Mwaka 1775 wakati makoloni 13 ya Uingereza huko America yanajitangazia uhuru kutoka kwa Uingereza iliundwa
Kamati ya watu 5 au
The Comittee of Five iliyoundwa kuandaa mkataba wa kujitangazia Uhuru wa makoloni yao 13 au
United States Declaration of Independence. Hii kamati ilihusisha
- John Adams
- Thomas Jefferson
- Benjamin Franklin
- Roger Sherman
- Robert Livingston
Hii kamati iliundwa na watu 7 waliokuwa na ushawishi mkubwa kwenye hayo makoloni wakati huo. Watu hao ndio wanajulikana kama
Founding Fathers of the United States nao ni
- John Adams
- Benjamin Franklin
- Alexander Hamilton
- John Jay
- Thomas Jefferson
- James Madison
- George Washington
Hawa Founding fathers ndio walisaini mkataba kusitisha vita uliojulikana kama
Treaty of Paris. Baada ya kupata uhuru wao, wakaitisha Bunge la Kwanza kabisa (
United States Congress) ili kuunda serikali ya kwanza na katiba yao kuirekebisha.
George Washington ana tambulika kama
Father of the Nation sababu alikuwa Jemedari (commander in chief) wakati wa mapigano. Baada ya kumalizika na wamepata uhuru, aliachia ngazi jeshini na sehemu zote ili Mkutano uamue nani kuwa kiongozi wa nchi yao huru sababu hakuwa anataka uongozi yeye alipigana ili wawe huru. Lakini kutokana na mchango wake na alivyokuwa anapendwa, Electoral College waliamua kumfanya kuwa Raisi wao wa kwanza (First president of the United States of America).