Actually huo ni uchaguzi na pia na ni aina ya Demokrasia maeneo husika yameamua kuichagua na kuitekeleza.
Mathalani Niger, Rais Mohamed Bazum ni kweli alichaguliwa na wananchi kwa kura lakini pia Jeshi lilipompindua wananchi kwa maelfu walijitokeza tena ktk uwanja wa mpira na maeneo mengine nchini humo, kuunga mkono Jeshi kwa Mapinduzi ya Amani, lakini zaidi sana kumuunga mkono Gen. Abdoulrahame Tchiani kwamba ndio kiongozi wao.
Hali hii imetokea pia maeneo mengine kama vile Burkina Faso, Mali na Guinea.
Wananchi kuunga mkono Jeshi na viongozi wa Mapinduzi ni Demokrasia pia Lazima wananchi waheshimiwe Mawazo na matakwa yao.