Kwangu Mzee Kikwete ndiye baba wa Taifa, hao wengine mnaowasifu hawana maajabu

Kwangu Mzee Kikwete ndiye baba wa Taifa, hao wengine mnaowasifu hawana maajabu

Vipi sheikh!!
Toka mungu wenu anyofolewe roho na Mungu mwenye enzi mmechanganyikiwa mno

Mungu hafi sheikh. Wewe ni Division 5 ?maana unadhani kila anayempinga Kikwete ambaye ni Kilaza atakuwa ni mtu kama wewe? Katika Marais vilaza ambao Tanzania iliwahi pata basi ni Kikwete. Huyu ndo aliwawezesha hata nyie ambao hamna Elimu muajiriwe kwa vyeti fake. Ndo maana mnamwona kama baba yenu. Siwalaumu. Ni uelewa na elimu hamna. Sisi tunapiga kazi na vyeti vinaruhusu.
 
Hello!
Mambo mengi munayoyaona katika taifa hili yalifanyika kipindi cha Rais Kikwete na yale yaliyofanyika kipindi cha Magufuli na Samia mengi yaliasisiwa au kutiliwa mkazo zaidi kipindi cha Kikwete.

Kipindi cha Magufuli tumetangaziwa viwanda hewa maelfu kwa maelfu, kipindi cha Samia sijui tuko kwenye sera ya utalii au nini. Wala sijui Mimi kuwa tuko kwenye kitu gani.

Ukosefu wa ajira uliopo sasa musisingingie ni global issue, ni Magufuli aliyeua sekta binafsi ambaye ni mwajiri mkuu. Ukiua sekta binafsi umeua wananchi wako.erikalini nako tusiseme, ajira alizotoa ndani ya miaka 7 ya utawatala wake ni sawa na mwaka mmoja wa Samia. Takwimu ziko wazi tuache kupamba vitu vya hovyo.

Mimi ndani ya miaka 3 (2013 -2015 ) niliajiriwa mara nne, sehemu zote 3 niliacha kazi mwenyewe, sehemu ya 4 ndiko niko mpaka sasa.

Nilipanga 2020 niachane kabisa na mambo ya ajira ila nilivyoona jinsi sekta binafsi zinavyopepetwa na Mh. Magufuli nikasema siwezi kufanya huo mchezo wa kuacha kazi ya kudumu nikauze vocha au vinywaji vya jumla.

Hata sasa katika utawala wa Samia siwezi kuthubutu kuacha kazi ili nijiajiri.
Sasa hivi hata ukiwa na PhD ndani ya miaka 3 huwezi kuchangia ajira mfululilizo.

Eti unemployment ni global issue, hiyo global issue kwanini ianze kwenye utawala wa Magufuli?

Kuna wakati tunaogopa kusema ukweli maana tutashughulikiwa. Sababu ni uhuru wako kikatiba kutoa maoni bila kumbughuzi mwingine, yes, JK ni baba yako wa Taifa.
Ila Taifa hili, oficially lina baba yake. Hizi nyingine ni mbwembwe tu. Maana haya madhira yote yametengenezwa na watu wawili kwa mfululizo...awamu ya tatu na ya nne.
Mwenyezi Mungu atunusuru waja wake
 
Back
Top Bottom