Kwanini Afrika tunashadadia Mapinduzi ya Kijeshi?

Bora watawale milele angalau wanaleta maendeleo na maendeleo yaonekanne.

Majeshi ambayo kwa miaka mingi yametuka na mafisadi kukandamiza haki za Raia sasa wamechoka na wamegundua wanatumika vibaya kutesa ndugu zao kwa fiada ya familia.
chache.

Ni kama wamezinduka. Huu moto wake hauzimiki
 
Hakuna mfumo wa uchaguzi wa kumuondoa mtawala na chama kongwe au kilichotawala kwa muda mref ndani ya bara la Africa!! Wameona hiyo ndio solutions cha kushangaza wananchi wanasapoti jeshi kuchukua Nchi........... Think bout it!!
Watawala wengi wa kiafrica wanatumia Demokrasia kama kiini macho cha kuwahadaa raia kwamba eti dola ibadilishwe kupitia sanduku la kura wakati ni hujuma tu zinafanyika ili chama tawala kiendelee kubakia madarakani kwa gharama zozote. Huu mtindo utaigharimu CCM siku si nyingi.

Tunahubiriana Amani ili wezi na mafisadi waendelee kuitawala nchi na kujineemesha wao na familia zao kilafi huku raia wakiteketea na umaskini. Hii sio sahihi kabisa.
 
Unashangaaa nini wizi wa mali za taifa angalia pesa ziko Kwa ajili ya family zao
 
Mtaandamana kuikataa CCM wao wakiwa wanawaangalia tu? 😂 My friende amka usingizini utajikojolea hata mtoto kumuachisha nyonyo sio jambo rahisi sababu maziwa ni matamu.

Hivyo tunatumiaga njia za kikatili kama kupaka aloe vera au pilipili ili tu ajifunze in the hard way kuwa imefikia wakati anatakiwa aache kunyonya.

Kabla hujafika barabarani unatakiwa upewe kibali na polisi ambapo kamanda lazma ataibuka kwenye vyombo vya habari na kukupiga mkwara wa hatari kwamba hicho unachotaka kukifanya hawatakivumilia na utajuta 🤣
 
Kuna kikundi cha raia wanadiriki kujiita "Wenye Nchi" katika ardhi ambayo inahubiri amani na demokrasia 🤣!!! Ni mambo ya kustaajabisha.

Damu ya mwenye haki haiendi bure, ipo siku yaja tutaondokana na hili jinamizi.
 
Sielewi ni Kwa nini Afrika inakuwa ni ngumu sana kuwaondoa viongozi "wabovu" wasiotakiwa Kwa njia ya kura, badala yake kazi hiyo hufanywa na wanajeshi.
Ukiona familia moja au ka chama kamoja kana ongoza nchi miaka nenda rudi bila kuachia madaraka ujue nyuma yake kuna support ya jeshi. Siku wanajeshi wanapo shindwa kuvumilia upuuzi licha ya kuhongwa sana na watawala ndio huamua kufanya yao. Mapinduziiii, daima.
 
1. Kwa sababu hakuna uchaguzi huru na wa haki.

2. Marais wengi ni wezi na wabinafsi pia ni vibaraka wa waarabu au wazungu.

3. Wapo tayari kutoa rasilimali za Nchi kwa kujipendekeza kwa mabwana zao
 
Nakubali ✔️
 
Tatizo ni nini kwa Afrika kutegemea majeshi kufanya mabadiliko ambayo kimsingi yanatakiwa yafanywe kupitia mifumo ya kiuchaguzi?
Hiyo mifumo ya kiuchaguzi imekaa kiujanjaujanja tu (tume isiyo huru huku mwenyekiti akiwa mteule wa mmoja wa wagombea), isitoshe hata mifumo yenyewe haiheshimiwi na wenye mamlaka, rafuu za kila aina (wakurugenzi kukataa kupokea fomu za wagombea, mawakala wa upande mmoja tu kuruhusu vituoni), rushwa na mengine mengi tu.

Hata hao majeshi nayo yakishapindua huwa vigumu kukabidhi madaraka kwa raia (mfano huko Sudan, Mali (kila siku wanasogesa uchaguzi mbele))...

Africa inahitaji mapinduzi ya kifikra zaidi, yatakayoleta namna bora zaidi ya kujitawala na kujiletea maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…