Kwani lazima kuoana?

Kwani lazima kuoana?

Kuoa/kuolewa ni moja ya siku kuu tatu za mwanadamu.. vilevile hakuna anayependwa upweke.. vilevile, ni bora uwe peke yako na mwenye amani tele maishani kuliko kuwa ndani ya ndoa na uwe mpweke! Dada usife moyo...muombe mungu...... Mfano hai: Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi kaoa.. tena uzeeni!
 
Sasa sijui na wale waliooa na kuolewa na wanatoka nje ya ndoa zao sijui tuwaiteje? I guess wao wanaheshimika zaidi na "jamii" kwa vile wako kwenye ndoa....

Hahahahahaa! kwa Tz ndio hivyo,akina FATAKI ndo wanaheshimika sana.Yani hii ipo kote hata kwenye uchumi.Yani mtu ukiwa fisadi kazini lazima uheshimike kwenye jamii kwa kuwa una fweza,lakini ukiwa ''mwaminifu'' ndio unaonekana ZOBA.
 
heshima ya mtu inakamilika kwa kuoa/kuolewa?....cku hizi mbona kwenye ndoa uhuni ndio kiboko?.....

Hapana (red) ila kuna mtazamo wa jamii (potofu au la, sijui) kwamba mwanamke ambaya hajaolewa bado hajakamilika. Kuna mama mmoja (ana shule na fweza pia) ila hakubahatika kuolewa. Kuna siku alikuwa anaingia ofisini na giza (gubu) la nguvu kiasi kwamba siku hiyo watu wote wa chini wanamkimbia. Madai ya wengi ni kuwa amekosa mtu wa kumpunguzia msongo wa mawazo na mfadhaiko (frustrations, sijui kama ndiyo tafsiri sahihi.

Suala la uhuni halina uhusiano na kuoa/kutooa au kuolewa/kutoolewa ingawa hiyo hali ni risk factor, kwa sababu mtu wa namna hiyo lazima apate mkate kwa kuwaibia wenzake (scavenging)!
 
Hii ni dhana potofu! Ni nani anayetoa mamlaka ya kuamua kuwa wale ambao hawajaoa au kuolewa ni wahuni? Uhuni ni nini?

asante shem le kwa kweli unagonga mule mule tu

hao wana ndoa ni wangapi wanaongoza kwa kuzini (nyumba ndogo kila kona)

kwa kweli sitaogopa hukumu za macho ya watu as far as the truth is within me....

I will never despair.........uhuni mtu anafanya popote tu kwenye ndoa au hata akiwa hana ndoa!!
 
JF leo imenigomea siwezi ku-quote post pia iko slow sijui wenzangu kama mnakumbana na hili
 
offtopic
charity avatar yako kila nikiingalia na smile nimeshindwa kunyamaza
avatar17204_8.gif
 
asante shem le kwa kweli unagonga mule mule tu

hao wana ndoa ni wangapi wanaongoza kwa kuzini (nyumba ndogo kila kona)

kwa kweli sitaogopa hukumu za macho ya watu as far as the truth is within me....

I will never despair.........uhuni mtu anafanya popote tu kwenye ndoa au hata akiwa hana ndoa!!

cku hizi ndoa ni fashion tu, ili mradi mtu na yeye aonekane ameoa/olewa, uhuni mtindo mmoja, kuumizana tu....
 
cku hizi ndoa ni fashion tu, ili mradi mtu na yeye aonekane ameoa/olewa, uhuni mtindo mmoja, kuumizana tu....

kuna wakati nahisi watu wanaingia kweny etaasisi hii takatifu bila hata kujua maana yake...

maisha kweli yamebadilika, si kifungo cha maisha tena.....
 
mie huwaga najiulizaga pia,kuolewa na kuzaa watoto ni kitu must??? As a young woman...i dont want any of this...nikisemaga hivi kila mtu ananishangaa???labda nikifika huko nitajutia.ila kwa sasa am 26 and yes i dont want to get married..and i dont want children!!........huyo dada nadhani anahitaji moral support....!!
kama hutaki vyote, na kutendwa uache. Vinginevyo utajikuta una mtoto na umeolewa bila kujijua
 
cku hizi ndoa ni fashion tu, ili mradi mtu na yeye aonekane ameoa/olewa, uhuni mtindo mmoja, kuumizana tu....

Nyamayao hapa umeongea kweli tupu ..ndoa zimekuwa kama fashion tu maana imeharibika kabisa...tunakoenda hali ni mbaya zaidi
 
Wanajamvi wenzangu kimsingi "Ndoa" ni agano la msingi kwa binadamu yeyote kama yalivyo maagano mengine kama Upadri,Utawa n.k.Tatizo linakuja kumpata huyu mwenza utakayejiridhisha kuishi naye kwa maisha yako yote haswa sisi wakristo.Hivyo basi ktkt kutafuta mwenza ndipo wengine wanapobahatika kuoa au kuolewa mapema tofauti na wengine lakini la msingi ni Upendo,Kuheshimiana na Uaminifu.Kwa siku za karibuni imeonekana ya kwamba wanaume walio tayari kuingia kwenye Ndoa ni wachache mno ukilinganisha na wasichana wanohitaji kuolewa kwa udi na uvumba.
Hapo ndipo baadhi wanapofikia hatua ya kukata tamaa lakini tumeshashuhudia watu wakioana umri ukiwa umekwenda na bado wakaweza kuishi vizuri ukilinganisha na waliowahi kuingia humo.Hivyo basi jambo la msingi ni kila mmoja kutunza afya yake na kumuomba Mungu kumuangazia mwenza aliye mwema kwa maisha ya baadae.Huu ni mtizamo wangu
 
Kuoa, kuolewa, watoto, familia vyote ni hiyari.

Akikwambia mtu ni wajibu, wajibu kwa kifungu gani? Toka lini tukapangiana maisha? Watakusaidia kukaa na mume/ mke?

Ndoa is really overrated.
 
Mwambie kuoa au kuolewa si lazima.
Ni sawa na kuoga sio lazima uoge ila ni muhimu.
 
Hi,
Ninamshauri huyu Dada atulie muda wake ukifika Mungu atampatia ubavu wake.

Kuolewa ni jambo jema lakini uangalie usije ukatapeliwa na wakora ni vema ufanye uamuzi sahihi

Elisante Yona
 
Wanawake hufikiri kuolewa ni kila kitu, na kwa kawaida ndoa nyingi huwa ni matokeo ya mashinikizo ya mwanamke na jamii.
wanaume wengi hawachulii ndoa 'serous' sana.
 
Wanawake hufikiri kuolewa ni kila kitu, na kwa kawaida ndoa nyingi huwa ni matokeo ya mashinikizo ya mwanamke na jamii.
wanaume wengi hawachulii ndoa 'serous' sana.

Roy kama umefatilia posts vizuri utagundua mtazamo wa watu juu ya mwanamke ambaye hajaolewa......kuna mawazo hasi juu yake

hivyo hizi pressure zinapelekea wanawake ku-despair pale usipokuwa makini, kujitambua n akujiamini. Lakini si kwamba tunafikiri kuolewa ndo kila kitu........puliiiz kheee!!!

social pressure inawatumbukiza wengi sana wasikupaswa kuwa....kama huyu sasa yupo tayari kuolewa na 'yeyote'
 
mimi naona kuoa au kuolewa si jambo la lazima sana

Inategemea mipango yako ya maisha ni nini,pia kama unataka kuoa au kuolewa na mtu au mwenzi wako hujampata haina haja sana kuwa desparate.You will end up in misery!

Ni bora kutulia tu na kumuomba mwenyezi Mungu kama ni mapenzi yake basi lazima utampata anayekufaa au kama ulikuwa kwenye relationship inawezekana kuna aliyekuwa ameandaliwa kwa ajili yako lakini ukapuuza tu
 
Mama, mwambie kuoa/olewa au kutoa/kutoolewa na uamuzi tu, ila kama yeye anapenda sana naaolewe lakini si kila mwanamume atakayekuja manake ataibiwa huyo. Atulie tu kama ni mume atampata tu na aendelee kuomba kwa Mungu kama anaamini katika nguvu ya Mungu!
 
Hii ni dhana potofu! Ni nani anayetoa mamlaka ya kuamua kuwa wale ambao hawajaoa au kuolewa ni wahuni? Uhuni ni nini?

Mhuni ni yule anayetumia tendo la ndoa bila ya yeye kuwa ndani ya ndoa kwani tendo hilo linakubalika katika ndoa tu na si vingnevo. Na ndiyo maana lina sifa ya kuitwa "tendo la ndoa"; tofauti na ngono, uzinzi, uzinifu, zinaaa. Ndiyo maana nikasema huyo dada hataki kuishi kama mhuni, yaani hataki bila ya kuwa katika ndoa kufaidi vya watu wa ndoa, yaani kutumia tendo la ndoa ambalo moja ya malengo yake ni kupata watoto.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom