Kwa watu wanaomfahamu Nyerere ni nadra na tabu kupata kauli yake akisema '' mimi au Nime''. Nyerere hakupenda kutajwa kama yeye bali alitumia sana wingi '' Sisi, tuli.. n.k'
Akiwaaga Wazee wa Dar es Salaam pale Diamond kwa nadra nilimsikia akisema '' Nilikuwa Mkristo peke yangu''. Katika siku nadra sana hiyo ilikuwa moja akitumia neno ''Nili..''
Tatizo la kuandika kitabu chake ni kwa kutambua alishirikiana na watu wengine na ni ngumu sana kuandika 'Memoir' yake . Nyerere hakujifaragua wala kujikweza
Nyerere alifahamu kuandika 'Mmemoir' angegusa mambo mengi kama ugomvi wake na akina Abdul Sykes, Bibi Titi, Rais Karume, ujamaa, kutaifisha mali, Bakwata, Mali za Kanisa n.k. na pengine angeligawa Taifa zaidi kwa kitu kidogo cha kuepukika.
Nimesoma kitabu cha AH Mwinyi na BW Mkapa. Ukweli wamekwepa vitu vingi vya msingi.
Hiyo yote ililenga kutoleta mjadala wa kuligawa Taifa. Mkapa hakupenda alilazimika tu. Hivyo kuna sababu za kwanini hakutaka na kwanini alikubali baadaye
Nyerere alikubali baadaye kwasababu aliona bila sauti yake upotoshaji ulikithiri.
Hoja kwamba aliingizwa siasa na wazee wa Dar es Salaam haina msingi na ni ya kupuuzwa.
Nyerere kabla ya kufika Dar es Salaam alikuwa katika siasa.
Nyerere alikwenda masomoni Scotland ambako alikutana na wanasiasa wa dunia.
Kwa ujio wake Dar es Salaam mambo mengi yalibadilika.
Nyerere aliandika au '' kunukuu'' katiba iliyoitwa ya TANU. Hakuna aliwahi fanya hivyo kabla
Nyerere akasambaza chama kwa nguvu sana nchi nzima, hakuamini siasa za Mzizima pekee
Mwalimu akaungwa mkono na Watanganyika na kupata 'uhalali' wa kwenda UNO.
Uwezo wa Mwalimu unathibitika ndani ya baraza la wazee wa TANU(rejea picha ya Mohamed Said). Mwl aliwakuta na harakati, akafanya nao kazi asilimia 98 ikiwa ni Waislam.
Nyerere akawaongoza kufikia Uhuru wa nchi. Huyu anafundisha au anafundishwa?
Hii haina maana Mwalimu alikuja na harakati, la hasha, vyama vilikuwepo.
Kilichomsaidia Nyerere ni elimu na kuwa na ufahamu wa dunia na siasa za dunia.
Hiyo ndiyo siri ya kupokelewa kisha kuwaongoza! na si kuingizwa !
Ngongo Kiranga
Hilo alishajibiwa mwengine...
Dudu kaandika hayo hapo chini na mimi nimeona nifungue uzi mpya niweke maelezo katika hayo maneno yake ili kusahihisha makosa ya historia ya TANU ambayo yamekuwa yakijirudia sasa nusu karne:
MAKOSA YANAYOJIRUDIA KATIKA HISTORIA YA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE NA TANU
Dudus said:
''... watu wa pwani walikuwa na advantage ya Kiswahili kwa wakati huo kiliwabeba sana. Ningeletwa mimi mhadzabe na Kiswahili wapi na wapi! Inasemekana hata Nyerere wakati anafanya urafiki na wazee wa Kariakoo hadi wakamkabidhi TANU, Kiswahili kilikuwa kinampa shida to some extent; ila kimalkia ungedhani anaishi kwenye corridor za Buckingham.''
Jibu langu kwake hili hapo chini:
Dudus,
Mwalimu Nyerere hakupokelewa Dar es Salaam na mzee yeyote alipofika mwaka wa 1952.
Hii ni katika moja ya makosa yaliyomo katika historia ya TANU.
Nyerere mtu aliyekuwa anajuananae kwa karibu sana alipofika Dar es Salaam ni Joseph Kasella Bantu.
Kasella Bantu akiishi Temeke.
Ilikuwa wakati mwingine Mwalimu akija mjini basi atalala kwa Kasella Bantu siku ya pili atarejea Pugu.
Kasella Bantu ndiye aliyempeleka Nyerere kwa Abdul Sykes.
Abdul Sykes alikuwa ndiye Secretary na Act. President wa TAA.
Hicho chama cha TAA kimetokana na African Association chama ambacho baba yake Abdul, Kleist Sykes alikuwa katibu muasisi mwaka wa 1929.
Hakuna mzee yeyote aliyempokea Nyerere alipofika Dar es Salaam kutafuta viongozi wa TAA wala hakuna mzee yeyote aliyemkabidhi Mwalimu chama cha TANU.
Wala Mwalimu hakupata kujulikana hadi pale alipokuja kusuhubiana na Abdul Sykes katika siasa za TAA kuelekea kuundwa kwa TANU.
Hii ilikuwa kati ya mwaka wa 1952 - 1954.
Katika historia ya TANU kutokea TAA wazee waliokuwa ndani ya uongozi wa TAA na wao kushiriki katika kuweka msingi wa kuunda TANU walikuwa Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Said Chaurembo aliyekuwa Liwali Mahakama ya Kariakoo.
Hawa walikuwa wajumbe katika TAA Political Subcommittee ilyoundwa mwaka wa 1950.
Wajumbe wa TAA Political Subcommttee walikuwa Dr. Vedast Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Sheik Hassan bin Ameir, John Rupia na Sheikh Said Chaurembo.
Wala si sawa kusema kuwa Nyerere aliunda TANU.
Historia ya TANU inaanza mbali sana kwa karibu ni mwaka wa 1945 Abdul Sykes, Ally Sykes na askari wenzao katika 6th Batallion KAR Burma Infantry wakiwa Kalieni Camp Bombay hapo ndipo katika mkesha wa Christmas, 1945 walipoamua kuunda TANU kudai uhuru wa Tanganyika na jina hili lilitolewa huko.
Hapo Kalieni Camp askari Waafrika kutoka Afrika ya Mashariki walikuwa wanasubiri kurudishwa makwao baada ya Vita Vya Pili Vya Dunia (1938 - 1945).
Urafiki wa Nyerere na wazee wa Dar es Salaam ulianza baada ya TANU kuundwa 1954 na mzee aliyekuwa karibu sana na Mwalimu alikuwa Mzee Mshume Kiyate mwaka wa 1955.
Ukipenda unaweza ukawaongeza na wengine kama Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi na Max Mbwana.
Historia hii nimeiandika kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).
Kulia ni Mzee Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Mzee Max Mbwana na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi.
Inasikitisha kuwa baada ya uhuru miaka 60 hadi leo hatuijui historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere wala historia ya TANU.
Kulia ni Mzee Mshume Kiyate, Julius Nyerere, Mzee Max Mbwana na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi Uchaguzi wa 1962.