Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Wasalaam wajumbe!
Mimi ninashangaa sana wanaodai kuwa ooh sijui maandamano yatavuruga amani ya nchi, kwani maandamano si yapo kikatiba na yameruhusiwa kabisa pale mtu anapohisi kua haki yake imepokwa?
Kama waandamanaji wanadai kua maandamano ni ya amani na wao hawatashika silaha au kitu chochote chenye kuumiza watembea mikono mitupu pengine na watakua na majani ya miti tu kuashiria amani, utaitaje kua maandamano ni ya haramu?
Ni askari yupi au chombo kipi cha dola chenye mamlaka ya kufyatua Risasi kupiga raia ambao hawana hatia yeyote anatembea kwa amani? Anaweza kufyatua risasi hiyo kwa mamlaka ya nani na anaruhusiwa kufanya hivyo kwa kifungu kipi kisheria au kwenye katiba ya nchi?
Kama watu wamekamata kura zilizopigwa tayari na ushahidi upo wazi, matokeo yanabadilishwa vituoni watu wanaona, mawakala wanatekwa na wengine wanatolewa kwa nguvu, ni mjinga gani atakayeamini kua huu uchaguzi siyo batili? Mnataka hawa wapinzani waseme kipi zaidi ya kupaza sauti na kutoka kudai haki zao?
CCM inachezea sana amani ya nchi hii, wanatolisha watu, wanajifanya kua wao wameshinda kwa uhalali wakati ukweli wanaujua. Kwakua wao ndio chama tawala hawawezi kuliona hilo na wala hawawezi kufurahia wakiona wenzao wakidai haki zao. Wakae kimya maana vitisho vyao haviwezi kua na maana kwa watu walioamua na ipo wazi kuna wapo watakaoumia kwa sababu ya hawa hawa CCM lakini mwafaka utakua umeshafikiwa.
Kikubwa tuviombe vyombo vyetu vya dola vikumbuke mkataba wao na wananchi kua Risasi na mabomu viliunda kwa ajili ya maadui wa nchi. Wananchi siyo maadui wa nchi hii. Wasisikilize maagizo ya walafi na wachumia tumbo wachache wasiokua na huruma na taifa letu.