Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KWA NINI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE HAKUNYANYUA KALAMU KUANDIKA MAISHA YAKE?
Naikumbuka siku hii kama jana vile.
Niko nje ya mipaka ya Tanzania ni nyakati za usiku niko kwa rafiki yangu mmoja ambae ajabu sana yeye ananiambia kuwa aliona kitu katika maandishi yangu toka enzi nikiandika na Africa Events.
Kila tulipokutana alinisisitiza kuwa nipunguze kuandika katika magazeti na majarida na niwe mwandishi wa vitabu.
Wakati ule nilikuwa hili naliona jambo nisiloliweza kabisa.
Huyu rafiki yangu ni ‘’publisher,’’ yaani mchapaji vitabu tena mchapaji wa sifa.
Sasa siku hii tumekaa nyumbani kwake baada ya chakula cha jioni na tunazungumza kuhusu mswada wa kitabu changu cha maisha ya Abdul Sykes.
Rafiki yangu huyu alikuwa kausoma mswada wote akaniambia, ‘’Mohamed umemwandika sana Nyerere tena kwa undani na umakini mkubwa sijapatapo kusoma popote pale mwandishi ambae amemuandika Nyerere kwa kiasi hiki ulichofanya wewe.’’
Huyu rafiki yangu akaendelea, ’’Mimi niliomba miadi na Nyerere na akakubali kukutana na mimi Butiama.
Tulipoonana nikamwambia kuwa kuna mchapaji angependa kufanya mradi wa kuandika maisha yako.’’
Rafiki yangu akaniambia kuwa jibu la Nyerere lilikuwa, ‘’Mimi sizungumzi na mtu wa kati waambie hawa jamaa zako waje wanione mimi mwenyewe binafsi.’’
Rafiki yangu akanambia kuwa huo ndiyo ukawa mwisho wa mazungumzo yao akanyanyuka na kuondoka kuwahi ndege arudi Dar es Salaam.
Huyu rafiki yangu ndiye alikuwa mwakilishi wa hawa wachapaji katika kanda ya Afrika ya Mashariki na Kati na Mwalimu akiwafahamu vyema hawa wachapaji.
Rafiki akanambia hakuona kama kulikuwa na haja ya yeye kulisema hili kwani anasema Mwalimu hili akilijua fika.
Sahib yangu huyu alinifahamisha kuwa jibu lile alilitegemea kwa kuwa yeye kabla ya kuja kumuona Mwalimu alikuwa amefanya utafiti wake na taarifa alizopata zilikuwa Nyerere hataki maisha yake yaandikwe ingawa aliwaruhusu waandishi wawili kutoka Maryknoll, W. R. Duggan na J. R. kuandika maisha yake, ‘’Tanzania and Nyerere,’’ (1976).
Tukawa tunashughulisha fikra zetu kwa nini Mwalimu Nyerere hataki kuadikwa na kwa nini yeye mwenyewe hanyanyui kalamu yake kuandika maisha yake.
Huyu rafiki yangu akaniambia kuwa yeye angependa sana kuchapa kitabu changu lakini hataweza kwa sababu ya ‘’conflict of interest,’’ kwani yeye anafanya biashara na Serikali ya Tanzania na ana wasiwasi na yale maudhui ya kitabu changu.
Akaniambia kuwa kwa uzoefu wake hakuna mchapaji Tanzania atakaechapa kitabu changu.
Kauli hii ilinitia huzuni sana.
Nikamuuliza kwa nini wachapaji hawataki kukigusa kitabu changu?
Rafiki yangu akanijibu kwa ufupi sana, ‘’Wewe unaandika historia ya Julius Nyerere bila ya idhini yake.’’
Rafiki yangu akaniambia, ''Mohamed you have to learn the trade.''
Kwa hakika nilihangaika sana na kitabu changu kwa miaka mingi.
Miaka ile nilikuwa kijana mdogo nisiyejua siasa za Afrika zinavyochezwa na biashara ya vitabu inazunguka katika mzunguko na muhimili upi.
Lakini baadae kama mtu aliyegutushwa kutoka katika njozi likanijia wazo nijaribu kuwasilianana na wachapaji wa Uingereza.
Hakika kila kitu kinakwenda kama Allah alivyokipanga.
Kitabu kikachapwa London.
Baada ya kuchapwa kitabu hiki changu ndipo ikaonekana lazima kitabu cha Maisha ya Mwalimu Nyerere kiandikwe.
Hiki ni kisa kingine hapa si mahali pake kukieleza.
Lakini laiti Mwalimu mwenyewe angenyanyua kalamu kuandika maisha yake kwa hakika tungestarehe sana na kalamu yake.
Mimi hukaa peke yangu kimya nikajifanya mimi ndiye Julius Kambarage Nyerere na sasa naandika maisha yangu.
In Shaa Allah iko siku nitakuonyesheni nilichoandika.
Nimepata kumuonyesha maandishi haya yangu publisher mmoja.
Ajabu sana akaniambia hiki ni kitabu lakini ni riwaya ya aina yake akanihimiza nikamilishe kazi hii.
Akatanitania akaniambia, ''Mohamed umekuwa Irving Wallace?''
Huyu Irving Wallace ni mwandishi wa riwaya akiandika vitabu vyake kutokana na matukio ya kweli katika jamii.
Ukweli ni kuwa mimi sikumgeza Irving Wallace.
Mimi nimemuiga Shafi Adam Shafi jinsi alivyoandika kitabu chake maarufu, ''Haini.''
Lakini uweli utabakia kuwa laiti Mwalimu angeandika kumbukumbu zake tungepata kitabu ambacho si cha kawaida.
Historia ya Mwalimu Nyerere na TANU na uhuru wa Tanganyika ina ladha ya pekee sana waandishi wa kitabu chake hawakuweza kuionyesha ladha hii katika mseto waliopika.
Mseto wao chooko na mchele haukuwa sawia.
Sikuambii mchuzi wa papa wa kulia mseto.
Viungo havikukamilika.