Ni ajabu kuona mpaka leo watanzania wanashindwa kuelewa binadamu tuko tofauti na hatufanani.
Humu kuna watu wanaanzisha nyuzi za Introverts na Extroverts lakini wengi bado hawajifunzi na wanaona kama utani au sifa fulani.
Huyo bila shaka atakuwa ni Introvert na ndio alivyo hivyo, kama hujawahi kukutana na watu wenye sifa hiyo basi hiyo itakuwa mara ya kwanza mkuu.
Wanawake wa aina hiyo mara nyingi wanakuwa smart kichwani sio mchezo hauwezi kulinganisha na hawa micharuko wanaopenda kuongea nonsense 24 hours a day kama wamemeza cassette.
Wana akili na wanajitambua sana na wanajua kukusoma yaani bila kuongea anajua kama una tatizo au kuna kitu unataka na hakuna siri kati yenu, kwa kutoa ushauri wenye akili ndio acha kabisa pia ni watafutaji wazuri na wanatulia sababu wanajua thamani yao na wanajua wanachokitaka.
For me that's what I call a perfect Woman, ni zaidi ya yule aliyemuimba Ed Sheeran. na bila shaka hamuendani mkuu.
Hiyo ni fursa inayojitokeza mara moja ndani ya maisha yako yote sababu hao wanawake wapo mmoja kati ya 1000 na ukibahatika kumpata mmoja then it's a gift from the God.
Eminem angekwambia this opportunity comes once in a lifetime.
Na inahitaji mtu mwenye akili na anayejua anachokitaka kuwatambua " kuzitambua those diamonds and golds in the rough",
Damn it! I wish hiyo opportunity ningeipata mimi, mkuu hao ndio wanawake wa kutengeneza nao maisha lakini bad news inaonesha hamuendani.
Binadamu unatakiwa kusoma wengine ili kuwa adaptable sababu sio kila mtu yupo kama wewe, na wengi mnashindwa hili.