Kwanini ACT-Wazalendo wanaishitaki Serikali ICC badala ya Mahakama ya Afrika Mashariki? Huu ni uzalendo?

Bushiri hakutolewa kwenye Madaraka na ICC isipokua na wanainchi, so wanainchi ndio kila kitu na sio ICC
 
Kwanini Wanazengo wasipewe nafasi wajichagulie mjumbe kumi wao bali kiongozi wajuu ndiye awateulie kiongozi wao?Hapo ndiyo utapata jibu ulilo uliza kuhusu ACT kwenda huko
 
Jiwe akafie mbali huko ICC. Anastahili kabisa.
 
Muwe mnaweka uzalendo kwanza kwenye kutenda haki, mnataka wengine wawe wazalendo wakati vyombo vya kutenda haki mmeshika nyie visitended sheria? Mahakama ya Africa ina tofauti gani na wale mazuzu wa waliosema kuiba kura ni uchaguzi Huru na wa haki?
 
Unafikiri waliopeleka hawajui hilo?
 
Uzalendo ni kutumia majeshi kuua, kuteka na kutesa raia pamoja na kuiba kura.
Kwa hoja yako hiyo, NANI HASA NI MZALENDO?

Je,

Mzalendo ni yule anayepanda kwenye jukwaa la siasa na kudharilisha wagombea wasio wa chama chako ikiwemo Rais aliyeko madarakani ambaye pia ni mgombea Urais kupitia Chama ambacho yeye ni M/Kiti!

Mzalendo ni wa huyo M/Kiti wa hicho chama kubeza wagombea Urais wa vyama vingine vya siasa hadharani kuwa hawana sifa za kuwa wagombea?

Wazalendo ni wa hao viongozi wa vyama hivyo kumtosa mgombea wa Urais kupitia chama chao katikati ya kampeni?

Uzalendo ni kupinga kila aina maendeleo yaliyokwisha kupatikana kuwa su chochote wala lolote?

Uzalendo ni wa hao wanaokimbia nchi baada ya kuhamasisha maandamano yasiyo na kikomo ili nchi isimame kwa shughuli zote kwa sababu waliadhibiwa kwenye sanduku la kura?
 
waangalizi wa afrika mashariki wanakwambia uchaguzi ulikuwa huru na haki halafu upeleke tena kesi kwao
 
 
Wanahangaika tu ICC haipo kwa ajili ya kusikiliza mashitaka dhidi ya chaguzi, kama ni hivyo Trump pia angepeleka malalamiko yake huko
 
Tumbili akikukosea huendi kumshitaki kwa nyani
 
Kufungua kesi ni jambo lingine na kushinda jesi ni jambo jingine. Ingekuwa busara watu wanyamaze mpaka mahakama itoe maamuzi.
 
Nop, Uzalendo ni serikali kuuwa raia wake baada ya kujiweka madarakani kwa ngunvu.
 
Wana haki kushitaki popote
 
Jiulize na wewe,siku zote kushabikia maovu na uonevu,je ni uzalendo wa aina gani,uzalendo halisi au maslahi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…