Warussia Wana kamsemo....."PALE UWEZO WA MTU UNAPOFIKIA MWISHO KUFIKIRISHA BASI LAZIMA AMWINGIZE MUNGU"
Rais Magufuli amefikia ukomo wa akili yake kufikiri namna ya kudhibiti ugonjwa wa Civid-19!!!Ndiyo maana amekimbilia Kanisani na Msikitini...!!!
Kinachonisuangaza kuhusu Rais wetu anashindwa kuelewa kuwa MUNGU ANA PRINCIPLES (Kanuni)zake ili asikie na kujibu maombi ya mwanadamu yoyote. Principle Moja muhimu ni TOBA. Taifa lazima litubu au liombe msamaha kwa dhambi au makosa ambalo limekosa mbele za Mungu lakini pia Rais mwenyewe na watu wake waombe radhi kwa MAOVU,MAKOSA DHAMBI walizowatendea Watz/Raia kwa maksudi au bahati mbaya!
Mifano ya DHAMBI/makosa hayo ni pamoja na UONEVU WA SERIKALI KWA RAIA kwa kutumia vyombo vyake vya ULINZI&USALAMA(Polisi,TISS,Mahakama, Magereza n.k.)
Mifano halisi ni SHAMBULIO LA TUNDU LISSU, KUPOTEA KWA BEN SAANANE,KUPOTEA KWA AZORY GWANDA,KUBAMBIKIA KESI WANASIASA WA CHADEMA NA KUWAFUNGA NA VIPIGO visivo na sababu zaidi ya UONEVU!
Bila ya Rais Magufuli na Serikali yake kuomba msamaha na kuchukua hatua madhubuti kuzuia maambukizi ya Covid-19.
Hatua za kuchukua kwa Sasa nu pamoja na:
- DAR na ZANZIBAR ziwe under quarantine na Partial Lockdown kwa siku 30. HAKUNA kutoka wala kuingia Dar au Zanzibar na wakazi wake HAKUNA kutoka na kuingia majumbani mwao.
- Serikali igawe mahitaji muhimu kwa wakazi wa miji hii kwa kutumia Fedha ya Maafa, Fedha ya michango toka Raia wema(6B+) na Fedha za Mwenge na Muungano.
- Kwa wale Raia wakorofi watakaotoroka kutoka miji hii 2 kwenda mikoani au Bara Basi mikoa husika iwabaini na wawekwe Quarantine ya 14 days kwa gharama zao wenyewe.
Kama hatua hizi 3 zikitekelezwa kwa umakini mkubwa Tanzania bado inaweza kudhibiti maambukizi yasienee nchi nzima. Kwa Sasa Dar na Unguja ni Kama WUHAN ya China ambako mlipuko wa Covid-19 ulianzia!
Mjumbe hauwawi, mie nimeshafikisha ushauri/ujumbe kwa wahusika.
Wasalaam.