Kwanini Balozi Mulamula alikuwa anaonekana smart sana na kuheshimika huko Ugenini?

Siyo kazi ya watanzania kujipendekeza kwa wazungu
 
na magufuli nae vipi alikuwa anaheshimika ulaya!
 
Ukiona hivyo anauza ramani... marekani hawakupendi bure....
 
Wamrudishe Kalemani aisee, watanzania wanataka umeme wa elfu 27 tena unaopatikana muda wote.
 
Mbona kafupi hivyo?? Hata salama ngale ni tolu kwake...
 
Ila huyu mama binafsi nikimsikiliza akiwa anaongea sielewi anaongea nini yupo smart ila hakua na Karama ya uzungumzaji.
Kwani uwaziri ulitaka awe Smart? Alimshinda Prof Kalamaganda?
 
Balozi Mulamula ni "top Diplomat" na ni mtu muhimu sana na hazina kwa taifa letu.

Ushauri wangu kwake ni kubakia hukohuko US na arudi kufundisha au aandike vitabu zaidi vinavohusu diplomasia ya kimataifa.
 
Hatutaki wanasiasa walio karibu na mabeberu. Nchi hii ni nchi yenye sera ya Ujamaa na tunaongozwa na wana mapinduzi (revolutionaries).
 
Keshaliwa kichwa,mwambie aheshimike na Sasa basi
 
Hatutaki wanasiasa walio karibu na mabeberu. Nchi hii ni nchi yenye sera ya Ujamaa na tunaongozwa na wana mapinduzi (revolutionaries).
Ni ukaribu upi huo?

Mtu kaishi kule na ana connections lukuki na pengine urefu wa kamba yake ni ndogo sana au pengine hana kabisa.

Tatizo ni lipi?
 
Nimejaribu kuitafakari kwa kina hii habari yako ili niielewe vizuri. Bila shaka wasomaji wengi hawataelewa ulichoandika hapa.

Lakini hii "hazina ya viongozi wenye weledi" mbona wanaliangusha taifa lao kiasi hiki? Kwa weledi wao huu, kwa nini wasijitokeze mbele sasa na kusema imetosha kwa taifa letu kufanywa kama dimbwi la walevi?

Huu weledi wao nadhani itafika mahali tuutilie mashaka.

Naomba unielewe vyema. Sikatai kwamba kuna watu 'smart' kabisa ndani ya nchi hii wasiopenda kuyumbishwa na hawa wapuuzi wanaoshika madaraka na kuyatumia visivyo. Ila nadhani kuna umuhimu sasa wa hawa watu 'smart' kusema imetosha; hatuwezi kuendelea kuiacha Tanzania ikitumiwa kama jalala.
 
U smart unafutwa na kuharibiwa na wizi wa hii mijitu. Nachukia wizi from basement of my heart
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…