Kwanini ardhi ya Mbagala haina thamani?

Kwanini ardhi ya Mbagala haina thamani?

Ukanda huo wote kuanzia Temeke,mbagala na kuendelea huko chini vikindu,kisemvule mpaka huko mkuranga wamejaa waswahili hata Uuzaji wa viwanja ndo ule wa Futi (40ft×50ft) Viwanja vingi vya Mbagala havijapimwa ...wauzaji wanafanya makadirio tuu Unauziwa bila kujali uelekeo ndo maana unakutana na nyumba zimekaa hovyo hovyo

Haya yote yamewafanya watu wengi kuwa discouraged

Lakini ukanda huo ni mzuri sana kwa viwanja vya biashara (viwanja vinavyotazamana na barabara kuu)

Sent using Jamii Forums mobile app

Ulitaka ijae mizungu au miarabu?

Uswahili ni laana?

Wewe sio mswahili?

Goba, Mbweni hawapo waswahili?
 
Kuna eneo lipo nilipita juzi juzi... Aisee ni moto wa kuotea kwa mbaaali... Kuna mijengo km sio mbagala dadek.

Mbweni inasubiri
Unaona sasa? kumbe hujawahi tembea mbagala na ndio maana unashangaa sababu mmekaririshwa mbagala ni uswahilini, na sio wewe tu ni wote waliocomment humu. sijui mnatokea wapi aisee!
 
Sababu kubwa ni mzunguko mdogo wa pesa na usalama..... mpaka leo hii unapata sahani ya wali kwa 500.......

Mambo ya kuvunjiana milango ni vitu vya kawaida sana kule.......

Kule vijana wengi ni wakabaji pindi jua linapozama.......kule ukipata break down ni Bora ukimbie kuliko kubakia hapo........ umaskini umewafanya watu kule kuwa wanyama......
 
Watu wengi wa Mbagala wako uncivilized (sio wastaarabu).
Vibaka wengi, makelele kila kona, kuna hekaheka nyingi sana kiasi kwamba mtu usiyependa hekaheka huwezi kuishi Mbagala.

Binafsi hata wauze kiwanja laki 5 siwezi kukaa Mbagala, kuingia nyumbani kwako saa 3 usiku unaingia kwa wasiwasi maana wakabaji kibao maisha gani hayo sasa
 
Sababu kubwa ni mzunguko mdogo wa pesa na usalama....
Si kweli mzunguko wa pesa ni mkubwa sana 24hrs watu hawalali
mpaka leo hii unapata sahani ya wali kwa 500.......
Zunguka kote hupati sahani ya wali kwa 500
Mambo ya kuvunjiana milango ni vitu vya kawaida sana kule.......
Nimekaa mbagala miaka 10 sijawahi kusikia kesi ya kuvunjiana milango
Kule vijana wengi ni wakabaji pindi jua linapozama.......kule ukipata break down ni Bora ukimbie kuliko kubakia hapo........

umaskini umewafanya watu kule kuwa wanyama......
Nitajie unyama uliowahi kufanyika mbagala halafu ulinganishe unyama unaofanya kila kukicha mikoani kwenu musoma,mwanza na shinyanga
 
Lakini mbona elimu ya dini inatolewa kwa wingi Mbagala?
Nani kasema? Mbagala sio kwamba Ina waislam tu. Waislam ni wengi. Na ukikagua uislam wenyew ni risk factor. Hata huko goba na mbezi au arusha waislam Wana Hali mbaya zaidi kufananisha na wenzetu. Unadhani ni mipango ya mungu?
 
Kiufupi naomba niseme huku serikali ilikusahau sana.ndio ikapelekea kuwa hivi tofauti na sehemu nyingine ,huku wamachinga wana dharau za hali ya juu mno kiasi cha kupanga mikokoteni ya machungwa tikiti barabaran au nguo barababan wakati gari zinapita ,refer hapo mbagala rangi tatu pita muda wowote utaona hiyo hali,kiugupi watu wengi akili yao ni ya leo yao tu kesho hawaijui, unauziwa kiwanja ujenge unaambiwa njia ipo ,mwisho wa siku mwenzako na yeye anauziwa jiran mnakosa pakupita,kuna jiran yetu hapa katangaza viwanja milion 6 ni mpare huu unakatika mwaka hata mtu kuja kuuliza hakuna.na huyu hatouza kamwe mana hakuna mipango miji kila mtu anajenga anavyotaka

Mtu anajenga hana raman fundi ndio anamchora chini kupata ramani,hiyo sehemu itaendelea lini? Ila kwa sasa huku mbagala na viunga vyake watu ninwengi mno na wanazaliana sio mchezo ni rahisi kukuta darasa moja lina wanafunzi 400 shule ya msingi,yan huku ni vituko mwanzao mwisho sijui viongozi wa huku wanafanya makusudi ,miaka nenda rudi shule zile zile watu wanaongezeka,kwa nini kuwe na thamani wakati viongozi wa huku ni vichwa maji.?
 
Goba pa kishua Sana aisee ni eneo flani hv uzungu mwingi , hakuna uswahili kule hata chembe , alaf kila mtu na time zake yaan , mpak unakutana na mbezi beach full kipupwe, sasa huko sjui mbagala , yaan Temeke yote pa kisenge mno, sishawishi mtu kwenda kule , huko ndo HQ ya panya road, ndo sehemu yenye joto Kali DSM nzima
 
Yaani ukiangalia lifestyle yenu watu wa Mbagala sometimes unaweza kusema kama mnaigiza lakini ndo maisha yanaenda hivyo
 
Sababu kubwa ni mzunguko mdogo wa pesa na usalama..... mpaka leo hii unapata sahani ya wali kwa 500.......

Mambo ya kuvunjiana milango ni vitu vya kawaida sana kule.......

Kule vijana wengi ni wakabaji pindi jua linapozama.......kule ukipata break down ni Bora ukimbie kuliko kubakia hapo........ umaskini umewafanya watu kule kuwa wanyama......
Umeambiwa na Nani? Mm mbagala nipo kila siku na hayo mm siku Tani nayo mkuu
 
Goba pa kishua Sana aisee ni eneo flani hv uzungu mwingi , hakuna uswahili kule hata chembe , alaf kila mtu na time zake yaan , mpak unakutana na mbezi beach full kipupwe, sasa huko sjui mbagala , yaan Temeke yote pa kisenge mno, sishawishi mtu kwenda kule , huko ndo HQ ya panya road, ndo sehemu yenye joto Kali DSM nzima
Halafu iko hivi mtu ambaye amezaliwa na kukulia wilaya ya Kinondoni au ambaye ameishi wilaya ya Kinondoni kwa muda fulani ni ngumu sana kufikiria anunue eneo ajenge na kuishi wilaya ya Temeke
 
Back
Top Bottom