Kwako Nape, umeona hela ya mkopo aliyokula Hayati Dkt. Magufuli?

Kwa hiyo hata kukomesha wezi na kufukuza vyeti feki nako tulitumia mkopo ?
 
Yaani watu wanasahau haraka sana,but muda ni mwalimu mzuri.
 
Hizo alama unazosema wanaziona wajinga tu,
Wenye uelewa wanajua alikua mpigaji mtukufu akishirikiana na SUKUMA GANGS.
Sasa mtashaaaaa
 
Sio lawama lazima tuhoji kwasababu ni pesa zetu, Wewe endelea kushukuru tu kwasababu unajua pesa ni za serikali
Miradi hujaiona?tena ya pesa nyingi.
Acheni kumchafua hayati pasipo sababu.
 
Kuongezea;
•upanuzi wa bandari ya tanga, mtwara na dar.
• ujenzi wa meli na vivuko ziwa tanganyika, nyasa na victoria pamoja na ujenzi wa kivuko cha nyamisati mafia.
• ujenzi wa njia za umeme vijijini kupitia REA.
• miradi mikubwa ya maji ukiwemo ule wa arusha, ule wa ruvu kupitia kisarawe hadi dsm, ule wa ziwa victoria mpaka mikoa ya tabora.
• ukarabati na ujenzi wa maabara, vyuo vya maendeleo, vyuo vya ualimu na shule za msingi na sekondari katika muonekano wa kisasa kabisa.
• ujenzi wa masoko ya kisasa na stendi za mabasi za kisasa ikiwemo dom, korogwe, iringa, dsm na maeneo mengine.
• kuongeza mikopo kwa wanachuo.
• kuhamishia makao makuu ya nchi dodoma zigo lililomshinda nyerere,mwinyi, mkapa na kikwete.
• ujenzi wa vituo vya afya, zahanati na hospital za rufaa mtwara, mbeya, dodoma pamoja na umaliziaji wa hospital ya rufaa mara iliyosimama toka enzi za nyerere.
• ujenzi wa maeneo ya kupumzika katika miji.
 
Wacha kutisha watu nyinyi wapigaji wakubwa na sasa tunaanza kuyaona kupitia kwa makada wenzenu wa ccm.
Unafiki mbaya jamani
Sasa asiekujua humu wewe ni upinzani kindaki ndaki nani!
Wewe ndio Wale mnaofurahia kwa wenzenu kuungue ili mpate mtakacho.
Hujawahi kuipenda ccm.
 
Kwa hela hii ya mkopo aliyokula Magufuli nipo tayari kukatwa kwenye mshahara wangu ili kuirudisha. Nipewe tu utaratibu wa kufuata.
 
Magufuli kama alikopa ni miradi alifanya tena ya maana,watz tunataka viongozi Wapiga deal ati ndio ujanja.
Now wanajidai wasafi huku hakuna kitu.
Wakiendelea na kumtusi Magu wajue wanaandaa mazingira ya kuwapa upinzani ushindi.
Binafsi nasikia ukakasi .kama hao wezi wanadhani JPM ni rank Yao watumie huo utoporo kwenye campaign ndo wayanua mbivu na mbich dadeki
 
Hahahaaa dah!
Anyway it is what it is.
 
Unafiki mbaya jamani
Sasa asiekujua humu wewe ni upinzani kindaki ndaki nani!
Wewe ndio Wale mnaofurahia kwa wenzenu kuungue ili mpate mtakacho.
Hujawahi kuipenda ccm.
Na sitokaa niipende kamwe ccm.

Imetutia umasikini sana kwa miaka zaidi ya 60.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…