Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

Mkuu unaowatetea hawatakubaliana nawe kwani wanajua wangesikiliza ugonjwa usingeingia. Hata sasa hivi wakisikiliza maambukizi yatapungua hadi kutoweka kabisa.

Mkuu unadhani kama wange:

1. Funga mipaka.
2. Zuia ndege na wasafiri toka nchi zilizo athirika.
3. Weka quarantine wageni wote wanaotaka kuingia nchini toka nje kwa siku 14.

Ugonjwa huu ungeingia nchini?

Kumbuka ugonjwa ulifika ulaya na marekani mapema mno kabla yetu. Ulaya na marekani waliizembea pia kwa kudhani ugonjwa ulikuwa wachina tu. Kama walivyozembea kwetu wakidhani huu ugonjwa si wa mtu mweusi.

Ushahidi wa nini na wapi walizembea upo. Huo ni wa baadaye.

Kwa sasa tafadhali mkuu tujikite kuzuia maambukizi zaidi. Nini cha kufanya kuifanikisha hilo tunakijua tungependa hatua zinazojikita huko maisha zaidi ya watu wasiokuwa na hatia yasipotee kizembe.
Duh! Kumbe naonekana kuna watu nawatetea?

Basi sawa mkuu hakuna nchi yenye corona ambayo haijafanya uzembe zote zimefanya uzembe kwa kutofanya kama ulivyoshauri na ndiyo maana corona imeingia nchi hizo.
 
Ulaya na China walikuwa hawana hivi vitu tena vyenye quality ya juu?

Sent using Jamii Forums mobile app


Shida ya sisi watanzania ni ujinga kupita kiasi. Makonda na mpuuzi kabisa na ameshindwa kuficha huo upuuzi wake tena bora kwa hili angekaa kimya kama huyo baba yake aliyekimbia kwa sentensi raisi tuu sasa hivi huyu raisi yuko mafichoni
 
Duh! Kumbe naonekana kuna watu nawatetea?

Basi sawa mkuu hakuna nchi yenye corona ambayo haijafanya uzembe zote zimefanya uzembe kwa kutofanya kama ulivyoshauri na ndiyo maana corona imeingia nchi hizo.

Vipi mkuu ulikuwa mmoja wa mliopewa majukumu kuuzuia ugonjwa huu kuingia nchini?

Unadhani hamkuzembea mahali mkuu?

Au mkuu unadhani kipengele hiki kinaweza kusababisha unga wako kumwagika?

Si lengo la uzi huu kutia kitumbua chake mchanga. Ndiyo maana muda wote nimekusihi sana, kuganga yajayo.
 
MODs tafadhalini msiufute huu uzi kama mlivyofuta ule wa siku tatu za sala ambao pia ulikuwa wa nia njema mno. Ni wazi kuwa wenye ujasiri wa kuandika nyuzi kama hizi kwa maslahi ya taifa ndani ya vitisho vilivyopo si wengi, hivyo tafadhalini msiwe sehemu ya kuwanyamazisha.

Wanasema nani mwenye kumfunga paka kengele? Ni muhimu sasa bila ya kupoteza muda zaidi wala kumung'unya maneno, tumfunge paka huyu kengele vinginevyo twafa tukijiona.

Wenye ujasiri wamejitahidi kuweka jitihada binafsi kuwahami wananchi.

Heko baba askofu Niwemugizi. Pongezi anazoendelea kuzipata baba askofu huyu ni wazi kuwa hatua za namna hii ndizo zilizokuwa zikihitajika kwa muda sasa.

Mh. Rais tafadhali tuachane na mambo ya uchumi na siasa. Ugonjwa huu utamaliza watu kwa uzembe wenu.

Gharama za kuwaweka watu manyumbani salama wasife kwa njaa (peke yake) tu ni ndogo mno na zitazidi kupanda kadri siku zinavyopita.

Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukishughulikia suala hili tangia mwanzoni wewe kama mtendaji mkuu imetugharimu kweli kweli. Hatukuweza kuuzuia ugonjwa
huu kuingia nchini, na wala hatukumwona hata mmoja katika safu zako aliyewajibishwa au kuwajibika.

Umekuwa ukilishughulikia suala hili kuuzuia ugonjwa huu kusambaa na bado ugonjwa unasambaa. Hatujamwona hata mmoja katika safu yenu aliyewajibishwa au hata kuwajibika.

Kwa mwendelezo huu ni wazi kuwa hatunayo nia ya dhati (seriousness) wala hatuchukulii umuhimu wowote mafanikio
au kushindwa katika vita hivi nyeti ambavyo hakuna taifa hata moja duniani lenye watu makini waliojaribu kuidunisha.

Kwa sababu ugonjwa huu unaenda kutuathiri kimaisha moja kwa moja (sisi na wapendwa wetu), kwa vile wawakilishi wetu labda hawakufikishii maoni yetu vilivyo, na kwamba eti wewe huyaoni haya, tunaomba kutumia maneno yako wewe mwenyewe:

"Kwa jinsi ambavyo umekuwa ukiendesha vita vya ugonjwa huu, tafadhali sasa NO!

Tunakupenda sana mheshimiwa. Lakini mheshimiwa kwenye hili la Corona, big No!

Kwa nini angalau Dar na Zanzibar haziko locked down? Mh. rais, Big No! Tumevumilia kweli kweli hadi tumelazimika kukupa ukweli huu. Mkuu big No!"

Cha kufanya kinafahamika. Kenya Rwanda na Uganda walio kama sisi wamefanya nini na sasa wanaudhibiti juu ya ugonjwa huu na karibu wanaanza kurejea kwenye shughuli zao za kawaida?

Please, Big NO!
Wenzetu wanamaliza, sisi tunaanza!
 
naiona lockdown inakuja muda siyo mrefu kulingana na idadi ya corona kati ya leo au kesho, maana kwa zanzibar ni 23 maambukizi mapya sijui kwa bara itakuwaje?
au ndo tuseme corona imeisha
😂😂😂...!
 
Nchi yetu ina akiba
Kwa nn isitumike
IMG_20200419_152843.jpg


Sent using Acity App
 
Vipi mkuu ulikuwa mmoja wa mliopewa majukumu kuuzuia ugonjwa huu kuingia nchini?

Unadhani hamkuzembea mahali mkuu?

Au mkuu unadhani kipengele hiki kinaweza kusababisha unga wako kumwagika?

Si lengo la uzi huu kutia kitumbua chake mchango. Ndiyo maana muda wote nimekusihi sana, kuganga yajayo.
Tatizo wabongo siasa imewaathiri sana na ndiyo maana hata suala hili mnalijadili kwa misukumo ya kisiasa, huu upuuzi wenu wa siasa mnauwezaga wenyewe maana kila jambo lina wataalamu wake na ndiyo maana tuna viongozi wenye kuleta siasa hadi penye kuhitajika utaalamu. Unafikiri mtu kama wewe ukipewa uongozi unaachaje kutanguliza siasa kwenye kuhitajika utaalamu.
 
Mkuu bandiko lako ka kiugoro ugoro halina mbele wala nyuma. Tafsiri za kuwa lockdown ni lockup unazipata tokea dictionary gani?

Kama haitoshi baada ya kujichanganya huko unapendekeza tena kuepuka maambukizi kwa kujiweka lockdown ukiwa tayari umesahau kuwa hiyo ni lockup kwa tafsiri yako.

Mengine uliyoandika ni kama unatokea sayari nyingine. Huna habari yoyote kuhusiana na muda mgonjwa anaweza kuwa hai na Corona. Huna taarifa zozote hata ni siku ngapi zinatosha kutambua mtu kama ana Corona au la. Huna hata taarifa lockdown ni kwa ajili ya nini.

Kwa kukuhurumia angalau kukupunguzia u mburula, uliwahi kuona haya humu jamvini?

View attachment 1424095
Kweli wewe zwazwa. Hivi unajua kwa mujibu wa WHO kuwa binadamu zaidi ya 150,000 hufa Kila siku kwasababu mbalimbali?
Na hiyo corona duniani imeambukiza watu wangapi na wamefariki wangapi? Tangu corona ianze haijafikisha kuua hata watu 180,000 kati ya zaidi ya watu 2,400,000 walioambukizwa. Na ni zaidi ya miezi sita.
Huo uhatari wake upo wp? Na waliopona wameponaje km ugonjwa hauna dawa? Tatizo mmepandikizwa hofu!
Madhara ya lockdown nimakubwa kuliko hata ugonjwa wenyewe. Watu watakufa njaa, wengine kwakukosa huduma muhimu na zaidi ongezeko la uharifu.
Sweden na nchi nyingi wamefanikiwa bila lockdown. Marekani tunashuhudia watu wanaandamana hawataki huo upumbavu wa lockdown. Tena ktk kipindi ambacho maambukizi kwao yapo juu. Wanamaabukizi zaidi ya watu 680,000.
Fuata maelekezo ya wataalam. Kama kufa utakufa tu so jiandae, km sio corona hata uzee utakuua!
 
Tukijikita kwenye matumizi ya barakoa, hata hizi za vitambaa tunaweza kukinga kuenea kwa korona kwa kiasi kikubwa, ni swala la enforcement tu kama alivyoanza kuagiza Makonda kwa wakazi wa Dar.
Naomba kuulizà swali hizi barakoa zinavaliwa kwa muda gani haraf unazifua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii issue kheri upambane wewe na familia yako tu. Kama una uwezo wa chakula na vitu vingine fanya hivyo, protect your family tu.
Wengine washaelimishwa na bado wanasubiri masia atakaeiponya nchi baada ya siku tatu za maombi, then waache waamini hivyo.

Mkuu hebu fikiria nyumba yako na familia yako ipo Manzese katikati na umeikinga kwa namna zote lakini ukaja moto ukashika nyumba zote zilizo jirani na wewe je mtapona? ni mfano ambao unaendana na Herd Immunity katika jamii
 
Back
Top Bottom