Sababu za mapinduzi zipo tofauti,kushindwa kwa serikali kuongoza nchi vyema,maslahi ya jeshi yakipuuzwa,Rais kutofautiana na jeshi,kung'ang'ania madarakani kwa muda mrefu n,k.
Gabon kama nchi kiuchumi iko vizuri,akuna nchi ya africa ilifanya uchaguzi pande zote wakakubali matokeo.ilikua ni kosa jeshi kukubali Ally Bongo kung'ang'ania akuongoza wakati sio mzima ki afya.
Uko sahihi sana kiongozi,
Mathalani Niger,
ufaransa iliamuru Rais Bazum kumtimua kazi mkuu wa majeshi Gen.Tchiani ambae sasa ndie kiongozi wa Mapinduzi, kwa mtazamo wake tofauti na Rais Bazum kuhusu uwepo wa makambi ya Jeshi la ufaransa na Marekani ktk ardhi ya Niger. Sasa b4 hajafutwa kazi akafanya yake na kazi ikawa imekamilika.
Hizi ni miongoni mwa baadhi ya sababu nyingine zilizopelekea Mapinduzi na zitakazoendelea kuwaondoa mamlakani viongozi wengi barani Africa.
Usaliti miongoni mwa viongozi.
Kuzorota kwa uchumi kupindukia,
Kuzorota kwa hali ya kiusalama,
Umaskini wa kutupwa,
Rushwa kupindukia na iliyokithiri kitaasisi.
Ukosefu wa ajira kwa vijana.
Nguvu ya mataifa ya nje kiuchumi na ushawishi ndani ya serikali za Africa.
Kuzorota kwa hali za maisha ya watu na makazi yao.
Njaa na ukosefu huduma muhimu za afya, maji, umeme, Elimu n.k.
Kutofautiana falsafa ya kuongoza. nchi miongoni mwa viongozi.
Uchu na ulafi wa Madaraka.
Kupuuzwa kwa Katiba, utawala wa Sheria na utawala bora.
Kubinywa na kukandamizwa kwa haki na uhuru wa habari na kujieleza.
Kupuuzwa kwa Demokrasia.
Kung'ang'ana Madarakani kwa nguvu au kwa wizi wa kura.
Kukandamizwa haki za binadamu na usawa.
Mabadiliko ya Katiba na Sheria mbalimbali za kuwabakiza viongozi mamlakani.
Haya ni baadhi tu ya mambo machache yanaweza kuchochea Mapinduzi.