Uchaguzi 2020 Kwani Maandamano yana tatizo gani watu kudai haki na ni halali askari kuyazuia?

Uchaguzi 2020 Kwani Maandamano yana tatizo gani watu kudai haki na ni halali askari kuyazuia?

Kama ni kweli kwa nini mzichome moto? Kwa nini mliharibu ushahidi?
Wadanganyeni mafala wenzenu
Nani kakudanganya zimechomwa moto zote?[emoji23][emoji23]

Jama kopo hili, hukuona Zitto kabwe Jana amazionesha kwa waandishi wa habari Siku ya Jana?
 
Huku kudharau-dharau nchi yako ndiko kumefanya hatuendelei kwa miaka mingi na ndiyo 7bbu mojawapo kuu wananchi wakawapigeni chini kwenye uchaguzi huu. Hata hivyo, ndiyo maana tunamhitaji kiongozi makini & mchapakazi kama JPM atuvushe kwenda juu zaidi ya hao unaowaghilibu.


Siyo dharau bali ukweli utabaki kuwa hivyo kama tunajadili bila mihemko!

Mojawapo ya namna nzuri ya kutoka hatua moja kwenda nyingine ni pamoja na kukiri udhaifu uliopo kwa wakati huo !
 
Hivi nyie CCM mna akili hata kidogo? Kwa hiyo hizo kura ambazo viongozi wa CHADEMA na ACT wameonyesha vyombo vya habari zimechomwa?

Halafu akili yako kiasi cha kuku hata haijui kuwa katika Tanzania, NECCM ikishamtangaza Magufuli mshindi, hairuhusiwi kupinga mahakamani! Yaani mtaji wa CCM ni ujinga ujinga ujinga. Na watu kama wewe ndio mtaji wa CCM.
Kura feki mlizotengeneza ili kuwadanya wananchi. Acheni upuuzi wenu. Kama ni za wizi kweli ziwekeni hadharani na majina ya waliofoji.
 
Kama mlikamata kura za wizi kwa nini mlizichoma? Kwanini msifungue kesi kupinga matokeo mahakamani na huo ndio ukawa ushahidi?

Maandamano hayaleti mabadiliko ya uchaguzi ambao CHADEMA wameshindwa kihalali.
Aisee
 
Kama mlikamata kura za wizi kwa nini mlizichoma? Kwanini msifungue kesi kupinga matokeo mahakamani na huo ndio ukawa ushahidi?

Maandamano hayaleti mabadiliko ya uchaguzi ambao CHADEMA wameshindwa kihalali.
na kama walizikamata lazima zilikua na mtu huyo mtu yuko wapi?

kwanini wasimuulize kazitoa wapi na nani kampa? huwezi tu kusema

nimezidaka kura feki ziwe tu zimekaa kama furushi la uchafu barabarani.
 
Chadema ushoga unawapeleka kasi Sana...Kenya Mara ngapi wameuana kwa mambo ya kipumbavu kipindi Cha uchaguzi..fanya HV kesho chukua jiwe ingia mtaani kampopoe FFU Amsterdam atakutetea....jiulize marekani kwanini waafrika wanauliwa na hatujawahi sikia Trump anapelekwa Hague...fanyeni kazi madogo


Fahamu kuwa siyo kila mchambuzi / mchangiaji mada anachangia kwa mlengo wa kiitakadi ya chama fulani.

Tujifunze kudhibiti mihemko yetu na huko ndiyo kuwa matured person!

Nikuulize TZ ina jumla ya watu wangapi?
Wangapi ni wanachama wa vyama vya siasa?

Utagundua kuwa waliowengi siyo wanachama wa vyama vya kisiasa lakini wanayohaki ya msingi ya kutoa maoni yao katika mambo mbali mbali bila kwenda kinyume na sheria!

Tafakali
 
na kama walizikamata lazima zilikua na mtu huyo mtu yuko wapi?

kwanini wasimuulize kazitoa wapi na nani kampa? huwezi tu kusema

nimezidaka kura feki ziwe tu zimekaa kama furushi la uchafu barabarani.
Hapo umemaliza uongo wao kabisa.
 
NIMENUKUU

UKIWAONA HAWA KATIKA MAANDAMANO, ANDAMANA!!
---------------------------------

1. Ukimuona Dudley, mtoto wa kwanza na Freeman Mbowe na wadogo zake wakiongoza maandamano nawe andamana. Freeman Mbowe pekee hatoshi, yeye hawezi kupigwa risasi hata moja. Nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani nchini inamlinda, ni jicho la Dunia anatazamwa, hakuna risasi inayoweza kuelekezwa kwake hata moja. Pale Mkwajuni Kinondoni risasi ilimkwepa Mbowe ikamuua Akwiline Akwelina. Wazazi wake wanalia hadi sasa, hakuna kitu. Usipowaona watoto wa Freeman Mbowe usiandamane!!

2. Ukimuona Alicia Magabe na watoto wake wa damu andamana. Alicia ni mke wa Tundu Lissu ambae Urais wa Lissu unamhusu zaidi kuliko mimi na wewe. Ukimuona Tundu Lissu peke yake usidanganyike kuandamana. Lissu ndie aliegombea Urais kwa Chama kikuu cha upinzani akiungwa mkono na ACT Wazalendo, huyu ni icon ya uchaguzi, ndie mwanamkakati ktk maandano hayo. Dunia yote ipo kwake, akifa hakuna cha kujificha, mission INATIKI.

Hakuna Askari mpumbavu anaweza kulenga shabaha ktk mwili wa Lissu, risasi zitaelekezwa kwako. Utakufa na si ajabu usifahamike, taarifa zako hazitofika popote, utakufa kama Mbwa, utazikwa siku inayofuata ktk kabuli la futi mbili au usizikwe kabisa. Usipomuona Alicia na wanawe, usiandamane!!

3. Ukimuona Bi Fourtuna Salehe na Bi Aweina Sinani na watoto wao katika maandamano andamana. Hii ni familia ya Maalim Seif ambayo inasemwa kuwa imepelekwa Oman mafichoni tayari. Wanasema watu wameuawa Zanzibar lkn hakuna jina la mtoto wa Maalim Seif wala wa mtoto wa Jussa hata moja. Usiwe mjinga, hukuzaliwa kuwa chambo, hukuzaliwa kwa ajili ya Urais wa Maalim au Lissu. Wakiwa Marais wewe haitokusaidia chochote. Usipomuona mtoto wa Maalim Seif, wake zake na familia yake jilalie zako nyumbani hauna cha kupoteza.

4. Ukimuona Anna Bwana, Wiza na Josina ktk maandamano yaliyoitishwa na wewe ungana nao, andamana kwa moyo mkunjufu kabisa. Hii ni familia ya Zitto Kabwe, akiwa peke yake muache aendelee na kazi yake. Zitto Kabwe ni Kiongozi wa Chama cha upinzani (KC), ni jicho la Dunia hawezi kupigwa risasi taratibu za kuzuia maandamano zinamtambua na kumlinda. Usipomuona mke wake, watoto na ndugu zake wengine achana na kazi hiyo haina faida itakupeleka kuzimu bure.

5. Ukimuona Askofu Bagonza na mkewe, na watoto wake wote ktk maandamano andamana. Akiwa peke yake muombee kwa Mungu, usijiunge nae. Ukimuona Lema na watoto wake, Sugu na mke wake na watoto zake, Msigwa na wadogo zake kutoka Iringa, Heche na mkewe na watoto wake andamana.

Ukiwaona wao peke yao usiandamane, Ubunge na Urais wao hauna maana yoyote kwako. Maisha yako ni ya kwako peke yako, pambana!!
#USIANDAMANE!!
Huu upumbavu peleka nyumbani kwako. Wanaandamana kudai maslahi ya familia zao au watanzania wote?
 
Polisi haitotoa kibali cha maandamano haya na wanajiandaa kuchapa watu. Akina Mbowe wanajua uchaguzi hautarudiwa lakini angalau ujumbe utakwenda duniani na pressure itakuwa kubwa

Huu ni mwanzo wa Serikali kusalimu amri somehow na kuanzisha mchakato wa kupata Tume Huru ya Uchaguzi.

Yaani Tume isipopatikana ndani ya 2020-2024, CCM wataendelea na mchezo huu huu mwaka 2025 maana wamenogewa sasa
 
Ccm wanatumia mtaji wa ujinga kuwatawala watanzania niliwahi kusema elimu yetu ina shida hasa ya uraia watu hawajui haki zao pia elimu imejenga utii usio na maana hata penye kosa sababu kuu ni neno upinzani limejengewa taswira ni vita, chokochoko,matusi, fujo, ilhali watawala ndio wanaongoza kwa kuivunja katiba ..
 
Hii yote uliyoandika ni UPUUZI.

Hata uwafundishe wawe na PhD kama kura zinaibiwa na NECcm kushirikiana na Policcm hazitavunjwa ni kazi bure


Sasa hayo maswala ya kudai kuandikwa kwa Katiba mpya pamoja na Tume huru na ya Haki ya Uchaguzi yanapaswa kwenda sambamba na utolewaji wa elimu ya Uraia ili kuleta tija zaidi.

Ufumbuzi wa hali iliyopo ni mtambuka kama nilivyoandika hapo juu!
 
Hakuna sheria inayoruhusu maandamano tz


Unashauriwa kurudia kusoma notes zako za Somo la Civis kama ulijaliwa kulisoma au wakati wa topic hiyo inafundishwa ulikuwa na udhuru hukuwepo darasani? Je hukuweza kuwauliza wenzio walichofundishwa wakati ulipokuwa na udhuru?!

Jiwekee mazoea ya kusoma magazeti, sikiliza taarifa za Habari utapata kujifunza na kufahamu mengi ili kusudi kabla ya kuandika au kunena jambo uwe na uhakika usijichoreshe kama hivyo watu wakaanza kupata shaka na kiwango chako cha elimu na ufahamu wako wa mambo ya msingi.

Hata RPCs, IGPs wa Zanzibar na Tanganyika juzi alisema Maandamano ni haki ya wananchi Kikatiba lakini wafuate utaratibu ikiwemo swala la kuomba kibali cha kuandamana.

Ingawa kwenye nchi zilizokomaa kidemokrasia huandamana bila kuomba vibali wala nini.

Kwa huko bongo ni vizuri kufuata utaratibu kwa kuomba kibali kama wanazani kuna unalizima wa kuandamana!
 
Kwanini msifungue kesi kupinga matokeo mahakamani na huo ndio ukawa ushahidi?
Wewe ni mpuuzi na hufai hata kuwa humu JF, nenda Facebook huko. Katiba inasema nn kuhusu kesi za uchaguzi. Unatujazia server tu.

"Wanaoshabikia ccm ni mbumbumbu"..Twaweza
 
Wewe ni mpuuzi na hufai hata kuwa humu JF, nenda Facebook huko. Katiba inasema nn kuhusu kesi za uchaguzi. Unatujazia server tu.

"Wanaoshabikia ccm ni mbumbumbu"..Twaweza
Ahaaaaa, hasira za nini? Halima alitakiwa atunze ushahidi, nyie kwa uongo wenu mkauchoma. Uongo wa kipuuzi kabisa. Kwani rais akiiba kura na ikiwa ni kweli uchaguzi hauwezi kurudiwa?

Nyie ni waongo sana,mnatengeneza uongo ili mpate huruma.
 
Of course iwapo watapewa kibali itasaidia hawa jamaa kupata kupumua maana kilichotokea kwao kiukweli ni mtihani mkubwa sana!

Wasema njia watakazopita na muda ijulikane ili watu wajue kama wanabadilisha njia n..k

Wawaambie wafuasi wao kuwa ni marufuku kufanya fujo wala udokozi wala wizi wowote.

Ilimradi kuwepo amani na utulivu!
 
Nakumbuka uchaguzi wa Kenya ulopita ulikuwa na sintofahamu fulani.

Wapinzani wakaandamana, rais aliyekomadarakani wakati huo Uhuru akayabariki akawaasa polisi wasijewakamgusa mtu yeyote, wao watoe ulinzi tu.

Wakaongea machungu yao, wakatoa nyongo na kuazimia misimamo yao n.k hatimae upepo ukatulia.

Maandamano yale yalifanyika kwa amani na ultulivu na actually yaliwapa kupumua wapinzani na kuondoa attentions kwa watawala na jamii kwa ujumla.

Vivyo hivyo hawa wa bongo nao wanaweza wakalitafakali hili na kuliangalia kwa mapana na marefu!
 
Back
Top Bottom