Telewolth bin champion
JF-Expert Member
- Dec 11, 2018
- 2,876
- 7,621
Watu wa aina hii hujifanya wajuaji kila nyuzi wasizoziweza hujibu wakati zipo nje ya uelewa wao, ujuaji wa JF unatia mashaka, mkuu usikate tamaa wapige elimu hawa watu wajue ulimwengu unaendelea wapihukutakiwa kujibu huu uzi kama haujausoma kwa maana unachojibu hakiendani na kichwa wala kiini cha uzi huu
Kuna muda punguza shobo unapoona comment yanguKuna muda kama hujui kitu ni bora kunyamaza na kuwaacha wanaojua watoe maoni yao.
Mtoa mada hajazungumzia FOREX kazungumzia Cryptocurrency aina ya USDT stable coin, ambayo ni tofauti na hayo mambo ya forex,
Na suala hili la Crypto halikwepeki kwa dunia ya sasa, ni ninyi wajinga wachache msiopenda kujifunzaa mambo mapya na technology ndio huona kila jambo utapeli.
Hata hivyo kaongelea mbadala wa uhifadhi wa fedha ktk mfumo wa crypto ili kukwepa matatizo ya huu mfumo wa kifedha uliozoeleka katka mabenki, hajaongelea trading wala huo uhuni wajinga mnaotaka kuhusisha nao.
Acheni utapeli wa kifalahukutakiwa kujibu huu uzi kama haujausoma kwa maana unachojibu hakiendani na kichwa wala kiini cha uzi huu
Mnapojadiligi na kutoa mapungufu ya hii mifumo mipya kwenu mbona huwa hamuilinganishi na hiyo mifumo mizee mnayoitumia kila siku?.Hatua hizi zote zinahitaji uangalifu wa karibu kwani usalama wa kidijitali unaanza na wewe mwenyewe; ni lazima uwashe mifumo ya ulinzi wa hatua mbili kama Google Authenticator au Passkeys kulinda akaunti yako na kuepuka ulaghai wa mtandaoni
Katika andiko lako, hujajadili kwa kina hapo 👆; sana sana unashangaa "old skul" kuendelea kuweka akiba zao benki. Hii ndio aya ulitakiwa ufanue vizuri; fafanua vizuri hapo ili twende sawa. Maswali yafuatayo yanaweza kuongoza.
How safe is the money?
What are the risks?
How would you manage the risks?
Nakubali mada yako ni nzuri na inafikirisha, lakini kuna mambo kadhaa umeyapa uzito mdogo au umeyaacha kabisa.Wakuu salama.
Kuna mada naona inabidi tuichambue kwa jicho la kisomi kidogo, hasa kuhusu jinsi tunavyouza jasho letu wenyewe kwa kuziachia benki za kiasili zishikilie akiba zetu za muda mrefu.
Ukiweka akiba ya Shilingi benki leo, kiuchumi unakutana na vitu viwili vinavyokula mtaji wako kimya kimya: tozo endelevu za kila mwezi kama makato ya kadi, usimamizi wa akaunti, kodi za miamala, na mfumuko wa bei unaoshusha nguvu ya manunuzi ya sarafu yetu. Shilingi inapoteza thamani kila mwaka dhidi ya sarafu ngumu; idadi ya namba kwenye akaunti yako itabaki pale pale, lakini uwezo wake wa kununua rasilimali unashuka kwa kasi.
Mbadala wa kisasa ambao wasomi wengi wamehamia sasa hivi ni ugatuaji wa kifedha kupitia sarafu thabiti, hususan USDT. Kwa wasiofahamu, USDT ni sarafu ya kidijitali ambayo thamani yake imefungwa moja kwa moja na Dola ya Kimarekani, hivyo haina yale mabadiliko ya ghafla ya bei kama yanayoshuhudiwa kwenye Bitcoin.
Ukiangalia kwa upande wa kinga ya mfumuko wa bei, benki za ndani zinatunza Shilingi inayoshuka thamani wakati majukwaa makubwa kama Binance yanatunza USDT, jambo linalofanya akiba yako ilindwe kulingana na mabadiliko ya thamani ya Dola ya Kimarekani hapa nyumbani. Kuhusu gharama, benki inakukata kila mwezi kwa ajili ya usimamizi wa akaunti au kadi, wakati kwenye kipochi cha kidijitali cha Binance unanufaika na gharama sifuri za utunzaji wa salio.
Vilevile, akaunti za amana za benki zina riba ndogo sana zinazomezwa na mfumuko wa bei, wakati mifumo kama Binance Earn inakuwezesha kuweka USDT zikazalisha faida thabiti ya kila siku. Mwisho kabisa, tofauti na urasimu na ukomo wa kutoa fedha benki, soko la Binance P2P linakuruhusu kubadili USDT zako kuwa Shilingi na kuzituma moja kwa moja kwenye akaunti ya simu au benki ndani ya dakika tano tu.
Hatua hizi zote zinahitaji uangalifu wa karibu kwani usalama wa kidijitali unaanza na wewe mwenyewe; ni lazima uwashe mifumo ya ulinzi wa hatua mbili kama Google Authenticator au Passkeys kulinda akaunti yako na kuepuka ulaghai wa mtandaoni.
Mabadiliko ya kiuchumi duniani yanaenda kasi sana na yanahitaji uelewa mpya wa kifedha. Je, unaonaje mwenendo wa tozo na makato ya sasa ya mabenki yetu ya ndani kwenye ukuzaji wa akiba binafsi? Na kwa wale wenzangu na mimi ambao mshahamia kwenye Binance na USDT hapa bongo, mnakutana na changamoto gani za kiutendaji au za kueleweka katika mazingira yetu? Weka maoni yako hapa chini tuchambue.
Hakuna utapeli hapo, kajifunze USDT ni nini? Hiyo ni njia ya kuhold dola ya marekani kidigitali. Full stop, unaweza kununua USDT kwa njia ya benki, au mobile, kulingana na exchange rate ya siku hiyo.Acheni utapeli wa kifala
Mkuu mbumbavu haelekezwi unapoteza energy yako tuHakuna utapeli hapo, kajifunze USDT ni nini? Hiyo ni njia ya kuhold dola ya marekani kidigitali. Full stop, unaweza kununua USDT kwa njia ya benki, au mobile, kulingana na exchange rate ya siku hiyo.
USDT zako zitabaki na thamani ya USD ya siku unapotaka kutoa/kuuza.
Wala mleta mada hajasema anakuunganisha au kwamba utapata faida umtafutie watu!
Uko sahihi mkuu Thanks for your appreciationMnapojadiligi na kutoa mapungufu ya hii mifumo mipya kwenu mbona huwa hamuilinganishi na hiyo mifumo mizee mnayoitumia kila siku?.
Mbona hamzungumzii utapeli ktk mifumo ya kifedha kwenye mitandao yenu ya simu/mabenki, kila siku mamia ya watu wanatapeliwa/kuibiwa/kupotelewa na fedha zao ktk mifumo hiyo hiyo mliyozoea mbona hamlalamiki?.
Ktk mifumo hiyo hiyo ya fedha japokuwa mnasema ina ulinzi then why bado mnaibiwa/kutapeliwa?, wengine fedha zenu wenyewe lkn bado mnapata shida kuziaccess kisa sababu mbalimbali za kijinga kutoka kwa hao wenye mifumo ya kifedha.
Imefika wakati ni hatari kutunza pesa ktk simu/benk maana kila siku inapungua kwa makato ya kihuni.
Jambo msilolijua ni kuwa kila kitu kinapoletwa ktk jamii kuna wajuaji hutumia mianya ya ujinga wa watu kuwatapeli kupitia mfumo huo huo either kuna mwanya ktk mfumo au ujinga wa watu, ndivyo hata ktk CRYPTOCURRENCY na FOREX kuna aina hii ya utapeli.
suala la msingi kwa sasa ni watu kujifunza mfumo huu wa crypto jinsi unavyofanya kazi na umuhimu wake ktk maisha na sio kuukwepa maana mbeleni muda mfupi ujao utakuwa mfumo wa lazima ktk mambo mengi ambayo hamjatarajia.
Hawa wajinga wachachd ndoWatu wa aina hii hujifanya wajuaji kila nyuzi wasizoziweza hujibu wakati zipo nje ya uelewa wao, ujuaji wa JF unatia mashaka, mkuu usikate tamaa wapige elimu hawa watu wajue ulimwengu unaendelea wapi
Watu kama hawa wajinga wajinga sio wa kuwapa kipaumbele mtu ashazoe kuongea na mademu zake/mashoga zake 24hrs :nimekumis nimekumis pia" hana time na uwelewa wa masuala ya kiuchumi so automatically hawezi kujadili professional topic kama hizi kutokana na akili yake ndogoKuna muda kama hujui kitu ni bora kunyamaza na kuwaacha wanaojua watoe maoni yao.
Mtoa mada hajazungumzia FOREX kazungumzia Cryptocurrency aina ya USDT stable coin, ambayo ni tofauti na hayo mambo ya forex,
Na suala hili la Crypto halikwepeki kwa dunia ya sasa, ni ninyi wajinga wachache msiopenda kujifunzaa mambo mapya na technology ndio huona kila jambo utapeli.
Hata hivyo kaongelea mbadala wa uhifadhi wa fedha ktk mfumo wa crypto ili kukwepa matatizo ya huu mfumo wa kifedha uliozoeleka katka mabenki, hajaongelea trading wala huo uhuni wajinga mnaotaka kuhusisha nao.
yeah uko sahihiKwa anaepata mashaka juu ya utunzaji wa fedha aidha bank au kwenye mifuko ya pesamtandao/cryptocurrency wallet.. fanya hivi nunua dhahabu itunze hiyo dhahabu!.
Hii mali hainaga mambo yakupoteza thamani bali kupanda tu, ipo stable na haiharibiki kirahisi
Safi sanaNakubali mada yako ni nzuri na inafikirisha, lakini kuna mambo kadhaa umeyapa uzito mdogo au umeyaacha kabisa.
◾️USDT si dola halisi.
USDT ni ahadi ya kampuni ya Tether kwamba wana dola halisi kwenye reserve. Kwa miaka, wamekuwa wakikabiliwa na maswali ya kutosha kuwa na reserve kamili. Ikiwa Tether itaanguka, upo uwezekano wa mteja kubaki na sufuri, kwa sababu kampuni ya Tether haina deposit insurance. Benki zina bima ya amana (up to a specified limit).
◾️Binance si salama kama benki.
Binance imekuwa ikishtakiwa na kufungiwa katika nchi mbalimbali kwa kukosa kufuata sheria za fedha. Akaunti yako inaweza kugandishwa kwa urahisi ikiwa wataona shughuli zenye utata. Pia, hakuna mtu wa kumwita au ofisi ya kwenda ukikumbana na tatizo—tofauti na benki yenye matawi.
◾️P2P ina hatari zake.
Wewe unasema P2P inachukua dakika tano. Lakini kwenye uhalisia, watu wamepoteza pesa kwa kupokea malipo kutoka kwa akaunti za wizi, au kwa kukutana na wadanganyifu wanaotuma confirmation za uongo. Pia, benki yako hapa Bongo inaweza kukufungia akaunti ikiwa itaona unaingiza pesa mara kwa mara kutoka kwa watu wasiojulikana—na huo utaratibu wa kuuliza maswali ni kero kama ile ya benki unayoitukana.
◾️Gharama za Binance sio zero.
Unasema hakuna gharama za utunzaji wa salio, lakini unakosa kueleza kuwa kila unapotuma USDT au kubadilisha, kuna network fees. Kwa mfano, kutoa USDT kwenye TRC20 kunakula $1-2 kwa kila muamala. Ukibadilisha USDT hadi Shilingi kwenye P2P, spread ya bei inaweza kuwa kubwa kuliko tozo za benki kwa mwezi mzima.
◾️Uchumi halisi unahitaji Shilingi.
Huwezi kulipa bills za maji, umeme, chakula, au kulipa karo kwa kutumia USDT. Kama ukiweka akiba yako yote kwenye USDT, wakati wa dharura utalazimika kubadilisha kwa haraka—labda kwa bei mbaya au kwa mtu asiyeaminika. Ukishindwa kupata mnunuzi wa P2P usiku wa manane, utakosa chochote. Benki unatoa kadi au simu ukapata pesa papo hapo.
◾️Riba ya Binance Earn sio uhakika.
Unasema Binance Earn inatoa faida thabiti ya kila siku, lakini kiuhalisia hizo fursa za kujaza USDT kwenye "flexible savings" au "lending" zina hatari zake. Binance inaweza kubadilisha viwango, au kama kuna shida ya soko, wanarudisha pesa yako polepole au kwa masharti magumu. Benki ingawa riba yake ni ndogo, haina hatari ya kupoteza mtaji wako mkuu.
Mfumuko wa bei na tozo za benki ni changamoto za kweli, lakini kukimbilia kwenye USDT na Binance kwa akiba zako zote ni kubadilisha hatari ya mfumuko wa bei kwa hatari kubwa zaidi ya kupoteza kila kitu. Mtu mwenye busara atatumia a prudent approach: akiba kidogo benki kwa matumizi ya kila siku, akiba kidogo kwenye USD halisi (au USDT kwa anayeelewa hatari), na si kuweka mayai yote kwenye kikapu kimoja.
Unachosema kina manufaa kwa mtu anayejua sana teknolojia na hatari za crypto, lakini kwa mtu wa kawaida, bado benki ni salama na rahisi zaidi.
Nje ya JF utaweza kunitukana?Get off your fucking ass hole
Tuma namba yako PM tufahamianeKulikua na haja gani ya kuniita fala hapo juu kama ulikua huitaji conflict
Ni maarifa tu bro, ukijua vizuri kutumia Binance app utachukua bank na mifumo ya cash. Pakua app ya binance na tuendelee kujifunza kuitumia🤔🤔🤔🤔 hizi mambo ni nzuri kuzisoma tu kwangu nitaangaika na Cash au bank ninazofahamu sitaki kuja kulia mimi.
Mkuu nishapiga project na hao binnace ofisi yao ya recruiting Iko Rwanda ukweli kunahitajika usimamizi wa serikali tuNi maarifa tu bro, ukijua vizuri kutumia Binance app utachukua bank na mifumo ya cash. Pakua app ya binance na tuendelee kujifunza kuitumia
Ofisini tena! Binance si ni application, ofisini inahusika vipi hapo? Achana na ofisini physically, application yenyewe inajitosheleza, unabadili cash yako kuwa usdt au stable coin yoyote unatunza pesa zako bila stress ya makato ya benki zetu na mifumo ya jadiMkuu nishapiga project na hao binnace ofisi yao ya recruiting Iko Rwanda ukweli kunahitajika usimamizi wa serikali tu