Kwani Makonda alitenda dhambi ngapi? Mbona anataka kuombewa na kila mtu?

Kwani Makonda alitenda dhambi ngapi? Mbona anataka kuombewa na kila mtu?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Kiukweli sijawahi kuona mtu anayetaka kuombewa na kila dhehebu, huyu ni wa kwanza , yaani ukivaa msalaba au Baraghashia , au ukishika Tasbih au Rozali basi atakuvamia umuombee!

Kwanini anataka aombewe na kila mtu , alitenda Makosa gani? Je ni mzima au amepata matatizo ya Ubongo , hivi hawa wanadamu anaotaka wamuombee wenyewe ni waadilifu kiasi gani?

Kwa Mujibu wa Maandiko Matakatifu , Njia pekee ya kusamehewa na Mungu ni kukiri makosa hadharani na kuwaomba radhi kwa mdomo wako wote uliowakosea , vinginevyo ni sawa kutwanga maji kwenye kinu .

Angalizo kwa viongozi wa dini , na angalizo hili mlizingatie , si kila mtu ni wa kukaribishwa mazabauni , mkiendelea hivi mtakumbana na adhabu ya Mungu waziwazi.

Hata sisi waumini wenu hatutakubali mtudhalilishe kwa kuwakumbatia wachafu na wauaji , TUTAWAONDOA KWENYE HIVYO VYEO KAMA ILIVYOWAHI KUTOKEA HAPO AWALI , JIHESHIMUNI

Screenshot_2023-12-01-15-58-57-1.png
Screenshot_2023-12-02-18-40-30-1.png
 
Back
Top Bottom