Neno BIBLIA lina maana ya mkusanyiko wa vitabu na ndani ya mkusanyiko huo kuna maandiko ya AGANO LA KALE na maandiko ya AGANO JIPYA.... Maandiko ya AGANO LA KALE ni mengi sana yamepangiliwa vyema na ni rahisi sana kueleweka kuliko maandiko machache ya AGANO JIPYA... Ndio maana Wasabato na Waislamu wengi wanayakubali sana maandiko ya AGANO LA KALE kuliko maandiko ya AGANO JIPYA.🙏
Ukisoma kitabu cha AGANO LA KALE kuanzia MWANZO hadi MALAKI unaweza kuwafahamu vyema wahusika wote na hata koo zao.👉 Lakini ukisoma kitabu cha AGANO JIPYA utaona waandishi wamelipua au wameunga unga vipande vya maandishi wala huwezi kukuta kurasa walau 4 zinaelezea kitu kimoja. Stori hazijitoshelezi
Kuanzia MATHAYO mpaka UFUNUO... Utakutana na stori au hadithi zilezile chache zinazofanana harafu utakuta mwandishi ktk AGANO JiPYA, anasema eti "Kuna mambo mengi aliyofanya Yesu, ambayo yakiandikwa mojamoja nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa" YOHANA 21:25.
Je, hii ilikuwa ni kweli? Waandishi walijisahau au waandishi waliamua tu kufanya makusudi Kwa lengo Yesu asiweze kusomeka kwa mambo mengi ambayo mengineyo (huenda) yangedhoofisha 'Utakatifu' 'Unabii' 'Uana wa Mungu' au 'Uungu wake?' Maana haiwezekani waandishi kama MATHAYO, MARKO, LUKA na YOHANA... Wakajikuta wote kwa pamoja wanaandika jambo lilelile kumhusu Yesu, bila ya kusimulia story tofauti wakati kila mmoja aliandika INJILI kwa wakati wake.
Kwamfano... MATHAYO angeandika INJILI yake kwa ufasaha kabisa kuhusu uzao wote wa Yesu uzao wa wazazi wake pamoja na ndugu zake wote. Kisha MARKO naye angeandika INJILI yake historia ya maisha ya Yesu kuanzia alipofikisha umri wa miaka 12 mpaka 29 kwamba (Yesu) alikuwa anaishi wapi, alikuwa anapendelea kufanya nini na nini na alipofikisha umri wa kufanya kazi alifanya kazi gani?
LUKA na YOHANA pamoja nyaraka kadhaa za akina Mtume PAULO... Wenyewe wangeandika kama hivi walivyoandika kazi za Yesu alipoanza kuhubiri INJILI akiwa na umri wa miaka 30... Naamini vitabu vingetosha kabisa na sisi wasomaji tusingechoka kuvisoma na wala tusingefikia hatua ya kutofautiana hata kuzalisha madhehebu mbalimbali ya kidini.
Angalia jinsi waandishi wote wa AGANO JiPYA walivyoacha kuandika Siku, Tarehe, Mwezi na hata Mwaka aliozaliwa Yesu... Watu wengine baadae walipokuja kusema kuwa "Yesu amezaliwa Desemba 25" Ndipo Wasabato na Waislamu walipoamua kupingana ktk hilo... Na sio ktk hilo tu...Hata kwenye masuala ya ulaji wa nyama ya Nguruwe, siku maalum ya kuabudu Mungu, Kufunga mwezi mtukufu, Sikukuu ya Pasaka na hata kuoa, kuolewa na Talaka... AGANO JIPYA halifafanui kwa uwazi kama ilivyo AGANO LA KALE.
Mitume na Manabii wote walioandikwa ktk kitabu cha AGANO LA KALE wametajwa kwa uwazi majina ya wazazi wao wote mpaka ndugu zao... Lakini ukisoma kitabu cha AGANO JIPYA ni vigumu sana kukuta majina ya wazazi wa mama yake Yesu na vigumu sana kukuta majina halisi ya ndugu zake Yesu. Ingawa inasemekana Yesu alikuwa na mama zake wadogo, Shangazj zake, Wajomba zake, Kaka na Dada zake...
Pia alikuwa na Babu pamoja na Bibi zake ambao wanatajwa kuwa ni (Anna na Yoakimu), lakini ndani ya AGANO JiPYA hawakuwekwa wazi.
Vilevile si rahisi kukuta ktk AGANO JIPYA imeandikwa kazi alizofanya Yesu (kabla hajaanza kuhubiri), si rahisi kukuta imeandikwa kama Yesu alikuwa na mke au mpenzi au alikuwa hana kabisa AGANO JIPYA limekwepa kabisa kuandika yote hayo, ingawa inatambua wazi Yesu alikuwa ni mwanadamu mkamilifu kama walivyo wanadamu wengine... Alikuwa Analala, Anakula na Kunywa, Alikuwa anavaa Nguo. Alikuwa anajisaidia haja ndogo na kubwa... Alikuwa anachukia na kufurahi... Alikuwa anachoka, Alibatizwa, Alitahiriwa, Alikuwa anasali na kuomba Dua na pia alikuwa na matamanio kama walivyo wanadamu wengine (maana alitamani hata kula matunda ktk mti fulani) na alipokuta matunda hakuna Yesu alichukia.
Kama ukisoma kwa kuunga unga maandiko ndani ya AGANO JIPYA, utagundua kuwa akina YUDA walikuwa wawili na mmoja ni ndugu yake Yesu. Akina Mariamu walikuwa watatu ambapo mmoja ni mama yake mzazi, wa pili mama yake mdogo na wa tatu ni Mariamu Magdalena (ambaye amezua gumzo sana ulimwenguni). Pia utagundua Simeoni Petro, Andrea, Yakobo, Yohana, Yuda, Yosefu au Yusufu, Salome na Yohana walikuwa ni ndugu wa mama mmoja (Mariamu mama yake mdogo Yesu) lakini baba tofauti. Lakini Yohana Zakaria alikuwa ni kaka wa Yesu (mtoto wa mama yake mkubwa Elizabeth).
Unga unga maandiko haya ili kuwajua ndugu wa Yesu: MATAYO 13:55 👉 MARKO 6:3 👉 LUKA 6:13:16 👉 MARKO 15:40 👉 LUKA 24:10 👉 MARKO 1:29 👉 YOHANA 19:25 👉 MATENDO 12:12:17 👉 MATENDO 12:2 na YUDA 1:1. Petro na Andrea baba yao ni Yohana. Yakobo na Yohana baba yao ni Zebedayo.
Bado kuna hili la mafumbo! Katika AGANO JIPYA kuna maandiko mengi yenye muundo wa Mifano, Methali na Mafumbo... Ambayo ni vigumu kwa watu wengi kuelewa wakati kitabu chenyewe kimatafsiriwa katika llugha zote za ulimwengu... Mfano ni INJILI ya YOHANA INJILI hii ndio imehusika zaidi kumficha mwanafunzi aliyependwa na Yesu bila ya kumtaja jina mpaka mwisho. Je, lengo hapa lilikuwa nini?
AGANO JIPYA haikuandika wazi kusema kama Yusufu na Mariamu (baada ya posa) walioana? Waliendelea kuishi pamoja hadi kifo kilipowatengenisha? Walizaa watoto wengine tofauti na Yesu? Je, walikufa wakiwa na umri wa miaka mingapi? Walizikwa wapi?
AGANO LA KALE wamezingatia kuandika yote haya... Lakini AGANO JIPYA limepuuzia Ndio maana watu wengi wanajikuta wakisema: "INJILI ni ngumu sana kuielewa mpaka uvuviwe na Roho Mtakatifu" MATENDO 19:13: 20 na MATENDO 8:9:25 🙏
Je, waandishi wa AGANO JiPYA walijisahau au waliamua tu kufanya makusudi kutoandika kweli yote?