Mkuu umeshindwa kujikita kwenye mada. Pitia mabandiko yako yote kwenye uzi huu ni wazi kuwa umejitahidi sana kulazimisha kuwa hapakuwa na uzembe ugonjwa huu kuingia nchini. Hii ikiwa pamoja na kuwa kwa hakika huna vigezo wala sababu yoyote yenye mashiko yenye kuonyesha kuwa uzembe haukuwapo.
Mkuu hatudanganyiki. Enough is enough. Aliyetufikisha hapa tunamjua na anayetuchulia kutaka kututanguliza akhera pia tunamjua.
Nini chimbuko la uzi huu - ni kumtaka sasa hata kama yeye ni dereva wa lori, kwa vile amekubali kutubeba na kwa kuwa nasi tumekubali kubebwa naye (mutual agreement) asimame sasa tuongee kwanza. Kwa maana siyo siri tena haturidhishwi na wala hatufurahishwi na mwenenendo wake kwenye hili.
Tatizo liko wapi hapo kwako kama hauna maslahi binafsi? Wapi umeona siasa katika bandiko langu kwenye uzi huu? Kwa nini umeshupaa hivyo kuwa hakuna uzembe bila kutoa ushahidi wowote kwenye hilo? Mkuu tushawishi kwa hoja basi kuwa uzembe haukuwapo. Ila usitulazimushe.
Eti nikipewa uongozi sitaacha kutanguliza siasa. Utakuwa ulikuwa unaota wewe si bure ikizingatiwa kuwa bandiko lako hili umeliandika usiku wa manane haswa. Aliyekwambia kuwa hata ninahitaji huo uongozi ni nani?
Ati kuwa jambo la wataalamu wameingia wanasiasa na kuwa kila jambo lina wataalamu:
".... misukumo ya kisiasa, huu upuuzi wenu wa siasa mnauwezaga wenyewe maana kila jambo lina wataalamu wake na ndiyo maana tuna viongozi wenye kuleta siasa hadi penye kuhitajika utaalamu."
Haieleweki kama unajitambua. Hawa tunaowalalamikia wanalipeleka jambo hili kitaalamu? Haya maombezi ndiyo utaalamu wenyewe? Hii mikusanyiko bungeni, kwenye ibada, masokoni, kwenye safari za umma ndiyo utaalamu wenyewe?
Mkuu alisema mwenyewe, "mtanzania wa leo siyo wa jana". Mwisho wa kumnukuu.
Kwa mabandiko yako ni wazi kuwa uzembe uliotuletea ugonjwa huu hapa nchini unakuhusu. Haiyumkiniki itakuwa ndiyo sababu ya kushupaa kwako huku. Vipi mkuu dhamira inakusuta?
View attachment 1424246