Mada yako umeichanganya kiasi kwamba ni ngumu kujua point yako kuu iko wapi? Kwanza hapo kwenye red, kwako wewe kuoana ni kuzaa, which is wrong. Kwani mimi mfano nilivyoolewa sikuwa na wazo la kuzaa. Na nilikaa kwenye ndoa 4 years ndio tukafikiria kuanza kuzaa. Kuoana kwa dhati ni msukumo wa mapenzi yaliyopitiliza yanayowafanya watu muhisi mkikaa pamoja 24/7 mtafaidi zaidi!
Pili mada yako inaonyesha unaona ni vizuri mtu kuwa na multiple partners at a time au kubadili partners now and then. Kwangu sioni kama ni poa hata kama kungekuwa hakuna magonjwa.
Tatu as long as jamii duniani kote bado inathamini ndoa (hata wadhungu wanaoana japo wanadivorce daily), kuwa single kwa kiasi fulani kunamfanya muhusika kujihisi socially excluded. Hata ulaya ukimuuliza mtu marital status kama ameoa/ameolewa anakujibu with a smile. Ila kama yupo yupo anakwambia it is a odd question. Why?