Mheshimiwa Rais, ninatambua mpango huu ULIKUWA na nia nzuri, nia thabiti na njema ya kuwapeleka vijana wetu jkt kwa mujibu wa SHERIA na huko wamefunzwa ukakamavu na uzalendo kwa nchi yao.
Mheshimiwa Rais natambua pia serikali inawapeleka vijana kule ikiwa ni njia mojawapo ya kujilinda na kuwa na jeshi la akiba ikiwa matatizo ya uvamizi yatatokea kwenye nchi yetu.
Mheshimiwa Rais kutokana na nyakati tulizopo pamoja na utandawazi wa sasa pamoja na malezi katika jamii, ni wazi vijana hawa wanaweza kukengeuka na kufanya ndivyo sivyo yani kwenda kinyume na kilichokusudiwa na kuleta na athari kubwa katika jamii haswa ikizingatiwa vijana hawa Wana mafunzo ya kutumia silaha na ukakamavu.
Mheshimiwa Rais maoni haya nayatoa baada ya kufanya tathmini ya kilichotokea siku ya tarehe 29, 30 oktoba 2025 katika maeneo flanflan ya miji na majiji katika nchi yetu.
Kwa heshima na taadhima mheshimiwa Rais ninaomba ikikupendeza ufute mpango huu kabisa Ili kupunguza jeshi la vijana mitaani wenye ukakamavu na mbinu za kijeshi ambao tusipoangalia watakuja kuleta balaa. Mheshimiwa Rais nikiwa kama mzazi wa vijana nakusihi futa SHERIA na mpango huo.
Nakutakia mafanikio mema katika shughuli zako za Kila siku katika kutuongoza
Asante