Uchaguzi 2020 Kwani Maandamano yana tatizo gani watu kudai haki na ni halali askari kuyazuia?

Huku kudharau-dharau nchi yako ndiko kumefanya hatuendelei kwa miaka mingi na ndiyo 7bbu mojawapo kuu wananchi wakawapigeni chini kwenye uchaguzi huu. Hata hivyo, ndiyo maana tunamhitaji kiongozi makini & mchapakazi kama JPM atuvushe kwenda juu zaidi ya hao unaowaghilibu.
 
Nitaandamana!

Lumumba bhana mara mama mkanye mwanao mara hakuna mtu ataingia barabarani.

Sasa vitisho vya nini kama mnaona watanzania hatupo tayari?
 
Kama mlikamata kura za wizi kwa nini mlizichoma? Kwa nini msifungue kesi kupinga matokeo mahakamani na huo ndio ukawa ushahidi? Maandamano hayaleti mabadiliko ya uchaguzi ambao CHADEMA wameshindwa kihalali.
Wewe punguza Ukuda!

Matokeo ya urais yanapingwa mahakama gani?
 
Wapinzani wajipange kipindi kuanzia sasa kutoa elimu ya uraia wafike hadi vijijini huko waweze kujenga capacity building na awareness kubwa!

Because of ignorance and lack of exposure huko mikoani, wilayani na vijijini raia hawana awareness kabisa!

Wakiona polisi na magwanda wanaogopa Yani kama enzi za ukoloni , fikiria?!

Raia anapaswa kujua polisi ni watumishi wetu wanalipwa kodi zetu tumewapa dhamana ya kutulinda raia na mali zetu.

Kule vijijini hao mawakala wakiambiwa hebu tupisheni kidogo tokeni nje watatoka bila hiyana wala kuhoji!

Wapinzani kubalini matokeo tudumishe amani!
 
Simnasemaga watangulie mbele hao, sasa wamesema wanatangulia mbele kuongoza maandamano mmeanza kuhamisha magoli.
 
Sidhani!

Mbona nchi nyingine maandamano ni jambo la kawaida kufanyika mara kwa mara? Mfano Kenya , Je wenyewe hawaogopi mapinduzi?

Labda ufafanue vizuri ueleweke!
Maandamano ya kutokumtambua raisi mteule aliyepo yanakoma wakati gani?
 
Hii yote uliyoandika ni UPUUZI.

Hata uwafundishe wawe na PhD kama kura zinaibiwa na NECcm kushirikiana na Policcm hazitavunjwa ni kazi bure
 
Hata uandike gazeti HAISADIII!

Tunaandamana kama kawa

Lissu , mbowe, zitto, maalim tupo nao wanatosha kabisa
 
Wanajua dikteta hakushinda
 
Fuata taratibu na kwa nini yawe yasio na kikomo
 
Mbona unaruka kama umechomwa kitu kina ncha kali? Nazungumzia kura za kawe mlizodai mnazichoma. Mngezitumia kumrudisha bi kidude.
We KIAZI KITAMU

Halima kurudi peke yake inasaidia nini?

Kwani kawe hazikuibiwa kura za urais?

Kwa kifupi ni nchi nzima kura zimeibiwa na sio utani nimeshuhudia kwa msimamizi kuondoka na bahasha ya khaki nyumbani, kumi na mbili yupo kituoni
 
Wapinzani wakaechini wafanye tathmini ya kina!

Wakubali watokeo tudumishe Amani !

Watafute wafadhili ndani na nje ya nchi, wapange teams za kupita kijiji na mtaa, wawe na roaster na phases!

Watoe elimu ya uraia !

Nia iwe njema na siyo kuleta hasama miongoni mwa wanajamii au serikali na wananchi!

Mpeleke wasomi ambao mtakuwa mmewapa mafunzo kwa muda maalum.

Itabidi muwalipe maana itakuwa ni kama ajira ya mkataba .

Mtaaambia wafanye vizuri ili baada ya evaluation mtawaongezea mkataba kwaajili ya kazi nyingine na kwamba itakuwa renewable kama watajitoa katika kuhakikisha wananchi wanaelewa.

Wananchi wapewe Uhuru wa kuuliza maswali na kujibiwa kirafiki.

Timing itapswa kuwa Nzuri na kuvutia mahudhurio ya wananchi husika.

Ni ushauri tu
 
We KIAZI KITAMU

Halima kurudi peke yake inasaidia nini?

Kwani kawe hazikuibiwa kura za urais?

Kwa kifupi ni nchi nzima kura zimeibiwa na sio utani nimeshuhudia kwa msimamizi kuondoka na bahasha ya khaki nyumbani, kumi na mbili yupo kituoni
Kama ni kweli kwa nini mzichome moto? Kwa nini mliharibu ushahidi?
Wadanganyeni mafala wenzenu
 
Chadema ushoga unawapeleka kasi Sana...Kenya Mara ngapi wameuana kwa mambo ya kipumbavu kipindi Cha uchaguzi..fanya HV kesho chukua jiwe ingia mtaani kampopoe FFU Amsterdam atakutetea....jiulize marekani kwanini waafrika wanauliwa na hatujawahi sikia Trump anapelekwa Hague...fanyeni kazi madogo
 
hata Mwl Nyerere angekuwa na akili kama zako nadhan bado tungekuwa utumwani
 
Hao wanaohimiza maandamano wanajinasibu kuwa ni wabobezi wa kila nyanja za kisheria na katiba. Sasa kama kweli hawana nia ovu dhidi ya Watanzania na Tanzania kwa ujumla kwa nini wasitumie ubobezi wao wa kisheria kutafuta "dhania haki" yao kwa ushahidi huo huo wa " kubumba" unaowafafanulia mleta mada!?

Wanashindwaje kutumia ubobezi wao kwenye jambo ambalo wanaona ni zito kwao!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…