Kwamba Tumefikia Mahala Mfanyabishara Anabembelezwa Kulipa Kodi?

Kwamba Tumefikia Mahala Mfanyabishara Anabembelezwa Kulipa Kodi?

Mazingira ya hii nchi ni magumu sana, yaani kodi zipo kumkomoa mwananchi na si kufanya awe na hali bora.
Watunga sheria ya kodi kubwa kwenye magari harafu wao wanajibanza kwenye VX za Serikali zikichukuliwa tuu wanakufa kwao huko hakuna hata mtu mwenye nafuu...wamefanya magari kama chombo cha starehe kumbe ni bidhaa kama bidhaa zingine tuu uliona wapi Nchi bado inajengwa ila hiyo kodi ya magari ya kubeba mchanga au mizigo ni balaa unakuta bidhaa zinaozea shambani huko Wakenya wenye nafuu wanaenda kuchukua kwa bei ya kutupa Ujinga ni ugonjwa mbaya sana na vinaenda pamoja na Umasikini havitoki kwenye damu unakua na maamuzi ya kimasikini kwa sababu umasikini upo kwenye damu hata upate kazi nzuri vipi utachukia wengine wasiishi maisha bora...
 
n

Swala siyo watu kukataa kodi, bali kutunga sheria isiyomlinda mlipa kodi na kumpa mwanya mdai kodi kutumia sheria kushinikiza rushwa.

Wafanya biashara wengi ni wadogo na wanachangamoto katika kutunza kumbukumbu. Hata ukiwa na kumbukumbu sahihi namna gani bado wanatabia ya kuzipinga hizi ili mradi tuu wakubane kukaribisha rushwa.

Hili swala la kutuma taarifa za mali kila mwezi ni ngumu na inatoa mwanya mkubwa kwa mdai kodi kukubana hata pasipo na sababu zozote.

Wewe nadhani ni mgeni na mazingira ya biashara/kodi in practice au umechukulia mfumo wa nchi ya dunia ya kwanza.
Nina mwaka wa 25 nafanya biashara unasema ni mgeni daah nakwambia nilifunga duka karikakoo kwa sababu ya usumbufu wa kijinga miaka ya 2007/8 pana wageni wamehama kuja Dalsm kununua mzigo kwa sababu ya huo usumbufu wa risiti muda mwingine wanachukua hadi bidhaa zao...
 
Tatizo ni siasa.
Serikali ikitaka iwape wote EFD ili iweze wakaba wote, tofauti na hapo isahau. Huwezi wapa wenye maduka EFD, machinga wabaki bila mashine
 
Yupo ndani anaangalia TV ya shemeji yake
Kuna siku pale kariakoo walikuja wale watu wa TRA kama una mzigo wowote unapelekwa ofisini kwao wanaanza kuwafundisha sijui risiti iweje na blah blah kibao.

Imagine wanakuchukua saa tatu asubuhi wanakukalisha huko mpaka saa nane then wanakuachia, Giza likiingia wao wao wanakaa karibu na transporter za mikoani na nje ya nchi kukamata mizigo af wakuombe Hela!

Linakuja kutokea jitu linalishwa na familia yake anaandika ujinga wake
 
Kwamba Tumefikia Mahala Mfanyabishara anabembelezwa kulipa Kodi na anaamua kulipa Kodi anayojigangia si ndio?

Kwamba mfanyabishara wa Tanzania atalipa Kodi bila task force eti maagizo si ndio?

Kwamba mfanyabishara ni ruksa kuficha bidhaa kwenye stoo bubu na kuziuza huko huko bila kulipa Kodi si ndio?

Tusidanganyane hapa hakuna mfanyabishara Yuko tayari kulipa Kodi Kwa hiari hata Mimi binafsi siwezi kulipa..

Nilitegemea Serikali iimarishe kitengo Cha malalamiko na fidia Ili kama Kuna kukadiriwa Kodi isiyo sahihi mtu a file malalamiko yake na ikibainika kuwe na fidia nk..

Pia kero kubwa ambayo hata Mimi naiona kwenye biashara ni wingi wa utitiri wa taasisi za compliance na zote Zina masharti yake,Sasa nilitegemea kuwe na merging ya pesa inayohitajika Ili hizo taasisi za compliance zibakie kwenye ukaguzi sio mfanyabishara kulipa pesa Kila sehemu kama zimamoto,nemc,leseni, Halmashauri,TRA,TMDA,nk
Pesa ingejumuisha kwamba mtu anatakiwa kulipa kiasi Fulani na Kuna mchanganuo kama vile ulinunua mafuta Kuna mchanganuo wa Kodi na tozo..

Kama ni hivyo basi sawa ngoja tuone mwisho wa siku itakavyokuwa ila inashangaza kuvunja taskforce Sasa sijui hiyo enforcement itafanyikaje..
Mbona issue imekuuma Sana? Wewe ndo ulikuwa msumbufu Kwa wafanyabiashara?

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
Kasi & mbinu za anayekimbizwa inategemewa na kasi ya anayemkimbiza
 
Nchi inaongozwa na Mapaka👇😁😁😁
AEb8rs.jpeg
16525976734300.jpg
AEb8rsjc_1.png
ummY_jc.jpg
 
Tatizo ni siasa.
Serikali ikitaka iwape wote EFD ili iweze wakaba wote, tofauti na hapo isahau. Huwezi wapa wenye maduka EFD, machinga wabaki bila mashine
Nakubaliana nawe, badala ya kuongeza idadi ya walipa kodi kwa ku expand walipa kodi tax base wanazidi kuminya zaidi pasipo na uwiano tija wale walipa kodi wachache
 
Kwamba Tumefikia Mahala Mfanyabishara anabembelezwa kulipa Kodi na anaamua kulipa Kodi anayojigangia si ndio?

Kwamba mfanyabishara wa Tanzania atalipa Kodi bila task force eti maagizo si ndio?

Kwamba mfanyabishara ni ruksa kuficha bidhaa kwenye stoo bubu na kuziuza huko huko bila kulipa Kodi si ndio?

Tusidanganyane hapa hakuna mfanyabishara Yuko tayari kulipa Kodi Kwa hiari hata Mimi binafsi siwezi kulipa..

Nilitegemea Serikali iimarishe kitengo Cha malalamiko na fidia Ili kama Kuna kukadiriwa Kodi isiyo sahihi mtu a file malalamiko yake na ikibainika kuwe na fidia nk..

Pia kero kubwa ambayo hata Mimi naiona kwenye biashara ni wingi wa utitiri wa taasisi za compliance na zote Zina masharti yake,Sasa nilitegemea kuwe na merging ya pesa inayohitajika Ili hizo taasisi za compliance zibakie kwenye ukaguzi sio mfanyabishara kulipa pesa Kila sehemu kama zimamoto,nemc,leseni, Halmashauri,TRA,TMDA,nk
Pesa ingejumuisha kwamba mtu anatakiwa kulipa kiasi Fulani na Kuna mchanganuo kama vile ulinunua mafuta Kuna mchanganuo wa Kodi na tozo..

Kama ni hivyo basi sawa ngoja tuone mwisho wa siku itakavyokuwa ila inashangaza kuvunja taskforce Sasa sijui hiyo enforcement itafanyikaje..

Hizo ni siasa za kinafiki za viongozi wetu.
 
Hata mletamada kasema kuna mahali panashida so bado tupo pamoja,
kuna marekebisho yanahitajika Ili mfumo wakuksanya kodi upate kueleweka kwa wafanyabiashara.
 
Nakubaliana nawe, badala ya kuongeza idadi ya walipa kodi kwa ku expand walipa kodi tax base wanazidi kuminya zaidi pasipo na uwiano tija wale walipa kodi wachache
Yatakiwa maduka yote yapewe EFD, Biashara zote zipewe EFD
TRA wakae wasubiri mapato yao
 
Ukicheka na Kima utavuna mabua.
Mfanya biashara wa bongo huyu huyu mjanja mjanja eti unajadiliana naye namna ya KULIPA Kodi alipe kwa hiari? Ukitaka kuamini suala la store na ma godown lilivyoguswa tuu wote wamewaka. Kimsingi maduka ni showrooms tuu. Ma equation yote na makaratedo yapo store na ma go down. Usione wafanya biashara wanalalamika hela hakuna sijui Kodi zimekuwa nyingi ukadhani ni ukweli. Ni waongo wakwepa Kodi wakubwa
 
Wanasiasa wabaya sana, wanachosema kwa wanaanchi ni tofauti na wanachosema kwa wataalamu wa TRA.

Ukweli ni kuwa nchi inahitaji kodi, zingine ziliwe zingine zitumike.

WaTz tujitambue, tubanane na wanasiasa wanaochezea kodi zetu na tujitahidi kulipa kodi, kodi kwa maendeleo endelevu hakuna namna.
 
Kwa mfanyabiashara yoyote kama haujawahi kukutana na kadhia ya TRA bado wewe haujawa mfanyabiashara..
TRA niwasumbufu kupita maelekezo.wanakatisha tamaa sana ya mtu kupambana na biashara..
Nilikutana TRA wanakuja kuomba receipt za Efd saa 7 usiku kwenye bar.
Unakutana na makadirio ya Kodi mil.12mil anakwambia hauwezi funga biashara..ukiongea Kwa ndani anataka rushwa..unampa ruswa Kodi inashuka mpaka laki 6.
Hawa watu ni wa hovyo sana..
 
Back
Top Bottom