Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,379
- 41,294
Nafikiri umeongea kwasababu ya ubinafsi zaidi..yan unampaka nafuta kwa mgongo wa chupa
Hapana, hujaelewa maandishi niliyoandika....
Binafsi sipendi ugomvi kugombana kukwaruzana hata kubwatukiana sipendi....
Nimekukera niite niambie Kasinde umezingua na umenikera na umeniboa...
Nami ukizingua nakuita nakwambia kistaarabu umeharibu na nimechukia....
Napenda amani, hata kama nimechukia napenda kumaliza tofauti kwa amani, kisa cha alubati kimenifikirisha namna dunia ingekuwa wanaume wangeishi namna hiyo....
Kikubwa amani ya moyo, ikifika mahala mwanamke/mwanaume amekusaliti kama huwezi kukubali basi utulie uvumilie uwe bwegez uishi kibishi.
Ama laah unaanza upya unaendelea na maisha yako vile unapenda/unataka.
Simsifii mtu, nimeukubali utashi alioutumia, kuna mambo mengine hayahitaji nguvu, akili tuu mtu wangu.