Kwanini ACT-Wazalendo wanaishitaki Serikali ICC badala ya Mahakama ya Afrika Mashariki? Huu ni uzalendo?

Kwanini ACT-Wazalendo wanaishitaki Serikali ICC badala ya Mahakama ya Afrika Mashariki? Huu ni uzalendo?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Tunazo mahakama za Afrika na mahakama ya Afrika mashariki lakini ACT wazalendo wamevuka mipaka hadi bara la Ulaya kupeleka malalamiko yao ya kisiasa.

Je, ICC ni bora kuliko mahakama za Afrika?

Je, ACT wazalendo ni wazalendo kweli?

Maendeleo hayana vyama!
 
Afrika Mashariki wana uwezo wa kumkamata Magufuli? Au hata Simon Sirro?

Al Bashir wa Sudan akiwa madarakani alijidai sana kama anavyojidai Magufuli sasa, na aliikejeli ICC kuwa si lolote si chochote, sasa habari yake kila mtu anayo, except Magufuli, I guess
 
Mahakama zote ulizotaja hapo hazina meno na haziwezi kutoa hukumu sawasawa na matendo yaliyofanywa, mara nyingi huwa zinahafifisha kuhukumu na kupitisha vifungo rafiki kama kufanya suruhu kwa wahusika.

Kama unafuatilia, mfano ni kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na late mchungaji Christopher Mtikila kwa mahakama hizo, ilihishia wapi?
 
Umesema Africa Mashariki...Marais wake ni akina nani vile? Jiwe, Kagame, Nkurunzinza na Museveni..hawa si ndio wanatoa pesa za kuendesha hizi Mahakama...kama hujatumwa jiongeze...
Katika maraisi wa Afrika Mashariki, wanaoripotiwagwa mara kwa mara huko ICC, aliyefunguliwagwa kesi na hiyo ICC ni nani vile????
KENYATTA peke yake.
 
Back
Top Bottom