Kwa kweli Afrika sijui niseme nini, sasa hata kule Niger ECOWAS itazidi kupata kigugumizi cha kuwaondoa wale wanajeshi waliopindua serikali halali. Na hakuna ushahidi wanajeshi wataleta neema wananchi wanayodhani wataipata. Ni sawa tu na nchi nyingine kama Kenya, Tanzania nk. ambazo wananchi wanakuwa na mzuka kwa raisi fulani anapogombea kisha akikaaa kidogo madarkani wakibaini hawezi kutimiza zile shauku zao wanaanza kumchukia ghafla.
Mfano HAPO KENYA Ruto alidhaniwa ataleta neema ya kiuchumi lakini ilivyoonekana neema haipo kirahisi walewale waliomchagua wanaanza tena kuandamana. Sudani ni hivyohivyo walimtoa Albashiri nini sasa wamepata?
Ni bora wananchi wenyewe wangeandamana jeshi likawasapoti lakini siyo kujifanya linachukua madaraka huku haijulikani ni lini watayakabidhi kwa raia, wanajeshi ni binadamu kama walivyo hao maraisi kwahiyo tusishadidie sana jeshi kushika madaraka.
Nadhani kuna mkono wa Urusi hata kama siyo moja kwa moja lakini Putin na New Order yake ana agenda fulani ya siri na Afrika tusipoangalia tutageuka vibaraka wa Urusi sawa tu na tulivyokuwa vibaraka wa nchi za Magharibi. Tunapigana Vita vya Ukraine bila kujijua