Kwanini Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere hakunyanyua kalamu kuandika maisha yake?

Kwanini Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere hakunyanyua kalamu kuandika maisha yake?

Maelezo yako ni ngumi ya uzito wa heavyweight haswa ila hapo uliposema Mwalimu hakutaka kuweka na ilikuwa sahihi kutoweka mambo yote kwenye maandishi mezani ndipo umeharibu. Ni bora yote yangeweka katika historia huru na ya wazi tu, yasingetugawa bali yangemulika mwanga mkubwa katika historia yetu.
US historia ya utumwa, ubaguzi na vita vya wenyewe kwa wenyewe imewekwa wazi hadi kwenye shule za msingi na imesaidia kusahihisha na kuliimarisha sana taifa hilo.
Yoda,
Kuna mambo yakimhangaisha sana Mwalimu.
Moja ambalo likimpa shida ilikuwa uasisi wa TANU.

Taji la kuanzisha vuguvugu hadi kupelekea kuundwa kwa TANU nani avishwe?

Hii ndiyo sababu kubwa hata ilipoandikwa historia ya TANU na Chuo Cha CCM Kivukoni Abdul Sykes jina lake halipo.

Tukaishi miaka yote na historia ya TANU bila ya Abdul Sykes mwenye kadi ya TANU No. 3 na mdogo wake kadi No. 2.

Kadi No. 1 ya Territorial President Julius Kambarage Nyerere na aliandikiwa na Ally Sykes.
Ikawa historia hii haipo.
 
Yoda,
Mwalimu hakuwa nyota peke yake ukiwa unakusudia kuwa mtu aliyeweza kuongoza harakati za kudai uhuru.

Wewe umemfahamu Mwalimu kwa sifa hiyo kwa kuwa hapakutolewa nafasi ya kueleza historia ya kweli ya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Ikawa kama vile ni mwiko kwa mtu kueleza historia nyingine yeyote ila hii ya Nyerere ya kuwa ni yeye pekee hakuna mwingine.

Wala halikuwa suala la kuwazidi wote.

TAA ilikuwa na watu hodari sana mfano wa Dr. Wilbard Mwnjisi, Dr. Michael Lugazia, Dr. Vedasto Kyaruzi aliyekuwa President wa TAA hata kabla ya Nyerere 1950.

Nafasi ya rais wa TAA kisha kuundwa TANU nafasi hii Abdul Sykes alimkusudia Chief David Kidaha Makwaia wa Siha.

Kisa hiki nimekieleza mara nyingi sana hapa barzani.

Hamza Mwapachu yeye aliona Nyerere anafaa zaidi kwa nafasi hiyo kuliko Chief Kidaha na tangiapo Chief Kidaha hakuonyesha nia ya kuitaka nafasi ile.

Mwapachu alitoa sababu zake za kumtaka Nyerere ashike nafasi ile.

Ni kisa kirefu kina mambo mengi lakini ikutoshe kuwa hata uchaguzi ulipofanyika mwaka wa 1953 kutafuta rais wa TAA kati ya Abdul Sykes na Nyerere, Mwalimu alishinda kwa kura chache na hivyo ile ''inner circle,'' kamati ya ndani ya TAA ilikubaliana Nyerere lazima ashinde uchaguzi ule TANU iundwe mwaka unaofuatia 1954 na Nyerere aongoze mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika.
Tunakubaliana walikuwepo wengi saaana ...ila Nyerere aliwazidi akili,hekima,busara ,Elimu ...wao (baba zako)walimzidi mali pekee!
Kama ambavyo Waarabu na Fedha zao wanaburuzwa na wazungu!
 
Tunakubaliana walikuwepo wengi saaana ...ila Nyerere aliwazidi akili,hekima,busara ,Elimu ...wao (baba zako)walimzidi mali pekee!
Kama ambavyo Waarabu na Fedha zao wanaburuzwa na wazungu!
Makulanga,
Mimi siko hapa kufanya ubishani na wewe kwani ubishi hauna tija yoyote.
Kawaida yangu mimi hueleza kile ambacho nakijua.

Una khiyari ya kuamini au vinginevyo.

Uwezo wa Nyerere hakuna ambae anaweza kuukataa mara nyingi nimesema kuwa kama kuandika kitabu changu nia ingelikuwa ni kumdogosha Mwalimu kitabu kingekufa miaka mingi sana iliyopita kama kilivyokufa kitabu cha 'Historia ya TANU'' (1981) kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni.

Azma na nia yangu mimi kuandika kitabu cha historia ya TANU ilikuwa kueleza historia ya kweli ya harakati za kudai uhuru.

Hili nimefanikiwa kufanya.
Kitabu kipo sokoni huu mwaka wa 24 na matoleo yaliyochapwa ni manne ''...and counting...''
 
Back
Top Bottom