Kwako Nape, umeona hela ya mkopo aliyokula Hayati Dkt. Magufuli?

Kwako Nape, umeona hela ya mkopo aliyokula Hayati Dkt. Magufuli?

Ukarabati na ujenzi meli mpya katika Ziwa Victoria
No

Naongezea ukarabati wa mashule na sekondary ukarabati wa reli ya zamani Dar-Isaka, ukarabati wa reli Dar Arusha mahospitali ya mikoa na rufaa, mahakama za rufaa kiala mkoa vitendea kazi kuanzia police mapaka halmashauri vya kukusanyia ushuru na migumo mingi ya tehama na mabadiliko yake
 
HELA YA MKOPO ALIYOKULA JPM HII HAPA.

Tuliona utendaji wa kuacha alama katika awamu ya tano, tuliona uwajibikaji uliotukuka na kwa hakika Mabadiliko ya kimaendeleo yaligusa kila mmoja wetu, kama uoni basi utashika utagundua Kweli kuna mabadiliko, kama hushiki basi utakanyaga na utagundua mabadiliko makubwa ya kimaendeleo, ukitoka Kibaha kuja Mbezi hadi Kimara utaona kazi kubwa iliyofanyika ya ujenzi wa Barabara ya Morogoro, utajua kweli Serikali ya Rais Magufuli ilifanya kazi, kwako Nape pokea salaaam.

Awamu ya tano ilivyoingia Madarakani tuliona utendaji huu,

-Ujenzi wa Hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (udsm).

-Ujenzi wa Hostel za Askari Magereza.

-Ununuzi wa Ndege 11 (Nyingine 5 ziko mbioni kuja).

-Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo,

-Upanuzi wa Airport Mwanza,Bukoba,Mbeya,Songea,Dodoma na Musoma.

-Upanuzi barabara ya Moroco DSM, Mwanza na Arusha.

-Upanuzi wa Kisasa Airport Dar ,terminal 3.

-Kusimamia misingi ya kimaadili ya Utumishi wa Umma, Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.

-Ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme (Standard Gauge)

-Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba.

-Ujenzi wa kota za Magomeni.

-Ununuzi na Ujenzi wa Rada Mpya 5 tano za kuongozea ndege katika anga lote la Tanzania.

-Elimu bure na Mafunzo ya kujitegemea katika Veta na Jkt kwa wahitimu wa Elimu ya Sekondari.

-Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

-Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

-Miradi Mikubwa ya Maji,Ujenzi wa Matenki makubwa Dar es Salaam na mradi mkubwa wa Maji toka Ziwa Victoria kuja Tabora hadi Dodoma.

-Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Jijini Tanga,Tanzania.

-Usimamizi wa Mazao Mfano Korosho,Pamba,Katani,Alizeti,kahawa,Chai,Maharage,Kilimo cha Mpunga na kutafuta masoko nje ya Nchi kwa ajili ya kupata fedha za kigeni kuinua uchumi wetu.

-Kuboresha Sekta ya Utalii kwa kununua ndege kurahisisha usafiri wa Watalii toka Mabara yote kuja Tanzania.

-Usimamizi wa Mapato ya Mali asili zetu,mfano Madini ya Dhahabu, Tanzanite na Almasi.

-Ukusanyaji Mapato baada ya kuziba nianya ya ufisadi na wizi wa mapato na mali ya Umma.

-Kujenga Utaifa na Uzalendo.

-Ujenzi wa Bwawa la Umeme katika Mto Rufiji "Stigglers Gorge".

Kwa hakika katika awamu ya 5,Serikali ya CCM iliyoongozwa na Rais Magufuli imeifanya CCM kuwa Mpya katika utendaji wa kasi na wa uhakika pasipo porojo wala propaganda, Mwenye macho anaona utendaji katika sekta mbali mbali kuijenga Tanzania Mpya ambayo itakwenda kuwa Baba la Uchumi barani Africa.

@KWAKO NAPE UMEONA MKOPO ALIOKULA JPM!?#😀
Alafu mkaishia kuwahadaa watanzania mabeberu sio watu wazuri, baadaye mnakaa nao mezani tunaonba mtukopeshe. Hv mlituonaje ?
 
Mm kinachonoshangaza wakati hizo pesa anazodai zlikopwa na matumizi yake hayafahamiki wao kama wawakilisho wa wananchi walikuwa wanafanyaje au zilitumika hovyo wakiwa wap hawa huwa hawatabiliki kabisa
Hawa ni wachumia tumbo tu; bajeti zote za serikali zipo na zilikuwa zinaonyesha wazi ni pesa kiasi gani kitakopwa na ni kiasi gani zitatokana na kodi, na miradi ya maendeleo itakayotekelezwa ni ipi na gharama zake ni zipi. Kuna miradi mingine ya maendeleo haikuwa ya lazima kama vile ujezi wa uwanja wa Chato, lakini hawa jamaa walipitisha bajeti ya wizara ya mawasiliano na uchukuzi kikiwemo kifungu cha ujenzi wa uwanja wa Chato bila kuhoji, halafu baadaye leo ndiyo eti wanalalamika. Tena bajeti ya uwanja wa Chato ilikuwa imeletwa bila kuwa na specifics za kutosha ila wao wakapiga makofi tu na kuipitisha bila kuhoji chochote.

Lakini leo hii ndipo wanajifanya wanajua kufuatilia hela za serikali kama siyo kutafuta sifa za kipuuzi tu
 
Magufuli kama alikopa ni miradi alifanya tena ya maana,watz tunataka viongozi Wapiga deal ati ndio ujanja.
Now wanajidai wasafi huku hakuna kitu.
Wakiendelea na kumtusi Magu wajue wanaandaa mazingira ya kuwapa upinzani ushindi.
Nimeshaaona kitu hata nape anjiona mjanja kwa sasa lakini kama sio nguvu ya magufuli kuna wabunge nakuhakikshia wansingefika hapo waliopo .leo ndo wako mstari wa mbele kumdhalilisha hayati magufuli .tuone kama 2025 watapanua tena mdomo
 
Back
Top Bottom