Mohamed,
Kugombana si lazima kutoleana kauli kali. Unachokiita 'ubaridi' ndio ugomvi wenyewe.
Abdul sykes kujiunga na AMNUT ni kiashirio cha ugomvi. Hivyo ugomvi ulikuwepo
Kwamba Ally Sykes aliktaa kumpa Mwalimu nyaraka za AA na TAA ni kitu kinachojibu aya ya tatu ya bandiko . Kama hakutaka nyaraka zitolewe alihodhi historia na kuipoteza mwenyewe, Buckingham palace wanamsemo '' If it's not documented, it didn't happen''.
Kuhusu Abdul kumpokea Mwalimu lina utata kutoka kwako. Bandiko lako la nyuma umeeleza Nyerere kutambulishwa na.... na kuna siku alilala Temeke.
Kwahiyo si Abdul aliyempokea wala Wazee, Nyerere alikuja Dar kama Mwalimu kutoka Scotland
Utata zaidi ni kwamba Nyerere alikuja mkutano wa chama mwaka 1948 kama katibu wa Tawi la Tabora. Kwa mantiki tayari alishakutana na viongozi wa chama akiwa kiongozi wa Tawi.
Kwamba alikutana na Abdul mwaka 1952! inawezakanaje akutanaye naye mara 2 na mara ya 2 iwe ya kwanza?
Kuhusu katiba kuandikwa au kunukuliwa hili nalo unalitia utata bila sababu.
Ikiwa kuna mtu aliwahi kuandika katiba au kunukuu kwanini huweki wazi?
Kuna msemo kutoka Sandrigham house kwamba '' the end justifies the means'' kwa maana nzuri tu, kwamba, Nyerere ndiye aliona uhitaji wa kitu katiba na kukiingiza katika mfumo wa chama.
Ikiwa kauli hii si kweli,tuonyeshe katiba ya AA au TAA iliyowahi kuwa ya chama.
Hata kama kuna sub committee , committee etc kama hawakuweka wazi, Nyerere anabaki mwandishi '' by default''
Nasisitiza ili kumuondoa Nyerere katika historia ya uandishi , unukuu au utakavyo, tuonyeshe katiba nyingine ya AA , TAA kabla ya Mwalimu, nani aliandika na iliwasilishwa wapi.
Bila hivyo hili halina mjadala '' the end justifies the means' Nyerere ni mwandishi 'by default'
Kusambaza chama. Rejea picha hapo juu na nyingine Nyerere akiwa Mafia.
Ipo video akiwa Lindi n.k.. Chama kilikuwepo, hoja ni kuwa aliyeamsha hamasa ni Nyerere.
Tunarudi kule kule, kama si Nyerere tuonyeshe kiongozi wa makao makuu AA au TAA aliyewahi kufanya ziara kama za Mwalimu na TANU kwa hamasa na uwazi kama Nyerere
Kuhusu EAMWS, hili sijui kwanini unaliongelea.
Nasema hivyo kwasababu ni aibu ''shame on ' wazee wako.
Unanikumbusha kisa cha jamaa aliyefanyiwa 'unyama' na wenzake. Asubuhi alieleza kila mtu
alichotendewa ili kupata sympathy bila kujua alikuwa anaanika '' dirty laundry'' hadharani.
Nyerere kama mtawala wa siasa na kama ilivyo kwa watawala wote ikiwemo viongozi wa dini hawapendi tishio katika kutawala. Kuundwa kwa EAMWS kulikuwa na sababu kuu mbili.
1. Hasira za kudai uhuru na kuachwa nyuma kielimu. Ilikuwa ni AMNUT 2.0
2. Waislam kuziba pengo la elimu lililoletwa na ukoloni.
Mfano, Mohamed Said mwandishi alianza kindergaten kanisani.
Elimu yake ya kati akasoma shule ya mission Dar es Salaam.
Huko Moshi hakukuwa na shule za Waislam, na ndivyo historia ilivyo
Wakati EAMWS inaundwa baraza la TANU lilikuwa na Wazee asilimia 98 Waislam(rejea picha ya Mohamed Said hapo juu). Baraza la TANU liliridhia kuvunjwa kwa EAMWS.
Nyerere alijua EAMWS ilikuwa na nguvu, na alitafuta chombo atakachokidhibiti, BAKWATA
Wazee wa baraza la TANU kwasababu ya kukosa maono, kukosa elimu na ufukara wa kipato wakaukubaliana na wazo hilo, hawakupinga, vinginevyo asilimia 98 ikiwa na 'support mikoani' kama Mohamed Said anavyoonyesha (rejea bandiko na majina ya Waislam hapo juu) Nyerere asingeweza kuvunja EAMWS
Waliokwenda kwa Sheikh Takdir ni Waislam. Waliounga mkono BAKWATA ni Waislam.
Nyerere single handedly asingeweza kuvunja EAMWS na kuwaweka akina Nasib.
Kumlaumu Nyerere ni makosa kwasababu alifanya akijua anafanya nini na alifanikiwa vizuri sana. Kumlaumu ni kuficha ukweli na udhaifu uliokuwepo na uliopo hadi sasa.
BAKWATA ni ile ile ya Nyerere .
Ukiangalia kwa undani factor ni mbili, elimu na ufukara wa kipato unaolazimisha watu kununuliwa kinyume na Imani yao. Haya si maneno mepesi na najua hayatakupendeza, bila kuyasema utakuwa unaidanganya jamii yako na utaendelea kuidanganya kwa kukwepa ukweli.
Narudia tena si maneno mepesi. Kule Windsor castle wanasema '' Call a spade a spade'
Swali unalotakiwa kulifanyia research ni hili, Nyerere aliwezaje' ku- overcome' asilimia 98 Waislam? Jibu lake litasaidia jamii kwa miaka mingi na si kuficha ukweli au kulalama.
Mwisho, kuhusu Nyerere kuingiwa na hofu napenda kukuhakikishia kuwa Nyerere ameshiriki mamb mengi sana ya Tanzania, Africa na Dunia.
Kitabu chako kisingemnyima usingizi.Kilichomsumbua ni upotoshaji akijua kwamba siku atakapokuwa hayupo upotoshaji utaangamiza Taifa.
Nyerere alijali sana Taifa lake kuliko yeye mwenyewe.
Kuandika kitabu kusingejibu hoja ya Tanganyika pekee, Mwalimu angezungumzia ukombozi wa Africa, ugomvi wake na Nkrumah, ushiriki wake wa siasa za kusini mwa Africa, mashariki ya kati , NAM na dunia kwa ujumla. Kuna mambo angeyaeleza yangeligawa Taifa, nitakupa mfano
Nyerere alivunja uhusiano na Israel kwa msingi ya kukiuka haki za binadamu na kuwakandimiza Palestina. Rais Magufuli alirudisha uhusiano huo bila hoja ya msingi.
Tulishuhudia Taifa lilivyogawanyika.
Wapo walioamini Nyerere alikuwa Sahihi kutoka pande zote za mzozo.
Wapo walioamini Magufuli yupo sahihi kutoka pande zote, lakini, suala la Magufuli lilichagizwa sana na hoja ya Udini. Mijadala ikaondoka katika 'core issue' ya uhusiano na Israel ikawa malumbano ya DINI. Hili ndilo Mwalimu alilikwepa, imagine angeweka yote mezani!
Kuweka yote mezani haina maana ya 'ubaya' lakini Wabaya wangeyatengenezea njia, kuyaandikia makala au vitabu kwa mitazamo yao na si uhalisia. Yanatokea sasa seuse angeyaandika.
Masalam
Ngongo JokaKuu Pascal Mayalla