Kwanini ACT-Wazalendo wanaishitaki Serikali ICC badala ya Mahakama ya Afrika Mashariki? Huu ni uzalendo?

Kwanini ACT-Wazalendo wanaishitaki Serikali ICC badala ya Mahakama ya Afrika Mashariki? Huu ni uzalendo?

Afrika Mashariki wooteee ni wale wale tuu ni kama kupeleka kesi ya nyani kwa Sokwe.
 
Africa mashariki huwa wanahalalishiana maovu yao kwa awamu so hawaaminiki....
 
Unafikiri waliopeleka hawajui hilo?
wangejua wasingefanya hivyo! Hiyo ni kutapata kwa mfa maji, kwani inaonekana kama hawajuii Rome statute; polisi kutumia nguvu kuzuia watu wasivunja sheria halali siyo mojawapo ya mambo manne yaliyoko kwe statute hiyo.
 
Tunazo mahakama za Afrika na mahakama ya Afrika mashariki lakini ACT wazalendo wamevuka mipaka hadi bara la Ulaya kupeleka malalamiko yao ya kisiasa.

Je, ICC ni bora kuliko mahakama za Afrika?

Je, ACT wazalendo ni wazalendo kweli?

Maendeleo hayana vyama!
Inapotokea watu kama Pius Msekwa, Butiku, Sinde, Msuya, Mongela, Malecela, Anne Abdalah, Yusuph makamba, Mzee Mwinyi, Kikwete, wote wote wamenyamazishwa na conflict of interest taifa linaelekea wapi?

Heri ya hao wanaojaribu ICC huwenda wakawa jiwe waliloliacha waashi kuinusuru nchi. Kwenda ICC ni teke la mwisho la kidemokrasia kuelekea kukata roho au kuingia hatua nyingine zisizo za kidemokrasia

Kama baba wa taifa angekuwa hai angewazaba vibao hawa wazee wetu. Hawa wazee wetu tunawatuza kwa masilahi yao na familia zao tu basi. Wafungwa midomo na familia zao.
 
Umesema Africa Mashariki...Marais wake ni akina nani vile? Jiwe, Kagame, Nkurunzinza na Museveni..hawa si ndio wanatoa pesa za kuendesha hizi Mahakama...kama hujatumwa jiongeze...
Ndio wanateua majaji pia
 
Lete ushahidi bwashee au mbege imeshapanda kichwani?
Lazima uwe mpum.avu hasa kuulizia ushahidi wa watu waliouawa. Majina yametajwa, picha zimeoneshwa, watu wameshiriki mpaka maziko yao, matundu ya risasi yapo mwilini mwa marehemu, halafu eti unataka ushahidi!! Kichaa mkubwa wewe.

Au unataka uingizwe kwenye kila kaburi la marehemu ndiyo uamini? Au mpaka auawe mama yako au mwanao ndiyo ujue thamani ya uhai wa mwanadamu? Wewe ambaye huwezi kuona thamani ya uhai wa mwanadamu mwenzako lazima utakuwa unaishi na roho ya shetani ndani yako.

Mungu mwenye mamlaka yote, tunakuomba, mtu huyu aoneshwe thamani ya uhai wa mwanadamu kabla ya kuonfoka kwake Duniani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom