Mkuu unachotakiwa kufahamu ni kuwa Waarabu hawakuleta wala kuanzisha biashara ya utumwa Afrika Mashariki na Kati. Sisi magwiji wa historia tunafahamu kuwa utumwa ulikuwepo Afrika Mashariki na Kati kabla ya karne ya saba ambapo Waarabu walianza kuja. Kuna makabila yalikuwa yanamiliki watumwa yaani slave owning societies kwa mfano Wanyakyusa, Wanyamwezi na wengineo (Rejea: Development of East African Societies to the ninteeth and twentieth Century kilichotolewa na TIE enzi zile kilikuwa na jalada jekundu, mimi nilikisoma 1994). Kwenye hicho kitabu kilichoandikwa na wataalam wetu zimetajwa jamii zote zilizokuwa zina mfumo wa utumwa. Mwarabu alipokuja aliukuta utumwa upo na yeye akaingia kwenye hiyo biashara akiuziwa na machifu.
Unachotakiwa kuelewa ni kuwa utumwa ulikuwa ni mfumo wa maisha na ulikuwepo duniani kote hata Ulaya. Ila hakuna biashara mbaya ya utumwa kama ile ya Trans Atlantic Slave Trade. Nenda kasome kitu inaitwa Horrors of the Middle Passage uone unyama waliokuwa wakiufanya wazungu dhidi ya watu weusi. Ukipata muda ingia maktaba kule UD utaona encyclopedia kibao kuhusu Trans Atlantic Slave Trade na volumes zingine utashangaa jinsi walivyotunza rekodi za unyama wao.
Sasa wewe gwiji wa historia mbona unatoa taarifa nusunusu tu. Halafu kwanini wewe gwiji wa historia unitajie chanzo kimoja tu cha historia ??? Hili naliacha najikita kwenye hoja ya msingi.
Machifu wa kiafrika kufanya biashara ya utumwa hakuwaondoi waarabu, wazungu wala jamii yoyote ile kwenye uwajibikaji wa huu unyama. Utumwa ni ushenzi wa hali ya juu sana, haijalishi umefanywa na nani.
Halafu sasa nadhani umejikita kwenye mfumo wa uzalishaji (MODE OF PRODUCTION), hii inaonyesha wewe ni mhanga mkubwa wa elimu ya kijamaa. You have allowed Marxism to shape your understanding of history.
Lakini kwasababu umeileta hii hoja basi ntakujibu kupitia hii hoja. Mfumo wa utumwa barani Afrika japo ni mfumo dhalimu, ulikuwa wa tofauti na sehemu nyingine yoyote ile duniani. Afrika walikuwa na utumwa wa kazi (Domestic Slavery), utumwa wa deni (Debt Slavery/Indentured Labour), Utumwa wa vita (War Slavery), Utumwa wa ngono (Prostitution Slavery) na Utumwa wa uhalifu (Criminal Slavery).
Sasa kama wewe umesoma vizuri historia utafahamu jambo moja muhimu: Watumwa wengi wa Afrika walikuwa wanakuja kuwa wanajamii baada ya muda fulani kupita. Hili ndilo lilichangia sehemu nyingi za bara la Afrika kuruka haraka au kutopitia kabisa mfumo wa uzalishaji wa utumwa (Slavery Mode of Production) kwenda kwenye mfumo wa Ukabaila (Feudal Mode of Production).
Waarabu na Wazungu wamefika hapa Afrika, tayari tulikuwa kwenye mfumo wa Ukabaila. Kama umesoma vizuri historia ya tanzania ndiyo utasikia mambo ya ubwanyenye, unyanyembe na umwinyi: Yote hii ilikuwa ni mifumo ya ukabaila na siyo utumwa kama wewe gwiji wa historia unavyotaka kuniaminisha hapa.
Utumwa uliokuwepo Ugiriki, Roma, Uturuki na Uarabuni ulikua utumwa wa mtu-bidhaa (Chattel Slavery), yaani mtu anakuwa mali ya mwenzake ambayo inaweza ikaingizwa sokoni. Sehemu chache za Afrika kama Ufalme wa Kongo ulikuwa na haka kamfumo, japo wenyewe walikuwa wanauza mateka wa vita.
Sasa kabla sijahitimisha, nataka kukupa chakula cha ubongo wewe gwiji wa historia (The Self Appointed Master of History) kwamba utumwa mbaya Afrika haukuwa ule wa bahari ya atlantiki (Trans-Atlantic Slave Trade) wa kuuza watu weusi, bali pia utumwa wa kibabari (The Barbary Slave Trade) ambao uliuza maelfu ya wazungu kwa mabwana wa kiarabu. Huu utumwa ulikuwa chini ya masultani wa kituruki na kiarabu wa Tunisia na Morocco.
Hili halipo kwenye mtaala wetu, na inabidi liwepo maana ni jambo muhimu sana. Watoto wanatakiwa wasome ili wafahamu madhara yake.
Mwisho kabisa, nadhani uko chini ya fikra kwamba mimi nawachukia waislamu na waarabu, nikitetea wazungu. Nadhani huku ni kushindwa kufanya mijadala kisomi na kiuwazi: Kitu kinachoitwa UTUMWA ni laana kabisa, uwe umefanywa na mwafrika, mzungu, mwarabu au mchina. Tena ni jambo la kishenzi kama utakuwa ulifanywa na watu ambao wana dini hizi kubwa kama ukristo na uislamu.
Leo nikitetea utumwa kisa ulifanywa na wahaya, wanyakyusa na wahehe kisa mimi ni mweusi AU ulifanywa na viongozi wa kidini kama Papa na Wafalme wa Ulaya ambao ni wakristo basi MIMI NAMI NITAKUWA MSHENZI MSHENZI TU, tena siyo mshenzi tu bali Mshenzi Baradhuli.
NB: Tunaposoma historia tunazingatia mambo mengi sana kama The Cultural Side, The Philosophical Side, The Moral Side, The Metaphysical Side na siyo The Factual Side only. Tena sisi wasomi wa kiafrika tunapochambua historia au fasihi lazima tuzingatie kitu kiitwacho NEGRITUDE kinacholenga kuwafanya watoto wetu waheshimu utu wao wa kiafrika siyo blah blah tu.