Kwanini Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere hakunyanyua kalamu kuandika maisha yake?

Kwako mzee Mohamed Said naomba kujua:Kwanini uhusiano wa Nyerere na kina Sykes uliingia ubaridi?

Abdul Sykes alikuwa mwanachama maarufu wa TANU na mtu mwenye elimu kiasi kwanini hakupewa nafasi ya uongozi katika serikali mpya ya Tanganyika?
Ngome...
Msome Daisy Sykes anavyoeleza hali ilivyokuwa na jinsi ilivyobadilika:

''Baba akiwa Katibu na Kaimu Rais wa Tanganyika African Association (TAA) chama ambacho kiliasisiwa na babu yangu na wenzake mwaka wa 1929 baba yangu Abdulwahid Sykes ndiye alikuwa kinara wa mambo mengi ya chama hiki kuanzia mwaka wa 1950 mara tu baada ya kifo cha baba yeke mwaka wa 1949.

Pamoja na yeye walikuwa baba zangu wadogo Ally na Abbas Sykes, wakitayarisha mikutano, kuhamasisha watu waliokuwa katika majimbo (kama mikoa ilivyokuwa ikifahamika wakati ule) kujiunga na chama na kuwafanya wananchi washiriki katika siasa za nyakati zile.

Walishiriki kwa mfano, kupeleka malalamiko (petition) ya watu wa Meru UNO katika kesi maarufu iliyokuja kujulikana kama Meru Land Case ambayo Tanganyika ilipeleka ujumbe New York.

Walishiriki katika kudai uwakilishi wa Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria (LEGCO) kwa njia ya kidemokrasia, mtu mmoja kura moja na pia kutoa fedha kwa safari za viongozi wa TAA na pia kuwawezesha kujikimu wao na familia zao hasa katika safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere kwenda UNO mwaka wa 1955.

Uhuru ulipokuwa dhahiri sasa unapatikana na ulipopatikana ulikuja na changamoto nyingi ambazo naamini baba hakuzitegemea.

Haitakuwa sawasawa ikiwa sitaeleza upeo wa juu wa baba yangu katika wema, huruma na unyofu aliokuwanao.

Hata nilipokuwa mtoto nilipata kushuhudia na kuona chokochoko na chuki dhidi yake bila shaka kwa ajili ya hasad kwani baba kwa kiwango chochote kile alikuwa mtu aliyefanikiwa na kwenye ngazi nyingi wengi hawakuthubutu hata kuota kukanyaga, lakini sikumuona baba kukasirika wala kutaka kulipiza kisasi.

Katika unyofu wa hali ya juu aliendelea na maisha yake.''

Waasisi wa African Association: Cecil Matola President, Kleist Sykes Secretary, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamis, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi na Rawson Watts.
 
Kwa watu wanaomfahamu Nyerere ni nadra na tabu kupata kauli yake akisema '' mimi au Nime''. Nyerere hakupenda kutajwa kama yeye bali alitumia sana wingi '' Sisi, tuli.. n.k'

Akiwaaga Wazee wa Dar es Salaam pale Diamond kwa nadra nilimsikia akisema '' Nilikuwa Mkristo peke yangu''. Katika siku nadra sana hiyo ilikuwa moja akitumia neno ''Nili..''

Tatizo la kuandika kitabu chake ni kwa kutambua alishirikiana na watu wengine na ni ngumu sana kuandika 'Memoir' yake . Nyerere hakujifaragua wala kujikweza

Nyerere alifahamu kuandika 'Mmemoir' angegusa mambo mengi kama ugomvi wake na akina Abdul Sykes, Bibi Titi, Rais Karume, ujamaa, kutaifisha mali, Bakwata, Mali za Kanisa n.k. na pengine angeligawa Taifa zaidi kwa kitu kidogo cha kuepukika.

Nimesoma kitabu cha AH Mwinyi na BW Mkapa. Ukweli wamekwepa vitu vingi vya msingi.
Hiyo yote ililenga kutoleta mjadala wa kuligawa Taifa. Mkapa hakupenda alilazimika tu. Hivyo kuna sababu za kwanini hakutaka na kwanini alikubali baadaye

Nyerere alikubali baadaye kwasababu aliona bila sauti yake upotoshaji ulikithiri.

Hoja kwamba aliingizwa siasa na wazee wa Dar es Salaam haina msingi na ni ya kupuuzwa.

Nyerere kabla ya kufika Dar es Salaam alikuwa katika siasa.
Nyerere alikwenda masomoni Scotland ambako alikutana na wanasiasa wa dunia.

Kwa ujio wake Dar es Salaam mambo mengi yalibadilika.

Nyerere aliandika au '' kunukuu'' katiba iliyoitwa ya TANU. Hakuna aliwahi fanya hivyo kabla

Nyerere akasambaza chama kwa nguvu sana nchi nzima, hakuamini siasa za Mzizima pekee
Mwalimu akaungwa mkono na Watanganyika na kupata 'uhalali' wa kwenda UNO.

Uwezo wa Mwalimu unathibitika ndani ya baraza la wazee wa TANU(rejea picha ya Mohamed Said). Mwl aliwakuta na harakati, akafanya nao kazi asilimia 98 ikiwa ni Waislam.

Nyerere akawaongoza kufikia Uhuru wa nchi. Huyu anafundisha au anafundishwa?

Hii haina maana Mwalimu alikuja na harakati, la hasha, vyama vilikuwepo.

Kilichomsaidia Nyerere ni elimu na kuwa na ufahamu wa dunia na siasa za dunia.
Hiyo ndiyo siri ya kupokelewa kisha kuwaongoza! na si kuingizwa !

Ngongo Kiranga
Shukran sana Mkuu.
 
Proved,
Ilikuja kujulikana baadae kuwa Mwalimu alikuwa na hofu na historia ya kuamka kwa Tanganyika na kuundwa kwa African Association mwaka wa 1929.

Historia hii haikuwa ikifahamika na wengi kiasi ikawa kama vile historia ya AA haikuweko na hakukuwa na mtu aliyekuwa anaifahamu.

Historia hii ilikuwako pamoja na nyaraza zake kuthibitisha yale yaliyotendeka hadi kufikia kwanza mageuzi makubwa ya TAA 1950 na kuelekea kuundwa kwa TANU 1954.

Kuanzia mwaka wa 1961 uhuru ulipopatikana kulitokea changamoto nyingi kufikia pale ilipotakikana sasa Mwalimu iandikwe historia yake.

Hili lilimtia Mwalimu hofu.

Hiki ndio haswa ulichotamani iwe mwanzo na 'title' ya andiko lako.
 
Mzee Said utaandika mengi sana kwa lengo la kumdogosha Mwalimu na kujitahidi kuwakuza Watu unaowaamini wewe.

Kwa yeyote atakayesoma maandiko yako akitumia akili kidogo tu atajifunza ya kuwa bado Mwalimu alikuwa ana sifa za kuongoza hata kama angefikia kwa Jamii tofauti na aliyoikuta jijini Dar....kibatari gizani.

Ni wewe ndie unayeng'ang'ana kutaka kutaja Mtu mmoja mmoja na haswa ukiwa na malengo yako binafsi.

Cha ajabu ni kuwa Mwalimu kama Muhusika Mkuu yeye anasisitiza "Wazee wa Dare es Salaam"....Mzee Said hupendezwi kabisa na hili wewe umeng'ang'ana tu na kina Sykes and co.

Kwa maandiko yako na hulka unayojitahidi kuionesha na kuihubiri kwa bidii ni uthibitisho tosha kuwa Mwalimu alipitia wakati mgumu sana kwa baadhi ya waliokuwa wamemzunguka...huku yeye akiangalia maslahi ya wengi kulikuwa na wachache waliokuwa wanajiangalia wao.

Nimewahi kuhoji hili mara kadhaa na hujawahi kutoa jibu sahihi...kwamba hivi kabla ya Mwalimu kufika Dar ni sehemu kiasi gani ya nchi walikuwa wanafahamu harakati za TAA au kina Sykes?. na je si Mwalimu ndiye aliyeiamsha nchi kujua nini kinaendelea kuhusu harakati za uhuru?.

Mwalimu alitumia maneno "nilikuta chama kimesinzia"...ni dhahiri kuwa "Wazee wako" walikuwa hawajui cha kufanya zaidi baada ya kuanzisha chama, heshima yao itabaki hapo wala hakuna mwenye shida na hilo.

Ni sisi na wewe tujiulize ni kwa nini Wazee wa Dar es Salaama walimuamini Mwalimu ndani ya muda mfupi?...huoni kwamba kuna uwezekano wapo ambao walikuwa karibu naye na hawakufurahia hili? lakini siku zote sauti ya wengi ni sauti ya Mungu...Wachache wasingeweza kuwashinda wengi.

Wazee wa Dar Es Salaam hawakujali Mwalimu ni nani bali walichojali ni kuwa huyu ndiye Mtu tunayemuhitaji...najua hutosema kama kina Sykes walimuonea wivu...ofcoz hata yeye asingekwambia.

Kuna mahali Mwalimu anasema alilazimika kufanya kazi na Wazee hata zile ambazo ni kinyume na imani yake, mfano kwenda makaburini n.k....kumbuka huku kote 'Wazee wako' labda hawakuwepo....kwa kifupi mambo yalikuwa mengi kuliko hata ambavyo wewe ulivyojikita kwenye kuwakuza Watu wako wachache tu.
 
Imani yake ya Kikuria au ya Kizanaki, mbona mizimu kwao huko nje nje tu?
 
Nguruvi3,
Mwalimu Nyerere hakupata kugombana na akina Sykes kwa maana ya ugomvi kama ule aliogombana na Sheikh Suleiman Takadir na Bi. Titi Mohamed ugomvi wa kutoleana maneno kwa hamaki.

Kilichotokea baina ya Nyerere na akina Sykes ni paliingia ''ubaridi'' baina yao na yale mapenzi na udugu uliokuwa baina yao taratibu ukaondoka na kupotea.

Pamoja na kupotea kwa mapenzi haya na historia ya akina Sykes katika kupigania uhuru wa Tanganyika ikafutika.

Inawezekana pia hali hii ya ''ubaridi'' ilizidishwa na Ally Sykes kumkatalia Mwalimu kumpa Nyaraka za TAA na TANU ambazo aliziomba kwake baada ya kifo cha Abdul Sykes.

Ally Sykes alidai kuwa hizo ingawa ni nyaraka za TANU lakini ni nyaraka zao na wasingeweza kuzitoa na kuzikabidhi kwa mtu yeyote yule.

Ingawa unasema kuwa Mwalimu alichelea kuandika kumbukumbu zake kwa kuogopa ''kuligawa'' taifa, tayari alikuwa keshaligawa kwa kuzuia Waislam wasiendelee na juhudi za kujikwamua katika elimu kupitia EAMWS.

Nyerere akaivunja EAMWS ili Chuo Kikuu Cha Waislam kisijengwe na kumfukuza Sheikh Hassan bin Ameir Tanganyika.

Haya yote ambayo Nyerere hakutaka yafahamike kwa kuhofia mgawanyiko leo hii yanafahamika.

Yote yamo ktika kitabu cha Abdul Sykes.

Hili la katiba wewe unalieleza unavyojua na mimi nimelieleza kwa ushahidi wa Nyaraka za Sykes kuwa Earle Seaton kama mshaurii wa TAA Political Subcommitee alishauri kuwa itumike katiba ya CPP.

Hii ni 1950 na Nyerere alikuwa bado hajafika Dar es Salaam.

Huyu Seaton ndiye aliyemwambia Abdul kuwa njia bora ya kupambana na Waingereza ni kwa wao kufungua mazungumzo na UNO.

Yapo mengi katika kipindi hiki ambayo kwa kuwa Nyerere hakuwako huenda hakuyajua au aliyajua akaamua asiyaseme.

Mfano wa jina lake kuwa kiongozi wa TAA alilolipendekeza alikuwa Hamza Mwapachu.

Abdul Sykes yeye alikuwa keshaanza mazungumzo na Chief David Kidaha Makwaia aingie TAA wamchague rais kisha waunde TANU na Chief Kidaha aongoze harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Hili la ''wazee'' hata mimi nakuunga mkono ingawa yeye mwenyewe Nyerere anasema alipokewa na wazee.

Nyerere hakupokewa na mzee yeyote alipokewa na Abdul Sykes.

Bahati mbaya sana yeye mwenyewe hakupata kulisema hili na lililokuwa jepesi ulimini kwake kulitamka ni hili la wazee ambao hata majina yao hakuyataja.

Kuwa Nyerere alisambaza chama inataka maelezo kwani TANU iliundwa kutokana na TAA katika majimbo na waasisi hao wa TANU huko majimboni walikuwa hata sura ya Nyerere hawaijui ikoje.

Mifano iko mingi tu katika historia ya wazalendo kama Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Msham Awadh, Abdallah Rashid Sembe wengi wengi waliounda TANU mikoani na Nyerere akafika huko kakikuta chama na wanachama wengi.

Hiyo picha hapo chini ilipigwa Iringa 1956 na ndiyo kwa mara ya kwanza Nyerere anafika huko na hao waliokuja kumpokea ni wanachama wa TANU wakiongozwa na Abbas Max na wengi wao walikuwa hawajapata kumuona.

Abbas Max alimshawishi Abdul Sykes akiwa mgeni wake hapo Iringa kuwa akirejea Dar es Salaam amshawishi Nyerere kuja Iringa.

View attachment 2164596
Mohamed,
Kugombana si lazima kutoleana kauli kali. Unachokiita 'ubaridi' ndio ugomvi wenyewe.
Abdul sykes kujiunga na AMNUT ni kiashirio cha ugomvi. Hivyo ugomvi ulikuwepo

Kwamba Ally Sykes aliktaa kumpa Mwalimu nyaraka za AA na TAA ni kitu kinachojibu aya ya tatu ya bandiko . Kama hakutaka nyaraka zitolewe alihodhi historia na kuipoteza mwenyewe, Buckingham palace wanamsemo '' If it's not documented, it didn't happen''.

Kuhusu Abdul kumpokea Mwalimu lina utata kutoka kwako. Bandiko lako la nyuma umeeleza Nyerere kutambulishwa na.... na kuna siku alilala Temeke.
Kwahiyo si Abdul aliyempokea wala Wazee, Nyerere alikuja Dar kama Mwalimu kutoka Scotland

Utata zaidi ni kwamba Nyerere alikuja mkutano wa chama mwaka 1948 kama katibu wa Tawi la Tabora. Kwa mantiki tayari alishakutana na viongozi wa chama akiwa kiongozi wa Tawi.
Kwamba alikutana na Abdul mwaka 1952! inawezakanaje akutanaye naye mara 2 na mara ya 2 iwe ya kwanza?

Kuhusu katiba kuandikwa au kunukuliwa hili nalo unalitia utata bila sababu.

Ikiwa kuna mtu aliwahi kuandika katiba au kunukuu kwanini huweki wazi?

Kuna msemo kutoka Sandrigham house kwamba '' the end justifies the means'' kwa maana nzuri tu, kwamba, Nyerere ndiye aliona uhitaji wa kitu katiba na kukiingiza katika mfumo wa chama.

Ikiwa kauli hii si kweli,tuonyeshe katiba ya AA au TAA iliyowahi kuwa ya chama.
Hata kama kuna sub committee , committee etc kama hawakuweka wazi, Nyerere anabaki mwandishi '' by default''

Nasisitiza ili kumuondoa Nyerere katika historia ya uandishi , unukuu au utakavyo, tuonyeshe katiba nyingine ya AA , TAA kabla ya Mwalimu, nani aliandika na iliwasilishwa wapi.

Bila hivyo hili halina mjadala '' the end justifies the means' Nyerere ni mwandishi 'by default'

Kusambaza chama. Rejea picha hapo juu na nyingine Nyerere akiwa Mafia.
Ipo video akiwa Lindi n.k.. Chama kilikuwepo, hoja ni kuwa aliyeamsha hamasa ni Nyerere.

Tunarudi kule kule, kama si Nyerere tuonyeshe kiongozi wa makao makuu AA au TAA aliyewahi kufanya ziara kama za Mwalimu na TANU kwa hamasa na uwazi kama Nyerere

Kuhusu EAMWS, hili sijui kwanini unaliongelea.

Nasema hivyo kwasababu ni aibu ''shame on ' wazee wako.

Unanikumbusha kisa cha jamaa aliyefanyiwa 'unyama' na wenzake. Asubuhi alieleza kila mtu
alichotendewa ili kupata sympathy bila kujua alikuwa anaanika '' dirty laundry'' hadharani.

Nyerere kama mtawala wa siasa na kama ilivyo kwa watawala wote ikiwemo viongozi wa dini hawapendi tishio katika kutawala. Kuundwa kwa EAMWS kulikuwa na sababu kuu mbili.
1. Hasira za kudai uhuru na kuachwa nyuma kielimu. Ilikuwa ni AMNUT 2.0

2. Waislam kuziba pengo la elimu lililoletwa na ukoloni.
Mfano, Mohamed Said mwandishi alianza kindergaten kanisani.
Elimu yake ya kati akasoma shule ya mission Dar es Salaam.
Huko Moshi hakukuwa na shule za Waislam, na ndivyo historia ilivyo

Wakati EAMWS inaundwa baraza la TANU lilikuwa na Wazee asilimia 98 Waislam(rejea picha ya Mohamed Said hapo juu). Baraza la TANU liliridhia kuvunjwa kwa EAMWS.

Nyerere alijua EAMWS ilikuwa na nguvu, na alitafuta chombo atakachokidhibiti, BAKWATA

Wazee wa baraza la TANU kwasababu ya kukosa maono, kukosa elimu na ufukara wa kipato wakaukubaliana na wazo hilo, hawakupinga, vinginevyo asilimia 98 ikiwa na 'support mikoani' kama Mohamed Said anavyoonyesha (rejea bandiko na majina ya Waislam hapo juu) Nyerere asingeweza kuvunja EAMWS

Waliokwenda kwa Sheikh Takdir ni Waislam. Waliounga mkono BAKWATA ni Waislam.
Nyerere single handedly asingeweza kuvunja EAMWS na kuwaweka akina Nasib.

Kumlaumu Nyerere ni makosa kwasababu alifanya akijua anafanya nini na alifanikiwa vizuri sana. Kumlaumu ni kuficha ukweli na udhaifu uliokuwepo na uliopo hadi sasa.

BAKWATA ni ile ile ya Nyerere .

Ukiangalia kwa undani factor ni mbili, elimu na ufukara wa kipato unaolazimisha watu kununuliwa kinyume na Imani yao. Haya si maneno mepesi na najua hayatakupendeza, bila kuyasema utakuwa unaidanganya jamii yako na utaendelea kuidanganya kwa kukwepa ukweli.

Narudia tena si maneno mepesi. Kule Windsor castle wanasema '' Call a spade a spade'

Swali unalotakiwa kulifanyia research ni hili, Nyerere aliwezaje' ku- overcome' asilimia 98 Waislam? Jibu lake litasaidia jamii kwa miaka mingi na si kuficha ukweli au kulalama.

Mwisho, kuhusu Nyerere kuingiwa na hofu napenda kukuhakikishia kuwa Nyerere ameshiriki mamb mengi sana ya Tanzania, Africa na Dunia.

Kitabu chako kisingemnyima usingizi.Kilichomsumbua ni upotoshaji akijua kwamba siku atakapokuwa hayupo upotoshaji utaangamiza Taifa.
Nyerere alijali sana Taifa lake kuliko yeye mwenyewe.

Kuandika kitabu kusingejibu hoja ya Tanganyika pekee, Mwalimu angezungumzia ukombozi wa Africa, ugomvi wake na Nkrumah, ushiriki wake wa siasa za kusini mwa Africa, mashariki ya kati , NAM na dunia kwa ujumla. Kuna mambo angeyaeleza yangeligawa Taifa, nitakupa mfano

Nyerere alivunja uhusiano na Israel kwa msingi ya kukiuka haki za binadamu na kuwakandimiza Palestina. Rais Magufuli alirudisha uhusiano huo bila hoja ya msingi.

Tulishuhudia Taifa lilivyogawanyika.
Wapo walioamini Nyerere alikuwa Sahihi kutoka pande zote za mzozo.
Wapo walioamini Magufuli yupo sahihi kutoka pande zote, lakini, suala la Magufuli lilichagizwa sana na hoja ya Udini. Mijadala ikaondoka katika 'core issue' ya uhusiano na Israel ikawa malumbano ya DINI. Hili ndilo Mwalimu alilikwepa, imagine angeweka yote mezani!

Kuweka yote mezani haina maana ya 'ubaya' lakini Wabaya wangeyatengenezea njia, kuyaandikia makala au vitabu kwa mitazamo yao na si uhalisia. Yanatokea sasa seuse angeyaandika.

Masalam

Ngongo JokaKuu Pascal Mayalla

Nguruvi...
Abdul Sykes hakupata kuwa na chama chochote kingine isipokuwa TANU.

Abdul Sykes hakujiunga na AMNUT yawezekana wewe unamchanganya na Abdulwahid Abdulkarim aliyekuwa Katibu wa AMNUT.

Kuwa ugomvi ulikuwako kwa kuwa Abdul alijiunga na AMNUT sababu hii haipo labda uje na nyigine.

Mnaipenda historia ya Abdul Sykes na Nyerere lakini hamuijui na hamtaki kuisoma zaidi mnakimbilia kuja kufanya ''bashing.''

Kleist Sykes, mtoto wa Abdul Sykes alipata kuulizwa na mwandishi wa Raia Mwema kama anafikiria kutoka CCM.

Kleist alijibu kuwa yeye hawezi kutoka CCM kwa kuwa CCM imetokana na TANU na TANU imeasisiwa na baba yake.

(Ally Sykes kadi yake ya TANU No. 2, Abdul Sykes kadi yake ya TANU No. 3, Julius Nyerere kadi yake ya TANU No. 1)

Kuhusu Ally Sykes kukataa kukabidhi nyaraka za TAA na TANU kwa Nyerere kunatokana na kukataliwa kwa nyaraka hizi kutumika katika mradi wa kuandika historia ya TANU mradi ambao waandishi walikuwa Abdul Sykes na Dr. Wilbard Klerruu.

Abdul Sykes akajitoa katika uandishi wa kitabu hiki.
Kisa hiki nimekieleza hapa barzani kinafahamika.

Vipi nyaraka zitakataliwe zisiwe kielelezo cha historia ya kuasisiwa kwa AA na TANU kisha nyaraka hizo hizo zitakiwe tena?

Hili suala la katiba nimelieleza na ikiwa wewe unasema kuwa Nyerere aliandika katiba ya TANU hakuna shida.

Watu mmeaminishwa mengi hadi mlipokuja kusoma kitabu cha Abdul Sykes ndiyo sasa mnajitokeza kuniuliza maswali nami najibu kadri ya ufahamu wangu.

Mlikuwa wapi miaka yote hamkuhoji historia rasmi ya Chuo Cha CCM Kivukoni?
Kwa nini ile mliiamini?

Prof. Haroub Othman alikwenda kumuuliza Mwalimu maswali kuhusu Abdul Sykes na kuasisiwa kwa TANU baada ya kusoma maisha yake kutoka kwangu.

Alikuwa wapi miaka yote?

Hakutosheka na mazugumzo ya Nyerere alikwenda kwa Ahmed Rashaad Ali kuuliza maswali zaidi.

Ahmed Rashaad alikuwa rafiki kipenzi wa Abdul Sykes kuanzia 1936 hadi Abdul alipofarikia 1968.

Nasimama hapa hayo ya BAKWATA nayakalia kimya hayana maana tena kwani hakuna asiyeyajua.

1648321376851.png

Kushoto Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashaad Ali na Sheikh Ahmed Islam Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere safari ya Umra 1997
 
Mzee Said utaandika mengi sana kwa lengo la kumdogosha Mwalimu na kujitahidi kuwakuza Watu unaowaamini wewe.

Kwa yeyote atakayesoma maandiko yako akitumia akili kidogo tu atajifunza ya kuwa bado Mwalimu alikuwa ana sifa za kuongoza hata kama angefikia kwa Jamii tofauti na aliyoikuta jijini Dar....kibatari gizani.

Ni wewe ndie unayeng'ang'ana kutaka kutaja Mtu mmoja mmoja na haswa ukiwa na malengo yako binafsi.

Cha ajabu ni kuwa Mwalimu kama Muhusika Mkuu yeye anasisitiza "Wazee wa Dare es Salaam"....Mzee Said hupendezwi kabisa na hili wewe umeng'ang'ana tu na kina Sykes and co.

Kwa maandiko yako na hulka unayojitahidi kuionesha na kuihubiri kwa bidii ni uthibitisho tosha kuwa Mwalimu alipitia wakati mgumu sana kwa baadhi ya waliokuwa wamemzunguka...huku yeye akiangalia maslahi ya wengi kulikuwa na wachache waliokuwa wanajiangalia wao.

Nimewahi kuhoji hili mara kadhaa na hujawahi kutoa jibu sahihi...kwamba hivi kabla ya Mwalimu kufika Dar ni sehemu kiasi gani ya nchi walikuwa wanafahamu harakati za TAA au kina Sykes?. na je si Mwalimu ndiye aliyeiamsha nchi kujua nini kinaendelea kuhusu harakati za uhuru?.

Mwalimu alitumia maneno "nilikuta chama kimesinzia"...ni dhahiri kuwa "Wazee wako" walikuwa hawajui cha kufanya zaidi baada ya kuanzisha chama, heshima yao itabaki hapo wala hakuna mwenye shida na hilo.

Ni sisi na wewe tujiulize ni kwa nini Wazee wa Dar es Salaama walimuamini Mwalimu ndani ya muda mfupi?...huoni kwamba kuna uwezekano wapo ambao walikuwa karibu naye na hawakufurahia hili? lakini siku zote sauti ya wengi ni sauti ya Mungu...Wachache wasingeweza kuwashinda wengi.

Wazee wa Dar Es Salaam hawakujali Mwalimu ni nani bali walichojali ni kuwa huyu ndiye Mtu tunayemuhitaji...najua hutosema kama kina Sykes walimuonea wivu...ofcoz hata yeye asingekwambia.

Kuna mahali Mwalimu anasema alilazimika kufanya kazi na Wazee hata zile ambazo ni kinyume na imani yake, mfano kwenda makaburini n.k....kumbuka huku kote 'Wazee wako' labda hawakuwepo....kwa kifupi mambo yalikuwa mengi kuliko hata ambavyo wewe ulivyojikita kwenye kuwakuza Watu wako wachache tu.
Mzee Said utaandika mengi sana kwa lengo la kumdogosha Mwalimu na kujitahidi kuwakuza Watu unaowaamini wewe.

Kwa yeyote atakayesoma maandiko yako akitumia akili kidogo tu atajifunza ya kuwa bado Mwalimu alikuwa ana sifa za kuongoza hata kama angefikia kwa Jamii tofauti na aliyoikuta jijini Dar....kibatari gizani.

Ni wewe ndie unayeng'ang'ana kutaka kutaja Mtu mmoja mmoja na haswa ukiwa na malengo yako binafsi.

Cha ajabu ni kuwa Mwalimu kama Muhusika Mkuu yeye anasisitiza "Wazee wa Dare es Salaam"....Mzee Said hupendezwi kabisa na hili wewe umeng'ang'ana tu na kina Sykes and co.

Kwa maandiko yako na hulka unayojitahidi kuionesha na kuihubiri kwa bidii ni uthibitisho tosha kuwa Mwalimu alipitia wakati mgumu sana kwa baadhi ya waliokuwa wamemzunguka...huku yeye akiangalia maslahi ya wengi kulikuwa na wachache waliokuwa wanajiangalia wao.

Nimewahi kuhoji hili mara kadhaa na hujawahi kutoa jibu sahihi...kwamba hivi kabla ya Mwalimu kufika Dar ni sehemu kiasi gani ya nchi walikuwa wanafahamu harakati za TAA au kina Sykes?. na je si Mwalimu ndiye aliyeiamsha nchi kujua nini kinaendelea kuhusu harakati za uhuru?.

Mwalimu alitumia maneno "nilikuta chama kimesinzia"...ni dhahiri kuwa "Wazee wako" walikuwa hawajui cha kufanya zaidi baada ya kuanzisha chama, heshima yao itabaki hapo wala hakuna mwenye shida na hilo.

Ni sisi na wewe tujiulize ni kwa nini Wazee wa Dar es Salaama walimuamini Mwalimu ndani ya muda mfupi?...huoni kwamba kuna uwezekano wapo ambao walikuwa karibu naye na hawakufurahia hili? lakini siku zote sauti ya wengi ni sauti ya Mungu...Wachache wasingeweza kuwashinda wengi.

Wazee wa Dar Es Salaam hawakujali Mwalimu ni nani bali walichojali ni kuwa huyu ndiye Mtu tunayemuhitaji...najua hutosema kama kina Sykes walimuonea wivu...ofcoz hata yeye asingekwambia.

Kuna mahali Mwalimu anasema alilazimika kufanya kazi na Wazee hata zile ambazo ni kinyume na imani yake, mfano kwenda makaburini n.k....kumbuka huku kote 'Wazee wako' labda hawakuwepo....kwa kifupi mambo yalikuwa mengi kuliko hata ambavyo wewe ulivyojikita kwenye kuwakuza Watu wako wachache tu.
May...
Ningeandika kitabu cha Abdul Sykes kwa nia ya kumdogosha Mwalimu kitabu changu kingekuwa kimekufa miaka mingi nyuma.

Hakuna popote katika kitabu hiki nimedogosha Nyerere.
Ikiwa umeona kuna sentensi ya dharau kwa Mwalimu iweke hapa watu waisome.

Hili la sifa ya uwezo wa Mwalimu kuongoza ilijadiliwa nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio Abdul Sykes alipokwenda na Ali Mwinyi Tambwe kupata kauli ya mwisho ya Mwapachu kuwa Nyerere atiwe katika uongozi wa juu wa TAA katika mkutano wa TAA wa 1953 na mwaka unaofuatia TANU iundwe.

Ukiwa hulijui hili ni bahati mbaya sana kwako kwani nimelieleza hapa mara nyingi tu.
Hili la chama ''kusinzia,'' alilosema Mwalimu kwa kweli naona haya kueleza zaidi.

Ile hotuba ya Diamond Jubilee Mwalimu kakosea au tuseme kuna mengi kasahau.

TAA kuanzia 1950 ilikuwa inafanya makubwa sana kuanzia kuunda TAA Political Subcommittee na kuandika mapendekezo ya katika kwa serikali hadi kusaidia safari ya Japhet Kirilo UNO 1952 na mengine mengi kama Abdul kukutana na Jomo Kenyatta katika mkutano wa siri Nairobi 1950 na safari ya Ally Sykes na Denis Phombeah kwenda Northern Rhodesia (Zambia) kuhudhuria mkutano wa wapigania uhuru wa Afrika chini ya Ikweta ulioitishwa na Kenneth Kaunda.

Sikulaumu kwa kutoyajua haya kwani historia hii haipo katika historia rasmi ya Chuo Cha CCM Kivukoni (1981).

Mwalimu katika hotuba ile anasema safari yake ya kwanza baada ya kuundwa kwa TANU ilikuwa Mbeya.

Mwalimu kasahau safari yake ya kwanza kuwa ilikuwa Morogoro na aliongozana na Zuberi Mtemvu na taarifa ya mkutano huu iliyoandikwa na Mtemvu ipo katika Nyaraka za Sykes.

Hapakuwa na wazee katika harakati hizi kama unavyonukuu kutoka kwa Mwalimu.

Ushahidi ni huo hapo juu.

Safari ya Abdul Sykes Nairobi 1950 kuonana na Kenyatta na Peter Mbiu Koinange na wazalendo wengine.

Tuchukulie kuwa Nyerere hakuwa anayajua haya na sasa mimi nimeyaeleza katika kitabu cha Abdul Sykes yanajulikana.

Tutosheke na ukweli huu.
Mimi sijamkuza wala kumdogosha yeyote katika utafiti wangu.

Nimejitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kueleza kama nilivyoyakuta katika utafiti.

Najua utashtuka sana nikikukwambia kuwa TAA ilikaribia kufa baada ya Nyerere kuchukua uongozi.

Hapa ndipo Abdul Sykes akafanya mazungumzo na wazee kukirejesha chama mahali kilipokuwa kabla.

1648326456404.png

Picha hiyo hapo juu ni Ally Sykes na Denis Phombeah viongozi wa TAA wakiwa uwanja wa ndege wa Chileka, Blantyre, Nyasaland (Malawi) baada ya kukamatwa na kufukuzwa Salisbury, Southern Rhodesia wakiwa njiani kwenda mkutanoni Lusaka, Northern Rhodesia (Zambia).
 
Nguruvi...
Abdul Sykes hakupata kuwa na chama chochote kingine isipokuwa TANU.
Abdul Sykes hakujiunga na AMNUT yawezekana wewe unamchanganya na Abdulwahid Abdulkarim aliyekuwa Katibu wa AMNUT.
Kuwa ugomvi ulikuwako kwa kuwa Abdul alijiunga na AMNUT sababu hii haipo labda uje na nyigine.
Mnaipenda historia ya Abdul Sykes na Nyerere lakini hamuijui na hamtaki kuisoma zaidi mnakimbilia kuja kufanya ''bashing.''

Kleist Sykes, mtoto wa Abdul Sykes alipata kuulizwa na mwandishi wa Raia Mwema kama anafikiria kutoka CCM.

Kleist alijibu kuwa yeye hawezi kutoka CCM kwa kuwa CCM imetokana na TANU na TANU imeasisiwa na baba yake.

(Ally Sykes kadi yake ya TANU No. 2, Abdul Sykes kadi yake ya TANU No. 3, Julius Nyerere kadi yake ya TANU No. 1)

Kuhusu Ally Sykes kukataa kukabidhi nyaraka za TAA na TANU kwa Nyerere kunatokana na kukataliwa kwa nyaraka hizi kutumika katika mradi wa kuandika historia ya TANU mradi ambao waandishi walikuwa Abdul Sykes na Dr. Wilbard Klerruu.

Abdul Sykes akajitoa katika uandishi wa kitabu hiki.
Kisa hiki nimekieleza hapa barzani kinafahamika.

Vipi nyaraka zitakataliwe zisiwe kielelezo cha historia ya kuasisiwa kwa AA na TANU kisha nyaraka hizo hizo zitakiwe tena?

Hili suala la katiba nimelieleza na ikiwa wewe unasema kuwa Nyerere aliandika katiba ya TANU hakuna shida.

Watu mmeaminishwa mengi hadi mlipokuja kusoma kitabu cha Abdul Sykes ndiyo sasa mnajitokeza kuniuliza maswali nami najibu kadri ya ufahamu wangu.

Mlikuwa wapi miaka yote hamkuhoji historia rasmi ya Chuo Cha CCM Kivukoni?
Kwa nini ile mliiamini?

Prof. Haroub Othman alikwenda kumuuliza Mwalimu maswali kuhusu Abdul Sykes na kuasisiwa kwa TANU baada ya kusoma maisha yake kutoka kwangu.

Alikuwa wapi miaka yote?

Hakutosheka na mazugumzo ya Nyerere alikwenda kwa Ahmed Rashaad Ali kuuliza maswali zaidi.

Ahmed Rashaad alikuwa rafiki kipenzi wa Abdul Sykes kuanzia 1936 hadi Abdul alipofarikia 1968.

Nasimama hapa hayo ya BAKWATA nayakalia kimya hayana maana tena kwani hakuna asiyeyajua.

Kushoto Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashaad Ali na Sheikh Ahmed Islam Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere safari ya Umra 1997
Mohamed
Najua unaghabika sana hoja zako zikichambuliwa.
Kazi ya utafiti haiishi katika 'publication' ni pamoja na kutetea hoja zitaokanazo.

Tofauti na wewe, mimi napitia hoja moja baada ya nyingine, mwenzangu kwa ghadhabu unaingiza hata yasiyokuwepo. Mfano, Kleist anahusiana vipi na hoja? A. Rashad yanahusiana vipi na hoja?

Nikirejea katika hoja, suala la katiba halina utata ikiwa una 'vithibitisho'.

Umepitia shajara la Kleist Sykes na nyaraka za Abdul Sykes ungetueleza katiba ya AA au TAA ilikuwepo, ilipitishwa lini na nani na ilitumika wapi.

Kutueleza kuhusu sub committee etc ni irrelevant, hazijibu hoja iliyopo mezani, Katiba.

Kwa sisi wengine kwa kusoma maandiko mbali mbali ikiwemo yako tunafikia hatma ya kwamba katiba ya kwanza ya chama cha siasa iliandikwa na Nyerere.

Ikiwa iliandika ilinukuliwa iliazimwa hilo ni jambo jingine the muhimu , Nyerere ndiye ali introduce katiba ya chama, na hili ni 'by default' .

Kuhusu Ally Sykes na nyaraka, kama alizihifadhi na kuna wachache wanaoruhusiwa kuziona ni hiari yake. Kumbuka kuwa ''If it's not documented, it did not happen''

BAKWATA linajulikana na hadi leo ni tatizo. Tatizo si wanaotaka BAKWATA , tatizo ni wanaosaidia uwepo wa BAKWATA na hapa ni Waislam. Hakuna BAKWATA bila Waislam.

Ukweli mchungu usiotaka kuusikia ni kama ule wa EAMWS.
Kwamba, tatizo ni 'wasomi' wanaotafuta hoja za kufunika uchafu na si kufagia uchafu.

Mfano, tatizo la BAKWATA linasemwa ni la BAKWATA na si Waislam.

Ukiiuliza Bakwata inahusiana na watu gani utajibiwa ni Bakwata.

Hakuna anayesema ni Waislam nbali Bakwata. Hivi hawa Bakwata si Wiaslam? Kuna dini inayoitwa Bakwata? Nani anayethibitisha muislam na mtu baki?

Muhimu kwako kama mwandishi ni kueleza ukweli si kusambaza hisia.
Ukweli utatoa majibu ya matatizo, kuficha tatizo hakusaidii kuondoa tatizo.

Ni wakati ukabiliane na ukweli, uueleze ukweli ili mwisho wa kulalama uje na matokeo chanya. Kwa miaka unamweleza Abdul Sykes na Wazee wako lakini je inatosha ? Kuna matokeo gani tofauti? Hadithi ni zile zile, zinaisaidia jamii yako kwa namna gani?

Majuzi umeandika kuhusu Postal codes na majina ya mitaa kuwatambua Wazee wako.
Tunarudi pale pale, jiji hili lilikuwa chini ya Mameya na Madiwani Waislam Wazee wako.
Vipi kuna mtaa wa Makamba? Uliidhinishwa na nani kama si Mameya na madiwani ambao ni ''Wazee au watoto wao''? Kwanini si Mshume Kiyate? Jiulize maswali na chanzo na si kukimbilia kuamsha hisia! Waulize wazee wako waliopo, kilitokea nini akina Mayor Sykes wakashindwa kuwaenzi wazee wao! Hawa ulikuwa nao karibu, je, uliwahi kuwauliza au kuwaeleza?

Kwanini huelezi sababu za kifo cha EAMWS kama ukosefu wa elimu na umasikini wa kipato!
Vinginevyo katika watu 100 iweje watu 2 au 3 wawashinde watu 98 au 97? Hivi huoni tatizo hapo?
Baraza la TANU lina wajumbe 98% halafu wanashindwa na Nyerere! real, hapa huoni tatizo

Mwisho, ninakusihi pamoja na uandishi wako mzuri zingatia kuwa ''precise and concise'' ukijikita kujibu hoja husika
 
KWA NINI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE HAKUNYANYUA KALAMU KUANDIKA MAISHA YAKE?

Naikumbuka siku hii kama jana vile.

Niko nje ya mipaka ya Tanzania ni nyakati za usiku niko kwa rafiki yangu mmoja ambae ajabu sana yeye ananiambia kuwa aliona kitu katika maandishi yangu toka enzi nikiandika na Africa Events.

Kila tulipokutana alinisisitiza kuwa nipunguze kuandika katika magazeti na majarida na niwe mwandishi wa vitabu.

Wakati ule nilikuwa hili naliona jambo nisiloliweza kabisa.
Huyu rafiki yangu ni ‘’publisher,’’ yaani mchapaji vitabu tena mchapaji wa sifa.

Sasa siku hii tumekaa nyumbani kwake baada ya chakula cha jioni na tunazungumza kuhusu mswada wa kitabu changu cha maisha ya Abdul Sykes.

Rafiki yangu huyu alikuwa kausoma mswada wote akaniambia, ‘’Mohamed umemwandika sana Nyerere tena kwa undani na umakini mkubwa sijapatapo kusoma popote pale mwandishi ambae amemuandika Nyerere kwa kiasi hiki ulichofanya wewe.’’

Huyu rafiki yangu akaendelea, ’’Mimi niliomba miadi na Nyerere na akakubali kukutana na mimi Butiama.

Tulipoonana nikamwambia kuwa kuna mchapaji angependa kufanya mradi wa kuandika maisha yako.’’

Rafiki yangu akaniambia kuwa jibu la Nyerere lilikuwa, ‘’Mimi sizungumzi na mtu wa kati waambie hawa jamaa zako waje wanione mimi mwenyewe binafsi.’’

Rafiki yangu akanambia kuwa huo ndiyo ukawa mwisho wa mazungumzo yao akanyanyuka na kuondoka kuwahi ndege arudi Dar es Salaam.

Huyu rafiki yangu ndiye alikuwa mwakilishi wa hawa wachapaji katika kanda ya Afrika ya Mashariki na Kati na Mwalimu akiwafahamu vyema hawa wachapaji.

Rafiki akanambia hakuona kama kulikuwa na haja ya yeye kulisema hili kwani anasema Mwalimu hili akilijua fika.

Sahib yangu huyu alinifahamisha kuwa jibu lile alilitegemea kwa kuwa yeye kabla ya kuja kumuona Mwalimu alikuwa amefanya utafiti wake na taarifa alizopata zilikuwa Nyerere hataki maisha yake yaandikwe ingawa aliwaruhusu waandishi wawili kutoka Maryknoll, W. R. Duggan na J. R. kuandika maisha yake, ‘’Tanzania and Nyerere,’’ (1976).

Tukawa tunashughulisha fikra zetu kwa nini Mwalimu Nyerere hataki kuadikwa na kwa nini yeye mwenyewe hanyanyui kalamu yake kuandika maisha yake.

Huyu rafiki yangu akaniambia kuwa yeye angependa sana kuchapa kitabu changu lakini hataweza kwa sababu ya ‘’conflict of interest,’’ kwani yeye anafanya biashara na Serikali ya Tanzania na ana wasiwasi na yale maudhui ya kitabu changu.

Akaniambia kuwa kwa uzoefu wake hakuna mchapaji Tanzania atakaechapa kitabu changu.
Kauli hii ilinitia huzuni sana.

Nikamuuliza kwa nini wachapaji hawataki kukigusa kitabu changu?

Rafiki yangu akanijibu kwa ufupi sana, ‘’Wewe unaandika historia ya Julius Nyerere bila ya idhini yake.’’

Rafiki yangu akaniambia, ''Mohamed you have to learn the trade.''
Kwa hakika nilihangaika sana na kitabu changu kwa miaka mingi.

Miaka ile nilikuwa kijana mdogo nisiyejua siasa za Afrika zinavyochezwa na biashara ya vitabu inazunguka katika mzunguko na muhimili upi.

Lakini baadae kama mtu aliyegutushwa kutoka katika njozi likanijia wazo nijaribu kuwasilianana na wachapaji wa Uingereza.

Hakika kila kitu kinakwenda kama Allah alivyokipanga.
Kitabu kikachapwa London.

Baada ya kuchapwa kitabu hiki changu ndipo ikaonekana lazima kitabu cha Maisha ya Mwalimu Nyerere kiandikwe.

Hiki ni kisa kingine hapa si mahali pake kukieleza.

Lakini laiti Mwalimu mwenyewe angenyanyua kalamu kuandika maisha yake kwa hakika tungestarehe sana na kalamu yake.

Mimi hukaa peke yangu kimya nikajifanya mimi ndiye Julius Kambarage Nyerere na sasa naandika maisha yangu.

In Shaa Allah iko siku nitakuonyesheni nilichoandika.
Nimepata kumuonyesha maandishi haya yangu publisher mmoja.

Ajabu sana akaniambia hiki ni kitabu lakini ni riwaya ya aina yake akanihimiza nikamilishe kazi hii.

Akatanitania akaniambia, ''Mohamed umekuwa Irving Wallace?''

Huyu Irving Wallace ni mwandishi wa riwaya akiandika vitabu vyake kutokana na matukio ya kweli katika jamii.

Ukweli ni kuwa mimi sikumgeza Irving Wallace.
Mimi nimemuiga Shafi Adam Shafi jinsi alivyoandika kitabu chake maarufu, ''Haini.''

Lakini uweli utabakia kuwa laiti Mwalimu angeandika kumbukumbu zake tungepata kitabu ambacho si cha kawaida.

Historia ya Mwalimu Nyerere na TANU na uhuru wa Tanganyika ina ladha ya pekee sana waandishi wa kitabu chake hawakuweza kuionyesha ladha hii katika mseto waliopika.

Mseto wao chooko na mchele haukuwa sawia.
Sikuambii mchuzi wa papa wa kulia mseto.

Viungo havikukamilika.

View attachment 2153570
Mudi,
Shikamoo.

Mtoa mada nadhani kuna mambo umeficha kwenye bandiko lako hili ili kuvutia kwenye yale unayotaka uma ufahamu. Umetumia mwanya wa mwalimu kutoandika ili kuprove nadharia zako.

Hakika mtego huu kuna wadau mbalimbali watautegua.

Mimi nipo nasoma comments.
 
Mohamed
Najua unaghabika sana hoja zako zikichambuliwa.
Kazi ya utafiti haiishi katika 'publication' ni pamoja na kutetea hoja zitaokanazo.

Tofauti na wewe, mimi napitia hoja moja baada ya nyingine, mwenzangu kwa ghadhabu unaingiza hata yasiyokuwepo. Mfano, Kleist anahusiana vipi na hoja? A. Rashad yanahusiana vipi na hoja?

Nikirejea katika hoja, suala la katiba halina utata ikiwa una 'vithibitisho'.

Umepitia shajara la Kleist Sykes na nyaraka za Abdul Sykes ungetueleza katiba ya AA au TAA ilikuwepo, ilipitishwa lini na nani na ilitumika wapi.

Kutueleza kuhusu sub committee etc ni irrelevant, hazijibu hoja iliyopo mezani, Katiba.

Kwa sisi wengine kwa kusoma maandiko mbali mbali ikiwemo yako tunafikia hatma ya kwamba katiba ya kwanza ya chama cha siasa iliandikwa na Nyerere.

Ikiwa iliandika ilinukuliwa iliazimwa hilo ni jambo jingine the muhimu , Nyerere ndiye ali introduce katiba ya chama, na hili ni 'by default' .

Kuhusu Ally Sykes na nyaraka, kama alizihifadhi na kuna wachache wanaoruhusiwa kuziona ni hiari yake. Kumbuka kuwa ''If it's not documented, it did not happen''

BAKWATA linajulikana na hadi leo ni tatizo. Tatizo si wanaotaka BAKWATA , tatizo ni wanaosaidia uwepo wa BAKWATA na hapa ni Waislam. Hakuna BAKWATA bila Waislam.

Ukweli mchungu usiotaka kuusikia ni kama ule wa EAMWS.
Kwamba, tatizo ni 'wasomi' wanaotafuta hoja za kufunika uchafu na si kufagia uchafu.

Mfano, tatizo la BAKWATA linasemwa ni la BAKWATA na si Waislam.

Ukiiuliza Bakwata inahusiana na watu gani utajibiwa ni Bakwata.

Hakuna anayesema ni Waislam nbali Bakwata. Hivi hawa Bakwata si Wiaslam? Kuna dini inayoitwa Bakwata? Nani anayethibitisha muislam na mtu baki?

Muhimu kwako kama mwandishi ni kueleza ukweli si kusambaza hisia.
Ukweli utatoa majibu ya matatizo, kuficha tatizo hakusaidii kuondoa tatizo.

Ni wakati ukabiliane na ukweli, uueleze ukweli ili mwisho wa kulalama uje na matokeo chanya. Kwa miaka unamweleza Abdul Sykes na Wazee wako lakini je inatosha ? Kuna matokeo gani tofauti? Hadithi ni zile zile, zinaisaidia jamii yako kwa namna gani?

Majuzi umeandika kuhusu Postal codes na majina ya mitaa kuwatambua Wazee wako.
Tunarudi pale pale, jiji hili lilikuwa chini ya Mameya na Madiwani Waislam Wazee wako.
Vipi kuna mtaa wa Makamba? Uliidhinishwa na nani kama si Mameya na madiwani ambao ni ''Wazee au watoto wao''? Kwanini si Mshume Kiyate? Jiulize maswali na chanzo na si kukimbilia kuamsha hisia! Waulize wazee wako waliopo, kilitokea nini akina Mayor Sykes wakashindwa kuwaenzi wazee wao! Hawa ulikuwa nao karibu, je, uliwahi kuwauliza au kuwaeleza?

Kwanini huelezi sababu za kifo cha EAMWS kama ukosefu wa elimu na umasikini wa kipato!
Vinginevyo katika watu 100 iweje watu 2 au 3 wawashinde watu 98 au 97? Hivi huoni tatizo hapo?
Baraza la TANU lina wajumbe 98% halafu wanashindwa na Nyerere! real, hapa huoni tatizo

Mwisho, ninakusihi pamoja na uandishi wako mzuri zingatia kuwa ''precise and concise'' ukijikita kujibu hoja husika
Nguruvi,
Ningekuwa naghadhibika ghadhabu zangu ungeziona katika majibu yangu kwa lugha kali na ufedhuli.

Mimi sina tatizo na yale unayopenda kuamini hiyo ni khiyari yako.

Ahmed Rashaad anahusika sana katika historia hii kwa kuwa alikuwapo toka siku ya kwanza historia hii inaanza 1950 Abdul alipochukua uongozi wa TAA.

Ahmed Rashaad anahusika sana kwani hawa wote ninaowaeleza hapa yeye anawajua vyema.

Ilikuwa Abdul ndiye aliyemjulisha Ahmed Rashaad kwa Jomo Kenyatta.

Ulikuwa unayajua haya?

Unajua mchango wa Rashaad katika historia ya uhuru wa Afrika?

Rejea nyuma katika makala zangu yupo.

Ama kutaka mimi nijibu maswali upendavyo wewe hili haliwezekani.

Wewe ukiuliza mimi In Shaa Allah nitakujibu na itakubidi ustahamili majibu yangu.

Sina Cha kutetea.
Natetea nini?

Kuwa historia hii haikuwapo na ni mimi ndiyo mtafiti wa kwanza kuiandika?
 
Mudi,
Shikamoo.

Mtoa mada nadhani kuna mambo umeficha kwenye bandiko lako hili ili kuvutia kwenye yale unayotaka uma ufahamu. Umetumia mwanya wa mwalimu kutoandika ili kuprove nadharia zako.

Hakika mtego huu kuna wadau mbalimbali watautegua.

Mimi nipo nasoma comments.
Marahaba Mhandisi,
Sijaficha kitu.

Walioficha historia hii sasa wanafahamika.

Ingependeza kwa sasa wewe shutuma hizo uzielekeze kwao badala ya kuninyooshea mimi kidole.
 
Nguruvi,
Ningekuwa naghadhibika ghadhabu zangu ungeziona katika majibu yangu kwa lugha Kali na ufedhuli.

Mimi sina tatizo na yale unayopenda kuamini hiyo ni khiyari yako.

Ahmed Rashaad anahusika sana katika historia hii kwa kuwa alikuwapo toka siku ya kwanza historia hii inaanza 1950 Abdul alipochukua uongozi wa TAA.

Ahmed Rashaad anahusika sana kwani hawa wote ninaowaeleza hapa yeye anawajua vyema.

Ilikuwa Abdul ndiye aliyemjulisha Ahmed Rashaad kwa Jomo Kenyatta.

Ulikuwa unayajua haya?

Unajua mchango wa Rashaad katika historia ya uhuru wa Afrika?

Rejea nyuma katika makala zangu yupo.

Ama kutaka mimi nijibu maswali upendavyo wewe hili haliwezekani.

Wewe ukiuliza mimi In Shaa Allah nitakujibu na itakubidi ustahamili majibu yangu.

Sina Cha kutetea.
Natetea nini?

Kuwa historia hii haikuwapo na ni mimi ndiyo mtafiti wa kwanza kuiandika?
Kwanza, mimi natoa hoja na kila unapoona swali kuna maana yake, fikirishi!
Mfano, kwa kudai Nyerere hakuandika katiba,iko wapi ya AA au TAA? Nani aliandika, ilikubaliwa wapi na lini ilianza kutumika. Kila swali hapo ni hoja lakini si swali ni fikirishi hasa kwa wasomaji siyo wasomewaji.

Pili, hoja ya Postal code. Hivi si Kleist alikuwa Mayor? Ilikuwaje hakutoa majina ya mitaa?
Kitwana Kondo, Abuu Juma , Adam Kimbisa, Ramadhan Nyamka, Chambuso, Mfaume hao wote ni ''Wazee wako'' leo unaongelea majina ya mitaa! Kwamba, tulipata uhuru tukifika leo.
Unaweza kuona ni swali lakini si swali kama unavyoliona. Haya mambo ni mapana !

Tatu sina sababu za wewe kujibu nitakavyo, lakini kuna principles tusizoweza kuziepuka.
Kuwa precise and concise ni moja kati ya hizo. ku address hoja ni nyingine
Najua unapopata tabu, hadhra uliyozoea ni tofauti kidogo

Huwezi kuingiza usichoulizwa ukaeleweka kwa watu wanaosoma maandishi kwa weledi
Unarudia rudia habari pasipo na ulazima. Hakubali hoja za wengine hata kama unajua ukweli wake

MS uliwahi kusema kitabu chako kitumike kufundisha Historia mashuleni! au nilisikia vibaya?
 
Sina zaidi ya kukueleza kuhusu katiba labda nikuwekee hapa niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes kuhusu katiba:

''Baada ya kuunda kamati hii, Abdulwahid alianza kuyaandikia matawi ya TAA ili kuyahuisha.

Jambo kubwa lililomkabili Abdulwahid na ile kamati ya siasa ilikuwa ni hadhi ya Tanganyika kama nchi ya udhamini chini ya Umoja wa Mataifa.

Abdulwahid alimuingiza katika kamati ya siasa Earle Seaton, mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akikaa Moshi ili aishauri kamati kuhusu mambo ya sheria na katiba.''

(Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951, Sykes' Papers).

Unaniuliza katiba ya AA iliyoundwa 1929 na unataka nikuonyeshe.

Kwa nini huwaulizi CCM katiba ya TANU na mswada wa kitabu cha Abdul Sykes na Dr. Wilbard Kleruu uko wapi?

Nadhani swali hili ni aula zaidi na ikiwa watatuonyesha huenda tukasoma mengi hasa yale ambayo Abdul aliyaleta katika historia ya TANU.

Majina ya mitaa Mzee Kondo alishalimaliza lakini watekelezaji hawakubadili jina la Tandamti kuwa Kiyate Mshume hadi leo zaidi ya miaka 30 imepita.

Mimi sipati tabu katika kuandika na kusoma.
Niamini katika hili.

Nadhani unajua kuwa nimechukua kikombe hapa JF kwa ajili ya uandishi wangu.

Nashukuru kuwa umejijibu mwenyewe kuwa nilisema kitabu changu kitumike kufundisha historia.

Ni hivi.

Oxford University Press, (OUP) Nairobi walinitia katika mradi wa kuandika vitabu vya kufundisha Kiingereza shule za msingi lakini wakati huo huo wanafunzi wasome historia za nchi zao.

Hadi wakati wanafanya mawasiliano na mimi OUP ilikuwa imeshachapa vitabu 14 kutoka Kenya na Uganda bahati mbaya hawakupokea mswada hata mmoja kutoka Tanzania.

Hapo ndipo walipowasiliana na mimi kuniomba wanijumuishe katika huo mradi na niandike kitabu.

Kitabu changu ''The Torch on Kilimanjaro,'' kimechapwa na kilizinduliwa hapa Dar es Salaam, Kilimanjaro Kempisky Hotel mwaka wa 2007.

Viongozi wote wakuu wa Wizara ya Elimu walikuwapo.
Kitabu hiki hakikupitishwa katika mtaala.

OUP wamenieleza kuwa hili limewashangaza iliwavunja nguvu kiasi walisimamisha kuchapa mswada ambao niliwapelekea.

Kitabu hiki kinasomeshwa Kenya na Uganda na kwengineko na kinakwenda sasa toleo la tatu.

1648354290436.png

1648354071626.png
 
Itakuwa labda alikuwa busy mno na majukumu..all in all asante mzee wetu kwa kutupa historia bila kuchoka achana na wanaosema wewe NI mdini...binafsi Mimi NI mkristo ila sijawahi kuona huo udini unaosemwa kuwa unaleta.kudos!
Ndege John wewe unaweza kuwa Si mdini ...ila bila shaka Mzee Mohamed ni mdini!
 
Nguruvi...
Sina zaidi ya kukueleza kuhusu katiba labda nikuwekee hapa niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes kuhusu katiba:''Baada ya kuunda kamati hii, Abdulwahid alianza kuyaandikia matawi ya TAA ili kuyahuisha.
Jambo kubwa lililomkabili Abdulwahid na ile kamati ya siasa ilikuwa ni hadhi ya Tanganyika kama nchi ya udhamini chini ya Umoja wa Mataifa.Abdulwahid alimuingiza katika kamati ya siasa Earle Seaton, mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akikaa Moshi ili aishauri kamati kuhusu mambo ya sheria na katiba.''
Hadithi inaishia hapo, hakuna katiba iliyoandikwa au kunukuliwa au kuchukuliwa popote.
Nyerere ndiye aliyefanya yote hayo na chama kuwa na katiba, aliandika
Hata kama hukubali lakini ukweli unabaki pale pale. Si rahisi lakini ndio ukweli
(Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951, Sykes' Papers).
Hiyo ni report si katiba. Kuna tofauti ya report na consitution , in fact ni vitu viwili tofauti
Unaniuliza katiba ya AA iliyoundwa 1929 na unataka nikuonyeshe.
Kwa nini huwaulizi CCM katiba ya TANU na mswada wa kitabu cha Abdul Sykes na Dr. Wilbard Kleruu uko wapi?
Usingejibu ingalikuwa bora!
Nauliza katiba ya AA ya Kleist Sykes iko wapi? Katiba si kitabu ni vitu viwili tofauti
Nadhani swali hili ni aula zaidi na ikiwa watatuonyesha huenda tukasoma mengi hasa yale ambayo Abdul aliyaleta katika historia ya TANU.
Si wewe umesoma nyaraka zao na baba yake! kinakushinda kipi?
Majina ya mitaa Mzee Kondo alishalimaliza lakini watekelezaji hawakubadili jina la Tandamti kuwa Kiyate Mshume hadi leo zaidi ya miaka 30 imepita.
Mameya : Amri Abeid, R. Nyamka, A. Kimbisa, Abuu Juma, Kleist Sykes , K.Kondo
Hawa wote walifanya nini kuhusu majina ya mitaa ya wazee wako?
Utekelezaji ni kisingizio tu, KK alikuwa na influence kubwa hilo lisingekuwa tatizo
Kwani hukusoma kitabu cha BW Mkapa kwamba Nyerere alimweleza akamuone nani!
Oxford University Press, (OUP) Nairobi walinitia katika mradi wa kuandika vitabu vya kufundisha Kiingereza shule za msingi lakini wakati huo huo wanafunzi wasome historia za nchi zao.

Hadi wakati wanafanya mawasiliano na mimi OUP ilikuwa imeshachapa vitabu 14 kutoka Kenya na Uganda bahati mbaya hawakupokea mswada hata mmoja kutoka Tanzania.

Hapo ndipo walipowasiliana na mimi kuniomba wanijumuishe katika huo mradi na niandike kitabu.

Kitabu changu ''The Torch on Kilimanjaro,'' kimechapwa na kilizinduliwa hapa Dar es Salaam, Kilimanjaro Kempisky Hotel mwaka wa 2007.

Viongozi wote wakuu wa Wizara ya Elimu walikuwapo.
Kitabu hiki hakikupitishwa katika mtaala.

OUP wamenieleza kuwa hili limewashangaza iliwavunja nguvu kiasi walisimamisha kuchapa mswada ambao niliwapelekea.

Kitabu hiki kinasomeshwa Kenya na Uganda na kwengineko na kinakwenda sasa toleo la tatu.
Ningeshangaa kuviona katika mitaala ya elimu ya watoto wetu
 
Hadithi inaishia hapo, hakuna katiba iliyoandikwa au kunukuliwa au kuchukuliwa popote.
Nyerere ndiye aliyefanya yote hayo na chama kuwa na katiba, aliandika
Hata kama hukubali lakini ukweli unabaki pale pale. Si rahisi lakini ndio ukweli

Hiyo ni report si katiba. Kuna tofauti ya report na consitution , in fact ni vitu viwili tofauti

Usingejibu ingalikuwa bora!
Nauliza katiba ya AA ya Kleist Sykes iko wapi? Katiba si kitabu ni vitu viwili tofauti

Si wewe umesoma nyaraka zao na baba yake! kinakushinda kipi?

Mameya : Amri Abeid, R. Nyamka, A. Kimbisa, Abuu Juma, Kleist Sykes , K.Kondo
Hawa wote walifanya nini kuhusu majina ya mitaa ya wazee wako?
Utekelezaji ni kisingizio tu, KK alikuwa na influence kubwa hilo lisingekuwa tatizo
Kwani hukusoma kitabu cha BW Mkapa kwamba Nyerere alimweleza akamuone nani!

Ningeshangaa kuviona katika mitaala ya elimu ya watoto wetu
Nguruvi...
Hakuna tatizo mimi nimeandika niliyoyaona una haki ya kukubali au kukataa.

Muhimu kwangu ni kuwa nilikuja na elimu mpya katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere mwenyewe na wasomaji wamekipenda kitabu hiki.

Baada ya mradi wa Oxford University Press, Nairobi, Oxford University Press New York na Harvard wakanitia katika mradi wa Dictionary of African Biography na nikaandika mchango wa Kleist Sykes katika historia ya Tanganyika.

Baada ya hapo ndiyo nikaalikwa Northwestern University, Chicago kuzungumza.

Baada ya hapo nikashirikishwa katika uandishi wa Nyerere Biography.

Wewe unaandika umejificha uso.
Mimi naandika hadharani.

Hii ndiyo tofauti kubwa kati yetu.
Huwajibiki kuamini vitabu vyangu.

Back
Top Bottom