Uchaguzi 2020 Kwani Maandamano yana tatizo gani watu kudai haki na ni halali askari kuyazuia?

Uchaguzi 2020 Kwani Maandamano yana tatizo gani watu kudai haki na ni halali askari kuyazuia?

Mpaka leo Kenya wanaendelea kufanya juhudi za kurudisha umoja na mshikamano wa Taifa miongoni mwa wananchi wa itikandi tofauti.

Rejea BBI
 
Mmh! Mgumu kuelewa wewe. Ili uweze kueleewa inabidi urudishwe kwenye tumbo la mamako halafu uzaliwe na mama mwingine.
Ahaaaa,hiki kipigo kimewachanganya sana. Ibara ya 41(4) ya katiba ya JMT inasema wazi uchaguzi unatakiwa ufanyike kwa mujibu wa katiba na sheria. Kama mmeibiwa ni kinyume ya katiba na sheria. Kama ushahidi wenu ni wa ukweli nendeni mahakamani acheni uongo na uzushi.
 
IMG_20201101_130527.jpg
 
Maandamano siyaungi mkono,maana huwa waandamanaji wanakuwa wapuuzi kutaka kulazimisha kila mtu awaunge mkono.

Watu wengine maisha ni magumu hawawezi kuandamana wakaacha kazi zinazowapa mkate wa familia.

Hapo wanataka kutukosea kabisa watanzania.Si kwamba hatuumii kufungwa magoli na ccm,ila umaskini unatunyima fursa ya kuacha kazi na kwenda kuandamana
 
Bado tuna safari ndefu sana, tunayaone kwa wenzetu tu sisi katiba imekaa kama kiini macho hakuna kinachofwatwa humo hata kidogo.

nikuburutana tu, kwani wakituruhusu tuandamane na wao wakawatuma Polisi kulisimamia hilo shida iko wapi? wao siwameshinda kihalali?

Basi watuache tuandamane wao waapishane kwisha.
Tatizo maandamo yamekaa kihaini yani mnapingana na maamuzi ya wengi huo ni uhuni na ushenzi kuna watanzania siasa sio ajira yao Sasa huwezi kuwazuia kufanya kazi zao kisa wewe imepoteza ubunge au urais wako
 
Tatizo maandamo yamekaa kihaini yani mnapingana na maamuzi ya wengi huo ni uhuni na ushenzi kuna watanzania siasa sio ajira yao Sasa huwezi kuwazuia kufanya kazi zao kisa wewe imepoteza ubunge au urais wako
Nisamehe mkuu sijakuelewa kabisa kwa uelewa wangu maandamo yamesharuhusiwa mpaka kwenye katiba ambayo na ww unaiamini na kuitetea, sasa iweje sisi tukitaka kuandamana iwe uhaini? Waliwezaje kusambaza wanausalama kwenye wakati wakupiga kura washindwe kuwatawanya tena kwenye sehemu tutakazo andamana? Mbona mioyo yenu mmeifanya kuwa ni migumu kiasi hicho? Inasikitisha sana na kuumiza ikiwa ya kwamba asie kipenda ccm anaonekana mhani/kibaraka. Mungu tusaidie tuvuke hili.
 
Back
Top Bottom