Kwani mkiachana lazima muwe maadui?

Kifamilia tu hakuna mgawanyo wowote wa mali
Kwahiyo hakuna talaka..
Je mlioana na mna cheti cha ndoa?

Maana kama mlioana na hamjaachana kwa talaka basi hiyo ndoa bado imooo na huwez kuoa mke mwingine kama wewe ni mkristu
 
Kwahiyo hakuna talaka..
Je mlioana na mna cheti cha ndoa?

Maana kama mlioana na hamjaachana kwa talaka basi hiyo ndoa bado imooo na huwez kuoa mke mwingine kama wewe ni mkristu
Ndoa ya kikristo na cheti kipo
 
Mkuu idhindi wa mambo magumu tayari unao.
Huenda sasa unaogopa jamii au ndg.
Mrudishe mzinzi mwenzako mmalize uzee huenda amejifunza
Hata biblia imekataa kumrudia mwanamke mzinzi halafu ndio unataka arudiane nae kisa tu walizaa pamoja
 
Baada ya miaka 6 huyo ex wake alipata ajali na alihitaji kuongezewa damu. Vin Diesel aliwahi haraka hospitalini kwenda kumuongezea damu na alipopona wakarudiana!
Huko alikokuwa alikuachaje? Au anasubiri nako kuishiwe damu akimbilie kudonate
 
Ndoa ya kikristo na cheti kipo
Basi kumbe hamjaachana ila mlichofanya ni kukubaliana kutokubaliana ndio maana mnaweza kuendelea hivyo.
Ila mkiachana kwa taraka mkagawana mali ile set back ya kurudishana nyuma kiutafutaji ndio ambayo hutengeneza chuki na kutotaka hata kuonana
 
Acha uhuni bro.
 
Wanawake wa Kiswahili wanatapika nyongo utasikia:-
Kibamia hicho
Kimoja chali
Mbahili
Shetani/Jini
Yaani anatukana baba/mama mkwe kama wame mkosea[emoji1787][emoji1787]
Tuliwahi kugombana na mchumba wangu akanitukana "mbwa wewe" baada ya hilo tusi nilikaa kimya, sikuwahi kumtafuta kwa namna yoyote(sio text wala kupiga simu)

Baada ya wiki mbili alianza kunitafuta na kutaka tuonane kwa mazungumzo, sikumjibu, akaanza kuniomba msamaha, sikumjibu kwa lolote mpaka leo, imeshapita miaka 2.5 sijawahi kuwasiliana naye!
,
Kuna mahusiano mengine hata huko friends zone hayafai kuwepo, unamsahau mtu kana kwamba hujawahi kumjua kabisa!
 
Kwa hiyo mkeo kageuka demu wako, ila tofauti ni kwamba haumuishi pamoja basiii...
 
Nimeipenda couple yenu

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Mstari unaotenganisha chuki na upendo ni mwembamba sana.
 
Kwa bongo kurudiana na mtu aidha ameshindwa kule alikoenda au anarud kukufanyia mbaya....full kulogana yaan tafran
 
Mkuu nakuelewa mwanaume anaumia sana akiwa na hakika "mkewe", narudia tena mkewe ameliwa na fulani hii huwaga haiishi milele hata kama ikitokea mmesameheana.

Mara nyingi matokeo huwaga ni hayo, mwanaume kubadilika sana, hasira zote anamalizia kwa wanawake wengine anakuwa Malaya sana, na asipokuwa makini anaweza pata magonjwa.

Ila, siku kaa chini tafakari, ya kuwa je wewe hukuwahi m' cheat mkeo? Au ni mara ngapi umefanya hivyo na mmeyaongea na yakaisha? Kama aliweza kukusamehe kwa hayo na mengine uliyoyafanya wewe bila yeye Kujua basi, mkuu piga moyo konde, mrejee mkeo na mlee watoto. Kwani madhara yatokanayo na kutengana kwenu ni makubwa zaidi kuliko mkipambana kurejesha ndoa yenu. Tafuteni mtu either mwanasaikolojia au kiongozi wa dini mzungumze nae kwa kirefu sana.

Mkuu, chini ya jua hakuna mkamilifu, sote tuna makosa na hukosea sababu ya ubinaadamu wetu, haukuanzisha familia ili siku ifike mtengane kwani muwape watoto madhira kwa mambo yenu binafsi- watoto wana haki ya kuenjoy raha ya kukua na familia na siyo vinginevyo, ndoa ina changamoto nyingi na ni Safari ndefu sana.

Lakini ndoa ina siri kubwa mnooo, ambazo kila mtu akizisema hapa unaweza Sema ya kwangu ni ya kawaida. Bro hakuna ndoa ambayo haina changamoto, ukiona watu wamezeeka kwe ndoa jua tu wamepita changamoto nyingi sana, busara ya hali ya juu imetumika pamoja na uvumilivu usiowa kawaida.

Muhimu mmepeana nafasi (space) kwasasa, ni jambo Muhimu kwa kila mmoja wenu kujitafakari wapi alikosea na nini anatakiwa kufanya kama fursa ya kurudiana.
 
Kiongozi wa dini tena,yani umerudie Mwanamke mzinzi eti kisa tu na yeye kama Mwanamke alishawahi kulala na wanawake wengine?,utakuwa ni upumbavu wa karne.

Tambua fika mwanamke aliyechepuka ataendelea kuchepuka mpaka Mwisho wa maisha yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…