Imani hii kupitia social media, forum za mitandao ya kijamii za wazi na siri pamoja na gaming apps wanawarubuni watu wa imani yao kufanya ugaidi kwa visingizio kibao.
Imani hii huwalenga watu kama waraibu wa madawa ya kulevya, watoto katika vituo vya mayatima au wasiona uwezo kiuchumi, raia wenye mtindio wa akili kuwarubini kutekeleza ugaidi
Nini kifanyike? Taasisi za kidini, familia zenye watu wenye uraibu wa madawa ya kulevya washirikiane na serikali ili ndugu zao wawekwe kwenye nyumba sahihi za sober House pia wale watakaogundulika na matatizo ya afya ya akili wapatiwe huduma za kiafya kabla hawajaingia katika mikono ya watu waovu magaidi watakaotaka kuwatumia watekekeze uovu.
taasisi za dini zilizoazimia kufanya utafiti ili matokeo ya utafiti huo yaweze kuisaidia Serikali zijikite
- Kubaini wanaoshiriki kurubuni ili kuzuia tendo la kigaidi lisitokee
- Taasisi za kidini kubaini na kuwalinda wale wanaolengwa kurubuniwa kujiunga na ugaidi
- Viongozi wa kidini ni watu wa mwanzo kabisa wa kuweza kubaini watu wenye mrengo wa kurubuni katika jamii yao
- Taasisi za kidini viongozi wao wote wapelekwe kwenye mafunzo chuo cha ulinzi wa taifa
- Viongozi wa kidini kuwa macho na kuripoti serikalini vitendo vinavyoashiria uwepo wa baadhi ya waumini wao wenye mirengo ya hatari
Jinsi ya Kubaini watu wenye misimamo mikali inayoenda kinyume na utaifa wa Tanzania.
Watu hao hupaza sauti kupinga umoja wa kitaifa kwa kupanda mbegu za wale wao na sisi sisi. Hawana uvumilivu wa tofauti za kiimani zilizomo ndani ya taifa.
Watu hao huandika makala ya kufifisha uwezo wa ulinzi na kiusalama wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama mfano kuingiza ushawishi wa kiimani katika jeshi la ulinzi hivyo kushiriki katika kuhatarisha ulinzi wa mipaka na usalama wa ndani wa nchi .
Watu hao wenye misimamo mikali ya kiimani nchini Tanzania huchekelea pale mtumishi wa vyombo vya ulinzi anapopoteza maisha kwa kushambuliwa na mtu wa imani yao.
Watu hawa huwa wamekulia katika mazingira ya ukatili, upweke, familia zilizovunjika, wahalifu wanaodai wameongoka, makundi waliyopo yanawapa mbinyo watende vitendo viovu waweze kukubalika ndani ya kundi lao dogo la watu wachache, hawajiamini siku zote kulaumu wengine ...
Watu hao huapa na kula yamini kushirikiana na watu wa nje wa imani yake kuidhoofisha Tanzania kwa kila namna ikiwemo kuwakataza waumini wao kujiunga ktk vyombo vya ulinzi na usalama, kuleta ushawishi wa utengano kwa kufuata imani ktk vyombo vya ulinzi na usalama.
Watu hao hawalali kwa kupakua, kusambaza na kuchapisha makala ya kuchochea migongano ya kiimani .
Mohamed Abubakar anaonesha ni mtu anayehitaji msaada wa kuelimishwa na viongozi wa imani yake. Anaonesha dalili na chembechembe za kurubuniwa kwa kufahamu au kutofahamu.
Ni muda sahihi wa utafiti huo kuwalenga watu kama Mohamed Abubakar na kuwapa msaada sahihi wanaostahili ili asiendelee kutumbukia katika shimo la msimamo potofu.
Tuendelee kumsoma na kumpa nasaha sahihi za kuweza kumsaidia aweze kuzinduka kutoka kurubuniwa na watu wachache waovu wavunja nchi ili asishiriki katika dhambi hii ya kuvunja taifa.