Hisia zangu zinasema kuwa atakatazwa. Kwa kinachoendlea sasa hivi sidhani kama watakubali atoe ujumbe wowote. Labda atumie njia za panya kama anaweza. Nilimsikia Heche akisema viongozi wa CHADEMA wanapotaka kumtembelea wanakatazwa kumwona. Pia nahisi hakuna atakayeruhusiwa kumwona mpaka ''upotoro'' wa Chande usomwe, na siku hiyo yule mama atajifanya kutoa hotuba ya ''the way foward'' na atarudia-rudia kusema kuwa Lissu ameomba atolewe ili wafanye maridhiano na yeye ''ameamua kumsamehe''.
Jambo hili halihitaji rocket science au hesabu za calculus kufahamu kuwa kinachoendelea ni muendelezo wa sarakasi na mazingaombwe unaofanywa na serikali haramu na batili iliyojiweka madarakani kwa njia isiyo halali.