
Wanatutesa sana Hawa tanesco
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa na kueleza madudu ya TTCL, Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu, lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
Usirudi nyumbani kumedoda
 
Cha kuongezea, nchi hii inakwamishwa kwa kila Rais kuja na maamuzi yanayokinzana na aliyepita kana kwamba wanatoka vyama tofauti.

Magufuli (R.I.P) alipigania kuifufua TTCL, huyu wa sasa anakuja na maoni tofauti, tuelewe nini!?

Kingine, vipi kuhusu ATCL? Imepiganiwa sana kiasi cha kuletewa ndege mpya, je, ina ufanisi wowote mpaka sasa!? Au imekuwa ni kaburi la pesa za mlipa kodi!?
Mbeba maono kafa na maono yake.
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa na kueleza madudu ya TTCL, Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu, lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
Ni njama tu za makampuni binafsi kuliua na hatimae kulibinafsisha shirika la ttcl ili wajipangie wao kwa uelewano bei waweze kuwanyonya wananchi. Hebu fikiri kabla nape kua waziri ttcl waliuza GB 1 kwa buku ila nape alizuru shirika la ttcl na kuwaonya hawatabebwa na wataangaliwa sawa na mashirika binafsi. Wakati wa magufuli alitilia mkazo kuinua ttcl kama shirika la umma linalotakiwa kuleta ushindani ili kutoa huduma yenye bei halisi kwa mwananchi. Badala yake sasa ttcl inakoromewa na watu kama nape isiwe shindani kwa kutoa bei nafuu ya huduma zake.
Pamoja na umuhimu wa sekta binafsi wanawrza kua wanyonyaji tu wa wananchi.
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa na kueleza madudu ya TTCL, Rais Samia Hassan amependekeza shirika hilo la umma libaki kusimamia mkongo wa Taifa tu, lachane na biashara ya mawasiliano ya simu.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi TTCL kwenye simu za viganjani.

Sasa sijui hizi line zetu itakuwaje yaani, tutafidiwa chochote au ndio vile tena?

Tunaitakia kila la heri.
Aisee..
Wameiba ngapi?!
 
Naamini Rais Dkt Samia atapata ushauri sahihi, TTCL haipaswi kuondoka kwenye simcard, usalama wetu kama taifa tunategemea kuwa na njia ya mawasiliano ambayo ni secure. Akumbuke kilichowatokea wachina, hawa voda/airtel/tigo/halotel etc wanaweza ondoka muda wowote yaani tena inaweza kuwa kauli ya rais kupinga ushoga au kuwaunga mkono Russia. TTCL wanipe mi niwe mkurugenzi nita hakikisha nina li turn around na kuwa profitable!
 
Kuna sekta makampuni au mashirika ya serikali ni vigumu sana kufanya biashara na kushindana na makampuni binafsi bila kubebwa.
TTCL wameajiri wazee wao wakagomea cdma wakati wenzao wanahamia Edge,3G
Wakashtuka na kwenda moja kwa moja hadi 4G minara hawana hivyo simu nyingine zikawa zinashindwa pata mawimbi.

TTCL wakatoa Bilioni zaidi ya 1 kuipa serikali gawio, afu ikaja iomba serikali iwape Tril 1 ijenge minara 1000 na kurekebisha miundombinu wezeshi
 
Back
Top Bottom