Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

Alishawaambia mtalimia meno leo huyohuyo unataka achukue hatua +ve kukuokoa kwa corona
 
Mkuu hebu fikiria nyumba yako na familia yako ipo Manzese katikati na umeikinga kwa namna zote lakini ukaja moto ukashika nyumba zote zilizo jirani na wewe je mtapona? ni mfano ambao unaendana na Herd Immunity katika jamii

Ajali haina kinga mkuu lakini kwa hili ..kila mtu ameshapewa hatua gani stahiki za kufanya na ndio maana nilisisitiza kwa wenye uwezo tu.

Pia Wakati wa dalili za kuzuka vita au machafuko, watu huwa hawakai majumbani wakisubiri serikali iwaambie tokeni nje ya mipaka. Huwa wanafanya hivyo ili kunusuru familia zao inapowezekana
 
Dah kazi kweli kweli. Aliimba bwana mmoja "tuko tofauti". Mwisho wa kumnukuu.

Ila ambaye:

1. Hakuzuia ndege tokea kulikokuwa na waathirika wa ugonjwa huu,
2. Hakuwaweka quarantine wageni wote wakiwamo wale wa kutokea China kwa angalau siku 14 kabla ya kuwaruhusu kuingia nchini,
3. Hakufunga mipaka
4. Nk nk,

Hakufanya hadi ugonjwa wa hatari kama huu ukaingia nchini.

Endeleeni kumfariji.

Ila waathirika sisi hatuna maneno mazuri kwake kwa balaa alilotuletea na analoendelea kulilea likiendelea kusambaa kizembe uzembe namna hii.
Mimi sina sababu ya kumfariji mtu wala kumshambulia bali naeleza uhalisi kwamba corona ni janga duniani ila kama wewe unaona hilo janga limesababishwa na uzembe basi ni sawa sina tatizo na wewe usione kwamba nataka kuitoa Tz kwenye lawama za uzembe,hapa siwezi kufanya hivyo maana kiujumla kila nchi ilifanya uzembe na Tanzania ni moja wapo hivyo haiwezi kuepuka lawama za uzembe.
 
Aunt punguza hasira,endelea kumuunga mkono mwana Ufipa mwenzio Askofu Niwemugizi maana alichokiamua Jimboni Lulenge ilikuwa ni katika kupingana na Rais Magufuli ktk kuliombea Taifa, ni hivyo tu.

Mkuu katika Mithali 26:4 kumeandikwa:

"Don't answer the foolish arguments of fools, or you will become as foolish as they are."

Mkuu uko vizuri kuliko hata baba askofu Niwemugizi.

Jimwage mkuu uko vizuri.

Baba askofu hajasaidia wowote kuepukana na maambukizi ya Corona kwenye uamuzi wake ila wewe na jiwe.
 
Hakuna mtanzania yeyote timamu anayetaka lockdown, Watanzania wanataka uwajibikike kama Rais wao, Watanzania wanataka uwazi wa wagonjwa wangapi wanakufa na wangapi wanaumwa? Watanzania wanataka kujua pesa za misaada ziko wapi? Watanzania wanataka kujua vifaa vilivyonunuliwa viko wapi?

Watanzani labda ungewaambia kwanini umejificha? Watanzania wanataka kujua kwa nini madoctor wanakimbia wagonjwa ? Watanzania wana haki ya kujua yote hayo?

Kama tatizo hakuna tanganza kuanzia leo kazi zote ziendelee kama kawaida.

Fungua shule, Rudi Ikulu uchape kazi au jiuzulu watu wanakufa wanateseka hospitali bila huduma zozote wewe umejificha haileti picha nzuri.

Magufuli unatushangaza sana sisi ndugu zako nakuomba achia Ikulu kama hauwezi kusimama na watanzania kwenye majanga ya Kitaifa.
 
Hehe Chadema mnafurahisha kweli

Mara Hatutaki lockdown mara Tunataka lockdown

Ndio maana hakuna anayewasikiliza maana hamueleweki mnataka nini
 
Serkali ipo makini, visa vya corona vinapungua ukilinganisha na Nchi zinazotuzunguka
 
Mtahangaika saana mmeshakata tamaa, kila mnaloshika linaanguka, 2020 inakaribia muonyeshwe mchezo.
 
Angalau Mungu alisikia maombi yako mleta uzi kuwa Korona Virusi viingie Tanzania.
Mungu hakatai maombi yetu.
 
Angalau Mungu alisikia maombi yako mleta uzi kuwa Korona Virusi viingie Tanzania.
Mungu hakatai maombi yetu.

Hata asingeomba lazima ingeingia tu, kama Mungu anatoa majibu kirahisi hivyo mda huu tunaoandika hapa JF corona isingekuwepo Tanzania.
 
Hakuna mtanzania yeyote timamu anayetaka lockdown, Watanzania wanataka uwajibikike kama Rais wao, Watanzania wanataka uwazi wa wagonjwa wangapi wanakufa na wangapi wanaumwa? Watanzania wanataka kujua pesa za misaada ziko wapi? Watanzania wanataka kujua vifaa vilivyonunuliwa viko wapi?

Watanzani labda ungewaambia kwanini umejificha? Watanzania wanataka kujua kwa nini madoctor wanakimbia wagonjwa ? Watanzania wana haki ya kujua yote hayo?

Kama tatizo hakuna tanganza kuanzia leo kazi zote ziendelee kama kawaida.

Fungua shule, Rudi Ikulu uchape kazi au jiuzulu watu wanakufa wanateseka hospitali bila huduma zozote wewe umejificha haileti picha nzuri.

Magufuli unatushangaza sana sisi ndugu zako nakuomba achia Ikulu kama hauwezi kusimama na watanzania kwenye majanga ya Kitaifa.
Amka kutoka usingizini. Ulikesha unaleta maombi janga hili liingie nchini. Sasa umefurahi? Bavicha mna utoto sana. Siasa mpaka kwenye magonjwa.
 
Back
Top Bottom