Kwani ''Mama'' amemalizana na sisi tuliokuwa tunaitwa ''sukuma gang''; Je, kwa sasa ni zamu ya waliokuwa wanafurahia na kufanya sherehe!

Magufuli ametuachia kitu kimoja kikubwa sana nacho ni kujiamini na kuthubutu, Magu alikuwa ni Nyerere wa pili, niliwashangaa wapambe walipoanza kufaya kila hila kumsiliba mwenda zake huku wakifurahi kwa kujikomba bila haya ,hata wale wa upande wa pili wakawa wanaupiga mwingi sana, sasa baada ya mwenyekiti wao kuambiwa ni gaidi wamerudi kwa kasi na kuanza kuchukia mpendwa wao kwa kila aina ya maneno, kwa sisi tunaowajua tulijua ni kwa muda tu huo urafiki wao hautafika mbali, kwani tabia zao hazibadiliki, kwanza ni hao hao walikuwa wanamkejeli mzee wa msoga kwa maneno ya mara dhaifu oh mara Vasco Da Gama, akaja Jiwe naye hawakuchelewa nae lakini Jiwe aliwshawajua hakutaka mzaha nao, sasa amekuja mwenye maneno matamu wakapiga mbinja na kujifariji hasa baada ya kuona mmasai pamoja na wale wengine wakiondolewa kwenye nyadhifa, jamaa ah wakaona sasa ndio wao, mwishowe sasa wanasaga meno, hawa jamaa kila uongozi ni mbaya kwao sijui wanataka malaika ndio awatawale, shida wanaongozwa na hao sijui akina Maria Sarungi na Fatuma, wamesahau kuwa hawa wadada wana msongo...
 
Alijipima kwa nguvu ya hayati mjeshi akaona ubavu mdogo akaachana nasi kiaina, sahivi kawa uchochoro anafungisha wenzie
 
Daah siasa za bongo ni hatari...

Kuna watu walijipa utaalamu wa siasa humu, huku hawajui lelote kuhusu siasa

Naamini kuna kitu wamejifunza,sisi yetu macho

NB: natamani hili jina la sukuma gang waendelee kulitaja hadi 2025, waje tuwaoneshe nguvu yake.
 
Kama walimmisi JK ambaye walimtukana sana naamini hata hayati JPM watammisi sana
 
Mama anacheza Kama Pele,alianza akawapa pipi kwa kumtia nguvuni Sabaya,wakashangilia,alipopiga tikitaka hatari majibu mazuri atatupa yule mwenyekiti wa kudumu.
Siasa za Tanzania ni ngumu sana kama huzijui! Hawakujua yanayotokea kwa sasa!
 
Yani walisahau msemo wa kizungu usemao " what goes around comes around"

Tunazidi kuwashangaa na mshangao wetu hautaisha kuwashangaa hadi pale watakapoacha kushangaa kama sisi tunavyoshangaa!
 
Reasonably fair analysis.
 
Wasije jaribu kuja kwenye kumsifu Magufuli.
Watulie huko huko


Sent using Jamii Forums mobile app
Magufuli alikuwa na mazuri yake. Hilo halina ubishi. Hivyo watu waliyo neutral, wasioegemea upende wowote ni lazima watakiri na kuna wakati wata-mis. Lakini kwa upande mwingine Magufuli alikuwa na mabaya yake. mbaya zaidi yale mabaya yalikuwa mabaya kweli kweli. Ni watu wangapi wamekufa au kuumizwa na hata kuwa vilema kwa sababu yake? Ulitegemea mtu aliyeponea chupu chupu kufa na bado akanyimwa stahiki zake nyingi tu kama Lissu ahuzunike kwa kifo cha Magufuli? Sasa hao wako wengi sana. Adui yako ambao hujui ni lini atakuua akifa hutafurahia? Com'on. Tusijtoe ufahamu kwa vitu vilivyo wazi. Ukweli ni kuwa pamoja na mazuri ya Magufuli, lakini kifo chake kimeleta faraja kwa watu wengi sana. Mtu kama Sabaya alikuwa na kibali cha kufanya umafia kwa watu wasiyo na hatia bila kuulizwa. Na hata kama walikuwa na makosa kuna njia za kuchukuwa!
 
Kilio cha Kukumbuka Magu kitasikika 2025 Pale Moguls Na Prominent watakapo take over majimbo, Wabunge almost wote wamepita kwa mbeleko ya JPM wajiandae kulia
 
Kinachonishangaza ni kuwa wananchi wamempotezea mbowe wamekomaa na miamala na tozo mwanzo mwisho mpaka kieleweke.
 
Aisee mkuu ningekuwa karibu yako ningekununua hata maji ya baridi kuonyesha heshima kwa ulichoandika. MsemajiUkweli anaujua ukweli ila ameamua tu kukebehi. Precedence aliyoweka Magufuli ni mbaya sana sana na itachukuwa mika na miaka kuifuta. Kiukweli ametuharibia nchi sana sana. Hebu fikiria tu uchaguzi uliopita jinsi ulivyokuwa. Kabla ya hapo hatukuwahi kuwa na uchaguzi wa kihuni namna hiyo. Marais wajao wote tayari wameshafundishwa uhuni wa kufanya. Kuja kutoka kwenye chaguzi za aina hii itakuwa ni kwa machafuko makubwa. Bila kufumua system nzima na kusuka upya mimi mbele naona giza. Kuna wanaodhani Mbowe na wapinzani tu ndiyo wataathirika kumbe hili ni janga la watanzania wote.
 
Kinachonishangaza ni kuwa wananchi wamempotezea mbowe wamekomaa na miamala na tozo mwanzo mwisho mpaka kieleweke.
Na wajinga wanadhani Mbowe ndiyo anakomolewa kumbe watanzania wote ndiyo wahanga.
 
Nakubaliana na mtazamo wako!
Kuna wanasiasa hasa ukiwajua malengo yao hawawezi tena kukusumbua kifikra.
 
Manung'uniko na ubambakiaji wa kesi vyote hivi vikizidi hasira ya Mungu itawaka, kuna mambo huwa nayafukiria sipati jibu hadi leo [emoji17]
Duuh una amin sana katika Mungu
Watu wengi wamewahi kufa katika historia wanavyokufa hasira ya mungu kwa nn iwake baadae na sio huruma yake kuzuia kwa muda huo
 
Hoja yako ni nzito lakini imebeba ukweli halisi wa siasa zetu nchini hasa upande wa wapinzani!

Ninakubaliana na angalizo lako.
 
Alijipima kwa nguvu ya hayati mjeshi akaona ubavu mdogo akaachana nasi kiaina, sahivi kawa uchochoro anafungisha wenzie
Duh!
Maoni yako yamenifanya nicheke!

Kwamba alijipima kwa nguvu ya mjeshi akaona ubavu mdogo na kuachana nasi kiaina! Inawezekana atarudi tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…