Kiufupi naomba niseme huku serikali ilikusahau sana.ndio ikapelekea kuwa hivi tofauti na sehemu nyingine ,huku wamachinga wana dharau za hali ya juu mno kiasi cha kupanga mikokoteni ya machungwa tikiti barabaran au nguo barababan wakati gari zinapita ,refer hapo mbagala rangi tatu pita muda wowote utaona hiyo hali,kiugupi watu wengi akili yao ni ya leo yao tu kesho hawaijui, unauziwa kiwanja ujenge unaambiwa njia ipo ,mwisho wa siku mwenzako na yeye anauziwa jiran mnakosa pakupita,kuna jiran yetu hapa katangaza viwanja milion 6 ni mpare huu unakatika mwaka hata mtu kuja kuuliza hakuna.na huyu hatouza kamwe mana hakuna mipango miji kila mtu anajenga anavyotaka
Mtu anajenga hana raman fundi ndio anamchora chini kupata ramani,hiyo sehemu itaendelea lini? Ila kwa sasa huku mbagala na viunga vyake watu ninwengi mno na wanazaliana sio mchezo ni rahisi kukuta darasa moja lina wanafunzi 400 shule ya msingi,yan huku ni vituko mwanzao mwisho sijui viongozi wa huku wanafanya makusudi ,miaka nenda rudi shule zile zile watu wanaongezeka,kwa nini kuwe na thamani wakati viongozi wa huku ni vichwa maji.?