Kwamba Tumefikia Mahala Mfanyabishara Anabembelezwa Kulipa Kodi?

Mazingira ya hii nchi ni magumu sana, yaani kodi zipo kumkomoa mwananchi na si kufanya awe na hali bora.
Watunga sheria ya kodi kubwa kwenye magari harafu wao wanajibanza kwenye VX za Serikali zikichukuliwa tuu wanakufa kwao huko hakuna hata mtu mwenye nafuu...wamefanya magari kama chombo cha starehe kumbe ni bidhaa kama bidhaa zingine tuu uliona wapi Nchi bado inajengwa ila hiyo kodi ya magari ya kubeba mchanga au mizigo ni balaa unakuta bidhaa zinaozea shambani huko Wakenya wenye nafuu wanaenda kuchukua kwa bei ya kutupa Ujinga ni ugonjwa mbaya sana na vinaenda pamoja na Umasikini havitoki kwenye damu unakua na maamuzi ya kimasikini kwa sababu umasikini upo kwenye damu hata upate kazi nzuri vipi utachukia wengine wasiishi maisha bora...
 
Nina mwaka wa 25 nafanya biashara unasema ni mgeni daah nakwambia nilifunga duka karikakoo kwa sababu ya usumbufu wa kijinga miaka ya 2007/8 pana wageni wamehama kuja Dalsm kununua mzigo kwa sababu ya huo usumbufu wa risiti muda mwingine wanachukua hadi bidhaa zao...
 
Tatizo ni siasa.
Serikali ikitaka iwape wote EFD ili iweze wakaba wote, tofauti na hapo isahau. Huwezi wapa wenye maduka EFD, machinga wabaki bila mashine
 
Yupo ndani anaangalia TV ya shemeji yake
Kuna siku pale kariakoo walikuja wale watu wa TRA kama una mzigo wowote unapelekwa ofisini kwao wanaanza kuwafundisha sijui risiti iweje na blah blah kibao.

Imagine wanakuchukua saa tatu asubuhi wanakukalisha huko mpaka saa nane then wanakuachia, Giza likiingia wao wao wanakaa karibu na transporter za mikoani na nje ya nchi kukamata mizigo af wakuombe Hela!

Linakuja kutokea jitu linalishwa na familia yake anaandika ujinga wake
 
Mbona issue imekuuma Sana? Wewe ndo ulikuwa msumbufu Kwa wafanyabiashara?

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
Kasi & mbinu za anayekimbizwa inategemewa na kasi ya anayemkimbiza
 
Tatizo ni siasa.
Serikali ikitaka iwape wote EFD ili iweze wakaba wote, tofauti na hapo isahau. Huwezi wapa wenye maduka EFD, machinga wabaki bila mashine
Nakubaliana nawe, badala ya kuongeza idadi ya walipa kodi kwa ku expand walipa kodi tax base wanazidi kuminya zaidi pasipo na uwiano tija wale walipa kodi wachache
 
Hizo ni siasa za kinafiki za viongozi wetu.
 
Hata mletamada kasema kuna mahali panashida so bado tupo pamoja,
kuna marekebisho yanahitajika Ili mfumo wakuksanya kodi upate kueleweka kwa wafanyabiashara.
 
Nakubaliana nawe, badala ya kuongeza idadi ya walipa kodi kwa ku expand walipa kodi tax base wanazidi kuminya zaidi pasipo na uwiano tija wale walipa kodi wachache
Yatakiwa maduka yote yapewe EFD, Biashara zote zipewe EFD
TRA wakae wasubiri mapato yao
 
Ukicheka na Kima utavuna mabua.
Mfanya biashara wa bongo huyu huyu mjanja mjanja eti unajadiliana naye namna ya KULIPA Kodi alipe kwa hiari? Ukitaka kuamini suala la store na ma godown lilivyoguswa tuu wote wamewaka. Kimsingi maduka ni showrooms tuu. Ma equation yote na makaratedo yapo store na ma go down. Usione wafanya biashara wanalalamika hela hakuna sijui Kodi zimekuwa nyingi ukadhani ni ukweli. Ni waongo wakwepa Kodi wakubwa
 
Wanasiasa wabaya sana, wanachosema kwa wanaanchi ni tofauti na wanachosema kwa wataalamu wa TRA.

Ukweli ni kuwa nchi inahitaji kodi, zingine ziliwe zingine zitumike.

WaTz tujitambue, tubanane na wanasiasa wanaochezea kodi zetu na tujitahidi kulipa kodi, kodi kwa maendeleo endelevu hakuna namna.
 
Kwa mfanyabiashara yoyote kama haujawahi kukutana na kadhia ya TRA bado wewe haujawa mfanyabiashara..
TRA niwasumbufu kupita maelekezo.wanakatisha tamaa sana ya mtu kupambana na biashara..
Nilikutana TRA wanakuja kuomba receipt za Efd saa 7 usiku kwenye bar.
Unakutana na makadirio ya Kodi mil.12mil anakwambia hauwezi funga biashara..ukiongea Kwa ndani anataka rushwa..unampa ruswa Kodi inashuka mpaka laki 6.
Hawa watu ni wa hovyo sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…