Kuna mambo kadhaa yanaiheshimisha wilaya Kinondoni kuliko wilaya ya Temeke
(1) MAENEO YA KISHUA
•Ukija na list ya maeneo ya ushuani mengi yako wilaya ya Kinondoni
(2)VIWANJA VYA KULA BATA NA BURUDANI
•Ukitaja maeneo ya starehe yenye hadhi kwa Dar mengi yako Kinondoni
(3)NYUMBA ZENYE HADHI
•Hapa nazungumzia mijengo ya kifahari na ya kisasa. Temeke imeachwa kwa mbali sana
(4)KINONDONI INA MATAJIRI WENGI NA WENYE KIPATO CHA KATI
•Nadhani hapa wanangu wa wilaya ya Temeke sijui kama mtabisha
(5)BEI YA VIWANJA KWA SQUARE METRE
•Wilaya Kinondoni bei za viwanja iko juu
(6)MAENEO YA KUFANYIA SHOPPING, OUTING, MIGAHAWA MIZURI, HOTELS, LOUNGES, PUBS, NIGHT CLUBS, MADUKA MAKUBWA YA NGUO
•Ukizungumzia mambo kama malls, supermarkets na mini-supermarkets, na vingine vinavyohusiana na hapo juu wilaya ya Kinondoni ni mbabe kwa wilaya ya Temeke
(7)CELEBRITIES WAKUBWA, WANASIASA WAKUBWA, WAKURUGENZI KWENYE MAKAMPUNI MAKUBWA NA MASHIRIKA YA UMMA NA NGO's, MAPROFESSOR
•In short watu wenye hadhi wengi na wakubwa na waheshimiwa serikalini wanaishi wilaya ya Kinondoni. Sijui kama hapo wanangu wa Temeke mna la kubishia
(8)NI RAHISI KUZIONA NDINGA NYINGI KALI ZA GHARAMA UKIWA WILAYA YA KINONDONI KULIKO UKIWA WILAYA YA TEMEKE
(9)SHULE NYINGI PRIVATE ZA KISHUA HAPA DAR ZIKO WILAYA YA KINONDONI (kindergarten, daycares, primary hadi seco)
•Hii inaonyesha waliosogezewa huduma hiyo ni watu wa aina gani
Wanangu wa wilaya ya Kinondoni kama mna jambo la kuongeza ongezeni hapo na wanetu wa wilaya ya Temeke karibuni kuzipangua hizo hoja japo juu mkiweza